Mwenyekiti tume ya lukuvi naye ni fisadi wa masuala ya ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti tume ya lukuvi naye ni fisadi wa masuala ya ardhi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Jatropha, Jun 21, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Wiki iliyopita Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam Mhe William Lukuvi alivamia ofisi za kitengo cha ardhi katika Manispaa ya Kinondoni na kuamuru Mkuu wa kitengo hicho kuwekwa rumande baada ya kutoridhishwa kuhusu maelezo yake kuhusu uuzaji wa viwanja va wazi hapa Jijini. Aliagiza pia milango ya ofisi hiyo pamoja na zile za Manispaa ya Ilala na Temeke kufungwa katika kile kinachodaiwa kuzuia watumishi husika kupoteza ushahidi wa vitendo vya uuzajji maeneo yaliyo wazi na ufisadi mwingine wa ardhi.
  Mkuu wa Mkoa pia aliunda Tume ya watu 7 (saba) kufanya ukaguzi na kubaini vitendo vya kugushi na ufisadi mwingione unaohusu masuala ya ardhi katika Manispaa zote tatu. Tume hiyo inaongozwa na Mkurugenzi wa Mipango Miji katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Albina Burra.

  Jina la Bibi Albina Burra sio geni masikioni mwa wakazi wa Kata ya Kibamba hususan Mitaa ya Luguruni, Kwembe Kati n.k katika Manispaa ya Kinondoni. Kati 2007 hadi sasa Bibi A Burra na timu ya wataaamu kutoka Wizara ya Ardhi walitenda ufisadi mkubwa sana wa ardhi kupitia Mradi wa uendelezaji wa maeneo yaliyoko pemebezoni mwa Jiji la Dar es Salaam (Luguruni Satellite City) ambapo fedha nyingi sana za serikali zimefujwa kwa njia za ulipaji fidia hewa, watumishi kulipwa posho na masurufu kana kwamba wanasafiri mikoani ilihali wanakwenda kufanya kazi hapa hapa jijini n.k. Inahofiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 3 (Tatu) za Serikali zilifujwa.

  Chini wake wanakaya 259 waliokuwa wakiishi eneo la Luguruni walilipwa fidia kwa kutumia fedha na hundi za Serikali pasipo kuwa wamefanyiwa uthamini wowote wa mali zao, na kasha kutakiwa kuhama kupisha utekelezaji wa mradi huo ndani ya siku 30 tu. Sheria ya Ardhi Namba 4 na % za 1999 zinataka mwanachi kupatiwa notisi ya siku 90 endapo anatakiwa kuhama kutoka katika ardhi/makazi yake. Hivyo kwa kuwapatia wakazi hao notisi ys siku 30 tu Bibi A Burra na timu yake walienga kuficha ubadhirifu wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ulipaji fidia wakazi hao.

  Kati ya wananchi hao wapo wachache waliotumiwa na watumishi wa Wizara ya Ardhi chini ya Bibi A Burra kuchukua fedha nyingi sana za fidia wakidai kuwa wanamiliki majengo yenye thamani ilihali ukweli ni kwamba walikuwa wakimiliki vibanda vya nyasi tu. Aidha watumishi waliokuwa chini ya Bibi A Burra walichukua picha za majengo mbali mbali na kuzitumia ckuchota fedha za fidia katika viwanja vitupu na fedha zote hizi kuishia mifukoni mwa watumishi wasio waaminifu wa Wizara ya Ardhi waliokuwa chini ya Bibi Albina Burra.

  Bibi A Burra na timu yake waliwalipa wakazi wa Luguruni fedha kidogo sana takribani Shilingi 300 kwa Mita Moja ya Mraba ya Ardhi mwaka 2007. Malalamiko makubwa ya wanachi yalimfanya Waziri wa Ardhi wa wakati huo Mhe John Magufuli kutembelea eneo la Luguruni na kuagiza uchunguzi kufanyika na akamkabidhi mwakilishi wa Kamanda Tibaigana orodha ya walipwaji fidia wote kwa uchunguzi zaidi.

  Kuhamishwa kwa Waziri Magufuli kutoka Wizara ya Ardhi kuliwapatia nafuu Bibi Albina Burra na timu yake ya watumishi wasio waaminifu. Baadaye mwaka 2008 (zaidi ya miezi 9 kutokea wakazi wa Luguruni kupatiwa malipo bila ya kufanyiwa uthamini wa mali zao ) Serikali ililazimika kuingia gharama upya za kulipwa watumishi, magari na posho ili kufanya uthamini wa mali za wakazi wa Luguruni na hatimaye kuwalipa fidia kwa kiwango kipya cha Shilingi 1800 kwa Mita Moja Mraba; ikiwa ni 600% ya kiwango kilichotumika awali.

  Kwa maneno mengine kwa kitendo cha Bibi Albina Burra na timu yake kuwataka wana kaya 259 wa eneo la Luguruni wahame kutoka katika makazi yao ndani ya siku 30 tu huku wakiwa wamewalipa fidia pungufu kwa kiwango cha 600% kilikuwa na cha wizi na ubadhirifu na ufisadi kwa kuwa laiti wakazi hawa wangekubali kuhama kimya kimya kama wafanyavyo wanachi wengi wangepoteza ya fidia kwa kiwango cha 600%.

  Hadi sasa hakuna hata mtumishi mmoja wa mradi huu aliyechukuliwa hatua zozote za kinidhamu wala kisheria kwa kuisababishia serikali hasara kwa kulazimika kurudia zoezi la uthamini upya.

  Licha ya kiwango cha fidia kuongezwa bado kiliendelea kuwa kidogo sana na kuwatumbukiza wakazi hao katika lindi la Umaskini, wengi wao walilazimika kwenda kuishi maisha duni katika maeneo yasiyipimwa na yasiyo na huduma za kijamii kama vile maji, shule, n.k. Baadaye 2009 Wizara ya Ardhi iliuza ardhi iliyotwaa kutoka kwa wananchi hao pasipo maendelezo yoyote kwa bei ya kati ya Shilingi 25,000/= hadi 30,000/= kwa Mita Moja Mraba. Huu ni ufisadi mkubwa kuwahi kutekelezwa na watumishi wa Serikali kwa jina na mgongo wa Serikali na uliratibiwa na Bibi Albina Burra.

  Baada ya kumaliza ufisadi katika eneo la Luguruni, timu hiyo ikawageukia wananchi wa eneo la Kwembe Kati na kuwanyang’anya ardhi yao kwa kisingizo kuwa wanapitisha miundo mbinu na kuwalipa fidia kidogo sana kwa kiwango cha Shilingi 1800 kwa Mita Moja Mraba. Baada ya hapo Timu ya Bibi A Burra ikapima viwanja katika ardhi na makzi ya wananchi wa Kwembe Kati pasipo kujali Master Plan iliyokuwepo, hati miliki zilizokuwepo n.k Na kasha kuwauzia wananchi hao ardhi hiyo hiyo pasipo maendeleo yoyote kwa kiwango cha Shilingi 6500 kwa Mita Moja Mraba.

  Katika upimaji viwanja eneo la Kwembe Kati timu ya Bibi Albina Burra (Mkurugenzi wa Miapngo Miji Wizara ya Ardhi) walitenganisha nyumba za wakazi wa Kwembe Kati na visima vyao vya maji, maegesho ya magari, mabanda ya mifugo na hata vyoo. Huu ndio utendaji wa Mkurugenzi wa Mipango Miji anayetarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Lukuvi!!!!!

  Kutokana na utendaji wa ubabaishaji wa Bibi Albina Burra na timu yake Serikali imelazimika kusimamisha utekelezaji wa miradi ya Luguruni na Kwembe hadi hapo mapungufu yaliyojitokeza yatakaporekebishwa; hali hii itaiingiza hahsara kubwa Serikali kutokana na kazi za marudio.

  Kwa upande wa Mradi wa Luguruni tarehe 21 Mei 2010 Serikali ililazimika kutangaza kutafuta Mshauri Mwelekezi ambaye pamoja na mambo mengine atatayarisha Mater Plan ya eneo husika. Hii ikiashiria kuwa Mkurugenzi Mipango Miji wa wizara ameshindwa kutayarisha “a workable Master Plan” .

  Kwa upande wa Kwembe Kati Serikali inafanya uchunguzi wa kina kuhusu madai makubwa ya ufisadi uliojitokeza.

  Hivyo kuwepo kwa Bibi Albina Burra ndani ya Tume ya Lukuvi kutawasaidia zaidi maafisa wanaotuhumiwa kuliko Serikali na Wananchi wake kwa kuwa ni mtu ambaye ana tabia ya kupotosha ukweli, hivyo atatumia nafasi yake kama mtaalamu wa Mipango Miji kuwapotosha wajumbe wengine kwa nia kuwanusuru maafisa wanaotuhumiwa.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mhhh haya yetu masikio na macho..huku sinza ndo balaaaaa Diwani wa huku kauza mpaka sehemu iliyopita mtaro wa maji.....sijui itakuwaje
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa mkoa amepotoka, mtu wa ardhi wizarani kuchunguza maovu ya Watendaji wa ardhi Ilala, Kinindoni na temeke ni sawa na kesi ya ngedere kuamuliwa na nyani.
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  rais kikwete fisadi namba moja yeye na akina rostamu la zizi na mamvi, mkuu wa mkoa fisadi la elimu, someni kitabu cha msema kweli, sasa na sasa albina bura, naomba kuikana nchi hii na kusubiri mabadiliko nikiwa raia wa nchi ingine, aibu, aibu, aibu
   
 5. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nataraji lukuvi hatofanya hili jambo kumnufaisha kisiasa, ardhi pamekuwa hovyo kuliko mahali popote pale tz hii, na wakuu wamefumba mamcho kwa mda mrefu sana! hii inatokana na kutokuwa na job rotation katika serikali yetu!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Salum Abdallah Mwaking'inda......pia katibu mwenezi CCM.....kamrithi yule Manara aliyetimuliwa kwa utapeli na mwenye kesi nyingi mahakamani....huyu Salim naye kakamatwa jana na Londa....sasa sijui hawa CCM wanateuana vipi......
   
Loading...