Mwenyekiti taifa chadema freeman mbowe na joseph mbilinyi mbunge wa mbeya mjini-ndani ya houston tx

Pro-Chadema wana mambo ya kizamani sana sasa kuweka picha ya Mbowe na maghorofa ya Marekani ndio nini utadhani msanii wa bongo movie.

Utazoe tu mwaka huu halali mtu mpaka kieleweke tunapiga kotekote. Furaha ya CDM wananchi ndio wameikubali na ninyi wenzetu mnanunua wananchi kwa sinia za wali na kanga.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Joseph Mbilinyi mbunge wa Chadema kuweni na uzalendo mnaondoka Tanzania mnaacha zoezi la sensa mnakwenda kufungua tawi Marekani.
Hivi na wewe unaunga mkono SENSA? Kweli Tanzania imejaa wasaliti
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Joseph Mbilinyi mbunge wa Chadema kuweni na uzalendo mnaondoka Tanzania mnaacha zoezi la sensa mnakwenda kufungua tawi Marekani.

Mbona hawa viongozi wetu wengine wametuambia tugomee sensa yenyewe. Kwahiyo haipo....
 
Usijali mkubwa watahesabiwa hata wale walioko masomoni nje watahesabiwa, hata wale walioko kwenye matibabu Apollo India watahesabiwa, na yeyote yule mwenye familia ambaye ameaacha binadamu ndani ya makazi yake Tanzania atahesabiwa.

Tunahitaji takwimu za watu na makazi, kumbuka sensa inakwenda nyumba kwa nyumba sio mtu kwa mtu. Hakuna sensa duniani inayohesabu watu barabarani.

Kama una swali lingine au kuna ambacho hujakielewa usisite kuuliza tena Kamanda.

NYUMBA KWA NYUMBA nimeipenda sana hii mkuu.

Mwenye uwezo wa kufikili hawezi endeleza ubishi.

Mbowe na J Mbilinyi watahesabiwa wananyumba na familia zitajibu hayo maswali kwa ufasaha mtoa maada yampasa kutambua hivyo.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Joseph Mbilinyi mbunge wa Chadema kuweni na uzalendo mnaondoka Tanzania mnaacha zoezi la sensa mnakwenda kufungua tawi Marekani.

Wat is sensa.
aha! silazima kuwepo wote nyumbani kuna msemaji wa kaya/familia mke wake atatoa taarifa, kingine billion 140 zote kwa sensa jamani ni nyingi kweli... wakati operation line wakula vijipesa tu.
 
Ngug RITZ naomba nikujibu suala lako kuhusu sensa, zoezi la sensa halimzuii mtu kufanya shughauli zake za kila siku mahali popote anapotaka na isitoshe cha muhimu ni kwamba taarifa sahihi ndo kitu cha muhim kuachwa nyumbani sio lazima mkuu wa kaya awepo PHISICALLY.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Joseph Mbilinyi mbunge wa Chadema kuweni na uzalendo mnaondoka Tanzania mnaacha zoezi la sensa mnakwenda kufungua tawi Marekani.

we uko timamu sensa inakusaidia nini ,unatibiwa mwananyala kwa asprin miaka yote ya sensa ,je baada ya kuhesabiwa sensa mwaka huu utatibiwa ulaya ama utapata faida gani kutokana na sensa funguka kichwa
 
Huyu ritz sio wa kubishana naye .akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa.wadau mnatakiwa kumjua huyu ritz ni nani ,upeo wake.inawezekana hapa mnampa darasa kumbe alikwenda shule hakueleika au ndio hakuna kitu kichwani.sasa tahadhari husipoteze muda ukiona post yake wewe cheka au andika nenda shule ukaelimike
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Joseph Mbilinyi mbunge wa Chadema kuweni na uzalendo mnaondoka Tanzania mnaacha zoezi la sensa mnakwenda kufungua tawi Marekani.

Mkuu, umeongea kama mtu ambaye hujui sensa ni kitu gani? Sensa siyo uchaguzi ambao kila mtu anatakiwa kuwepo kituoni physically.
Hivi unadhani katika madodoso ya sensa kila mtu katika familia yako atahojiwa? Mtu mmoja anatosha kutoa taarifa ya familia nzima kama anazijua vyema.

Tafadhali usijiabishe kwa upofu wa mapenzi kwa chama chako na kutaka kuleta lawama zisizo msingi kwa hawa waheshimiwa wawili na wengine wote ambao siku ya sensa watakuwa safarini ndani na nje ya TZ.
 
Pro-Chadema wana mambo ya kizamani sana sasa kuweka picha ya Mbowe na maghorofa ya Marekani ndio nini utadhani msanii wa bongo movie.

Ritz,POLE KUBWA!Unawatetea wananafasi yakujitete ila wameamua kujitoa akili!Chunguza vizuri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom