" Mwenyekiti, Nifikishie Maswali Yangu Haya Kwa Dr Slaa" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

" Mwenyekiti, Nifikishie Maswali Yangu Haya Kwa Dr Slaa"

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kishongo, Oct 24, 2010.

 1. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi nina maswali yafuatayo ambayo ningependa nimuulize

  1. Ningependa kujua kuhusu hao vijana wake wa kazi mashushushu wanaompa taarifa mbali mbali anazokuwa anadai ni mabomu analipuwa, kwa taarifa za hivi karibuni kama ile aliyotutangazia kwenye mkutano wa hadhara kuwa Mstaafu wa EAC ameuawa na polisi na maiti yake iko Muhimbili na ikaja kugundulika kuwa ni taarifa ya uwongo, je anatuhakikishia vipi kuwa yale mabomu yake ya nyuma yalikuwa ni ukweli?

  Pili vijana wake walioko TRA hivi karibuni walimpa tena taarifa za uwongo kuhusu gari iliyokuwa huko Tunduma, je ina maana yeye kila anachoambiwa anakichukulia kuwa ni kweli kabla ya kikifanyia kazi? Na kama kweli ana vijana mashushushu walio mahiri kwanini anatuletea mambo ya uzushi?

  3. Ikiwa yeye kama kiongozi anaamini kila uzushi anaousikia mjini, je anatuhakikishiaje kuwa atakapokuwa kiongozi hatavictimize watu kutokana na taarifa za redio mbao na uzushi?

  4. Kwanini hakemei wafuasi na wanachama wake wanaotumia matusi kumfanyia kampeni? Ina maana ameridhishwa au yeye ameidhinisha utovu wa nidhamu kwa wanachama wake?

  5. Hili ni swali langu la mwisho, kwa kuwa Chadema imetumia resource nyingi kufanya kampeni za urais na kutelekeza kampeni za ubunge, je akishinda ataundaje serikali bila kuwa na wabunge wa kutosha kutoka kwenye chama chake? Na kwa kuwa chama chake kitakuwa na wabunge wachache sana ambao hawataweza kupitisha miswada yoyote bungeni, je hizo ahadi zake za kutekeleza mambo ndani ya siku 100 atazitekelezaje?


  Hayo ni maswali yangu machache tu mwenyekiti naomba unifikishie maana mimi sitakuwepo kwa kuwa bado niko njiani!

  Msafiri.

  Source: MJENGWA BLOG
   
 2. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mwenzio kaacha kuleta huku sababu anajua haya maswali ni murua kwa washona viatu pale jamhuri! Au mazungumzo yaliyo busara wakiwa na michuzi wala chai kwa chapati! Au ndio wewe mwenyewe waja kwa jina jipya mbona kama sijakuona humu kabla!
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 4,021
  Trophy Points: 280
  swala la kura feki amelirudia tena Mövenpick jana kwa hiyo madai yake anayasimamia hapo swala ni IGP na Kirevu kupinga sasa sijui unataka aseme nini? kuhusu swala la mzee wa EAC, tuambie kwann Polisi walimficha kwa siku kadhaa kama si wanatumika pia?
   
 4. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Co kila anaye toa taarifa za uovu anatumiwa na dr slaa ilanihaki ya kila raia kikatiba kufichua uovu unaotokea. Kuhusu EPA Km isinge kuwa kwel wasingerudisha kiasi kidogo kwny zile fedha. Natumaini umeridhika.
   
 5. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Wewe umefufukia wapi leo

  hii ni moja ya maada mbaya sijawahi kuona.. Yaani ni mbaya sanaaaaaaa
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Hayo maswali peleka kwa Mahimbo
   
 7. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Co kila anaye toa taarifa za uovu anatumiwa na dr slaa ilanihaki ya kila raia kikatiba kufichua uovu unaotokea. Kuhusu EPA Km isinge kuwa kwel wasingerudisha kiasi kidogo kwny zile fedha. Natumaini umeridhika.
   
 8. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mwambie apeleke kwao Nyaregete,Rujewa MBARALI sio hapa... Kisha waambie wanakijiji wenzake kwanini mashamba ya Mbarali yaliuzwa kwa bei ya kutupa
   
 9. admissionletter

  admissionletter Senior Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe acha kuchambua mambo kwa lengo la kutengeneza viji - hoja ambavyo havina nguvu. Tumeshapata mtu mwenye mwelekeo mpya wa kubadili maisha yetu. Wewe ungeweza kufanya mambo aliyofanya bungeni wewe....? Hi taarifa kama hizi hizi ndio zilisaidia. Kuhusu wabunge, je CCM wakishinda lakini wakipata wabunge wachache we unaona itakuwaje?
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  hilo swali la mwisho hata binti yangu LEAH hawezi kuuliza? ni vyema tuwe tunawaza kabla ya kuandika
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  el cr**p
   
Loading...