Mwenyekiti NCCR Mbeya wamkataa Mbatia asema hana dhamira ya kweli kukiongoza chama hicho ili kiweze | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti NCCR Mbeya wamkataa Mbatia asema hana dhamira ya kweli kukiongoza chama hicho ili kiweze

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]30 NOVEMBER 2011[/h][h=3][/h]

  Na Esther Macha, Mbeya

  [​IMG]
  WENYEVITI wa NCCR-Mageuzi katika wilaya zote mkoani Mbeya, wamemtaka Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Bw. James Mbatia, kujiuzulu wadhifa wake kwa
  madai ya kusababisha chama hicho kikose maendeleo.

  Akizungumza na Majira kwa niaba ya wenyeviti hao, Mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa, Bw. Robnson Fongo, alisema uamuzi huo umefikiwa na viongozi hao baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa Bw. Mbatia kama kiongozi wa juu katika chama.

  Alisema Bw. Mbatia amekuwa akiamua mambo ya chama yeye binafsi badala ya kushirikisha viongozi wenzake ambao anapaswa kukaa nao ili kukijenga chama hicho.

  Aliongeza kuwa, kiongozi huyo pia ameshindwa kuwafanya viongozi waliochaguliwa katika vyombo vya maamuzi kupitia chama hicho kuwa na msimamo wa pamoja katika mambo yenye maslahi kwa chama hicho.

  Kwa upande wake, Katibu wa chama hicho Wilaya ya Chunya Bw. Nyawili Kalenda, alisema kauli zinazotolewa na kiongozi huyo mara kwa mara zinachangia kukibomoa chama hicho badala ya kukijenga.

  Katika mkutano huo, wenyeviti nane wa wilaya zote walishiriki kutoa maamuzi hayo na kudai kuwa, ruzuku ya chama hicho imekuwa ikiishia Makao Makuu bila kufika mikoani.

  Hivi karibuni, viongozi wa chama hicho mkoani Kigoma nao walitangaza kuunga mkono mkakati wa kumng'oa Bw. Mbatia madarakani.

  Azimio hilo limefikiwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho mkoani humo katika kikao chao kilichofanyika wilayani Kasulu na kuhusisha wenyeviti wa majimbo manne ya uchaguzi mkoani humo.

  Pamoja na mambo mengine, wajumbe hao walijadili kwa kina changamoto na mafanikio waliyopata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ndipo ikaibuka hoja ya kumkataa Bw. Mbatia kwa madai mwenyekiti huyo hana dhamira ya kweli kukiongoza chama hicho ili kiweze kushika dola.

  Walisema Bw. Mbatia amekuwa akitumia ruzuku ya chama kwa maslahi binafsi, kujenga makundi kwa viongozi na wanachama na kutoujali mkoa huo ambao ndiyo wenye wabunge wa chama hicho.

  Mjumbe kutoka Jimbo la Kigoma Mjini, Bw. Said Milindi, alisema umefika wakati wa kumshinikiza Bw. Mbatia kuachia madaraka aliyonayo ili kutoa nafasi kwa wanachama kuchagua kiongozi ambaye atakiwezesha chama hicho kupata mafanikio kama ilivyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Kwa upande wao, wajumbe kutoka Kigoma Kaskazini, Kusini, Muhambwe na Buyungu, walimtuhumu Bw. Mbatia kwa madai kuwa ni mpinzani wa vyama vya upinzani.

  “Kitendo hiki si kizuri hata kidogo, kinachangia kuvunja upinzani na kukipa nafasi chama tawala kiendelee kuongoza, umefika wakati wa kumshauri aondoke madarakani ili apishe wengine ambaye atatimiza malengo yetu kama chama cha upinzani,” alisema Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Kigoma Kusini, Bw. Venance Mwaka.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jimbo la Muhambwe, Bw. Alex Mpambayifyisi, aliunga mkono mkakati wa kumng’oa Bw. Mbatia akimtuhumu ameshindwa kutengeneza kadi za wanachama ili kuhamasisha wanachama wapya wajiunge na chama hicho.

  Jumla ya wajumbe 12 wakiongozwa na Mwenyekiti wa kikao hicho, Bw. Mahamudu Tungirayokama na waasisi wa chama hicho mkoani humo, walishiriki kikao hicho ambacho kiliazimia Bw. Mbatia aachie wadhifa alionao ili kukinusuru chama hicho.

  Majira lilipomtafuta Bw. Mbatia katika simu yake ya mkononi ili aweze kujibu tuhuma hizo, hakupatikana kwa kuwa ilikuwa imezimwa.   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Watu wanasema majibu ya dhambi ni hapa duniani, waliokuwa wanachama wa chadema waliohamia NCCR ,kupewa vyeo vikubwa na kugombea ubunge na kupita waliyasema maneno hayo ya mwandishi wa majira kwa viongozi wa chadema yeye alichekelea akawapokea kwa mbwebwe,sasa wakati wake umefika wakunq,olewa hana namna ni swala la muda tu banyamulenge wa kisiasa ndani ya NCCR wamempania jambo zuri ni kuondoka salama badala ya kuja kuondolewa kwa kashifa duuh dunia kweli ni tambala bovu
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mbatia for nccr throughout the life
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  na afute kesi aliyomfungulia mdee sababu hata uchaguzi ukirudiwa hawezi kumshinda mdee
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  aendeleze uboflo mana uenyekiti kweli umemshinda
   
 6. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Kumbe wale waliokimbilia NCCR kutoka Chadema wapo kwa ajili ya Maslai yao? wameshindwa Chadema sasa wanataka kumn'goa aliyewakaribisha huku NCCR
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hili nalo litakuwa janga kwa hiki chama
   
 8. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  msitetee Mbatia ni kweli hana hadhi ya kipinzani kwani huwa hana ushauri mzuri, kuna kipindi aliambiwa kuwa ni CCM B hakupinga. Anatumika sana kudhoofisha upinzani
   
 9. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ahoo! balatanguyee!
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hao wameshafika nakuambia mkakati wao ni kushika nafasi za juu kabisa za NCCR -Mageuzi na baadaye wawakaribishe wapendwa wao toka vyama vingine ,mmoja atakuwa mwenyekiti,mwingine katibu mkuu,mwingine katibu mwenezi na mwingie atakuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake NCCR,mbatia kama hakulijua hilo ajiandae tuu,kwa jinsi mchoro ulivyochorwa kwa usatdi hana siku nyingi atanq'oka tuu
   
Loading...