Mwenyekiti mstaafu UVCCM Wilaya ya Rombo atoa onyo kwa wanasiasa wana hatarisha amani ya nchi

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
%25255BUNSET%25255D.jpg

Alianza kwa kusema Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi rombo unaunga mkono kauli ya Raisi JOHN POMBE MAGUFULI ya kupiga marufuku mikutano ya siasa,maandamano na oparesheni zote zenye kila dalili za uvunjifu wa Amani na kutoa onyo kwa vyama vitakavyo jihusisha na uvunjifu wa amani.

Akizungumza kutoka moshi mjini mwenyekiti huyo mstaafu UVCCM WILAYA YA ROMBO alisema umoja huo unajukumu la kujadili mambo kadha wa kadha yanayo ligusa Taifa na pasipo shaka kuunga mkono kauli ya mh Raisi ya kupiga marufuku mikutano ya siasa ,maandamano na shughuli zozote zenye harufu ya uvunjifu wa amani,pia alienda mbali zaidi kwa kuwa kumbusha wananchi kuwa dunia ya sasa si dunia ya kupigana na serikali bali ni dunia ya kupambana na ukata na kujiongezea kipato,ni dunia ya kupinga kukandamizwa kwa haki za watoto na wanawake ni dunia ,ni muda wa kupambana na mataifa yenye dhamira ya kutunyonya.

Pia nawakumbusha viongozi wa ukawa wote kuwa wanamajukumu ya kuwafanyia wananchi na kuacha bla bla za kwenye majukwa,kwani wananchi wanahitaji kula,kuvaa,kulala,kufurahi na kujiendeleza na si ukuta ambao hautawasaidia kuwalipia ada watoto wao wala kulipia gharama za vitu katika maisha yao,pia nawaasa vijana wa bavicha kuwa wajitambue watambue mahitaji ya jamii na kutumia nguvu walizo nazo katika kutatua matatizo ya wananchi.Na si kuzidisha matatizo katika jamii.

Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa lolote duniani ,pale vijana wanapofanya vizuri Taifa husonga mbele,ila kama vijana watatumika kwa uharibifu husababisha machafuko sasa sisi wapenda amani hatutaacha yakatokea hayo.

Pia alitoa onyo kwa makundi mengine na vyama vya siasa vyenye mipango hiyo kuacha mala moja kwani kauli ya Raisi ndiyo ya mwisho.PIa wao kama vijana wa ccm kinacho unda serikali ni jukumu lao kuhakikisha viongozi wao wanakua salama katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi na kupinga hujuma zote zinazopangwa katika kuharibu matarajio ya wengi kutoka chama TAwala.

Chama cha Mapinduzi,serikali na vyombo vyake vya ulinzi havita ruhusu machafuko yatakayoletwa na kikundi cha watu wachache wenye kuamini mawazo yao zaidi ya wengine kamwe haita nyamaza.

Pia aliwaomba jeshi la Polisi na vyomba vingine vya usalama kufanya kazi kwa weledi na kuweka maslahi ya umma mbele.Na yoyote anaekaidi maagizo ya serikali na Raisi basi sheria zifate mkondo wake

Pia kiongozi huyo mstaafu Alitoa ONYO KALI KWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO PAMOJA NA MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA TUNDU LISSU NA BAVICHA,kuwa wasicheze na serikali.

Wasicheze na maisha ya watanzania wasio na mbele wala nyuma,wasicheze na watoto wanaohitaji kusoma na kukua katika maadili,pia wasicheze na akili za watanzania za kuwadanganya kama hawajielewi,kuwa serikali ipo makini na hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuvuliwa Nyazifa Zao ndani ya bunge,kuvunja kanuni za maadili za mtumishi wa Umma ni kosa la kumuondolea mtu sifa ya kuwa mbunge..

Kidumu chama cha mapinduzi,kidumu chama Tawala.

Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Africa.

Imetolewa na Mwenyekiti mstaafu Uvccm Wilaya ya Rombo.
 
Akija kujitambua itakuwa too late, ila sababu ndio kastaafu, masikini, anaweza asijitambue tena
 
Cha kusikitisha hii kauli yake eti wasicheze na wananchi wasio na mble wala nyuma yaani ni wazi amewadharau na kuwatukana waTanzania yaani hatuna mbele wala nyuma isipokuwa wao ndio wana mbele na nyuma.
 
Eti kiongozi wa uvccm anaonya wanasiasa wavunja amani,yaani ccm wanajihisi ni Miungu watu,wanaonya kama nani
 
Back
Top Bottom