Mwenyekiti mstaafu UVCCM atuhumiwa kuua Mwanafunzi

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
38,221
66,919
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Manyoni na Mkimbiza mwenge kitaifa siku za nyuma Jamal Kuwingwa na wenzake wawili wanatuhumiwa kumteka nyara na kumtesa hadi kufa kijana Boniface Kawonga aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Mwanzi mjini Manyoni kwa kumtuhumu kuwa kaiba simu ya mkononi yenye thamani ya shs 70,000/=.
Leo yalifanyika mazishi ya kijana huyo na mji wa Manyoni ulirindima kwa maandamano makubwa yakiwa na mabango kumtuhumu Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Chilolo kuwa anafanya njama za kuwatoa Mahabusu watuhumiwa kwa vile anauhusiano wa karibu na mshtakiwa wa kwanza (uhusiano ule wa kipekee).
Swali, mbona sasa hivi tuhuma za mauaji kwa viongozi wa sasa na zamani wa CCM zimekuwa nyingi?

source; Wananchi wa Manyoni mjini.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom