*KWA UFUPI YALIYOJIRI MAPOKEZI YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA MKOA WA DODOMA JUMATANO 13 /12/2017 VIWANJA VYA CCM MAKAO MAKUU*
Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Dodoma leo tarehe 13/12/2017 wamempokea Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri Denice James na Makamu Mwenyekiti Ndugu Tabia Maulid katika Ofisi kuu za CCM Dodoma.
Katika mapokezi hayo Mwenyekiti mpya wa UVCCM alipata kuwashukuru Vijana wa UVCCM Mkoa wa Dodoma kwa kumchagua na kuwataka Vijana wote wa UVCCM kurudisha heshima na hadhi ya Jumuiya ya Vijana wa CCM.
Pia Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri James amewataka Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na wilaya kuanza kufanya ukaguzi/uhakiki wa Rasilimali za Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) katika maeneo yako.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa amehimiza Umoja na mshikamano kwa Vijana wote wa UVCCM ili kuwafanyakazi kwa umoja na kutimiza malengo kwa wakati.Pia aliwataka Vijana wawe mstari wa mbele kupambana na Rushwa na sio kuwaachia Viongozi pekee.
Mwenyekiti kheir alifahamisha kuwa umoja wa vijana utafanya kila linalowezekana kulinda uhai na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi.
Aliwaonya waumini wa makundi uchochezi na kuwagawanya watu kuwa katika uongozi wake hatavumilia watachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni katiba na taratibu za jumuiya na chama.
Mapema akimkaribisha Mwenyekiti Kaimu katibu mkuu UVCCM alisema moto wa UVCCM umewashwa rasmi na hakuna wa kuuzima chini kiongozi mahiri Kheir Denis. Alifahamisha awamu ya kwanza ni kupokea wanachma na hatua inayofuata ni kukabidhiwa mpaka majengo yao kwa vile watakosa wafuasi wa kuyatumia.
Katika mapokezi ya Mwenyekiti na Makamu wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) walipokea wanachama wapya 200 kutoka vyama mbalimbali vya Siasa nchini.
Vijana Jeuri ya Chama
CCM Mpya, Tanzania Mpya.