Mwenyekiti mpya UVCCM Kheri James atema checheee

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
478
1,000
*KWA UFUPI YALIYOJIRI MAPOKEZI YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA MKOA WA DODOMA JUMATANO 13 /12/2017 VIWANJA VYA CCM MAKAO MAKUU*

Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Dodoma leo tarehe 13/12/2017 wamempokea Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri Denice James na Makamu Mwenyekiti Ndugu Tabia Maulid katika Ofisi kuu za CCM Dodoma.

Katika mapokezi hayo Mwenyekiti mpya wa UVCCM alipata kuwashukuru Vijana wa UVCCM Mkoa wa Dodoma kwa kumchagua na kuwataka Vijana wote wa UVCCM kurudisha heshima na hadhi ya Jumuiya ya Vijana wa CCM.

Pia Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri James amewataka Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na wilaya kuanza kufanya ukaguzi/uhakiki wa Rasilimali za Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) katika maeneo yako.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa amehimiza Umoja na mshikamano kwa Vijana wote wa UVCCM ili kuwafanyakazi kwa umoja na kutimiza malengo kwa wakati.Pia aliwataka Vijana wawe mstari wa mbele kupambana na Rushwa na sio kuwaachia Viongozi pekee.

Mwenyekiti kheir alifahamisha kuwa umoja wa vijana utafanya kila linalowezekana kulinda uhai na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi.

Aliwaonya waumini wa makundi uchochezi na kuwagawanya watu kuwa katika uongozi wake hatavumilia watachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni katiba na taratibu za jumuiya na chama.

Mapema akimkaribisha Mwenyekiti Kaimu katibu mkuu UVCCM alisema moto wa UVCCM umewashwa rasmi na hakuna wa kuuzima chini kiongozi mahiri Kheir Denis. Alifahamisha awamu ya kwanza ni kupokea wanachma na hatua inayofuata ni kukabidhiwa mpaka majengo yao kwa vile watakosa wafuasi wa kuyatumia.

Katika mapokezi ya Mwenyekiti na Makamu wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) walipokea wanachama wapya 200 kutoka vyama mbalimbali vya Siasa nchini.

Vijana Jeuri ya Chama
CCM Mpya, Tanzania Mpya.
IMG-20171213-WA0139.jpg
IMG-20171213-WA0727.jpg
IMG-20171213-WA0138.jpg
IMG-20171213-WA0725.jpg
 
Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
16,996
2,000
Siasa buana....we need concrete actions which shows he aims to put our development agenda forward
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,401
2,000
CCM imetufikisha hapa tulipo nchi imekuwa maskini sababu ya ufisadi wao alafu naona vijana kma hawa wanasupport ushenzi huo inanitia hasira sana ww heri james or whatever u call urself umesaliti mabadiliko wanaolilia vijana sababu CCM imeprove failure kwa miaka 50 how on earth unaanza kutuaminisha watanzania kuwa kupitia UVCCM yako wataona positivr changes za kimaendeleo..... Je kipi ambacho CCM wameshindwa miaka 50 ila wewe utaweza ndani ya miaka mitano!!

Old wine new bottle expect same B.S
 
e2n

JF-Expert Member
Dec 24, 2015
635

Wewe ukae kijiweni utegemee serikali ikutajirishe?
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
11,549
2,000
Kugawanya watu ndio itikadi yenu sasa sijui hapo anamwambia nani wakati ndani ya chama lao wameshagawanyana tyr
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
11,549
2,000
Wale vijana wa kiliberali taarifa kama hizi huwa hawapendi zi prevail humu. Hongera sana kiongozi wetu shupavu na mwenye kukijua chama cha mapinduzi na itikadi na sera zake vyema
Pole sana ndugu, pole na ccm yenu ya manunuzi na uhujumu!
 
Zee la kitaa

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
403
250
Nyie ndo ccm haswaaa wapi jamaa kaomba msaada wa kutajirishwa na serikali ili hali yy kakaa kijiweni? We kazi za serikali huzijui kwa wananchi wake?
The role of the governments are:-
1. Provide public goods to the country
2. Formulate and foster policy issues that facilitate national prosperity
3. Promote peace and security in a country.
4. And others you can add. Where the government failed.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,401
2,000
Wewe ukae kijiweni utegemee serikali ikutajirishe?
Sio initajirishe ila sera mbovu za CCM zimetufikisha hapa tulipo.... Sasa hta kma nina kipato jua vijijini hawana maji, hawana umeme hawana vituo vya afya na dawa za kutosha ukizingatia 70% wanategemea kilimo ambacho kwa sasa kipo ICU je hayo yanaweza kufanywa na mwananchi mwenyewe tena anayeishi chini ya dollar moja kwa cku!!!!

No wonder upo UVCCM
 
e2n

JF-Expert Member
Dec 24, 2015
635
1,000
Sio initajirishe ila sera mbovu za CCM zimetufikisha hapa tulipo.... Sasa hta kma nina kipato jua vijijini hawana maji, hawana umeme hawana vituo vya afya na dawa za kutosha ukizingatia 70% wanategemea kilimo ambacho kwa sasa kipo ICU je hayo yanaweza kufanywa na mwananchi mwenyewe tena anayeishi chini ya dollar moja kwa cku!!!!

No wonder upo UVCCM
Sasa huo umasikini unaoulalamikia umeletwa na Ccm unatoka wapi ? Mbona kwenye majimbo yenu hamfanyi hayo mnayoyaongea
 
e2n

JF-Expert Member
Dec 24, 2015
635
1,000
Nyie ndo ccm haswaaa wapi jamaa kaomba msaada wa kutajirishwa na serikali ili hali yy kakaa kijiweni? We kazi za serikali huzijui kwa wananchi wake?
Kwani kazi ipi ambazo haizifanyi. Ina maana hata wewe kwenye familia yako unatimiza kila kunachohitajika?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom