Mwenyekiti Mbowe, tazama vijana wa chama na upuuzi wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti Mbowe, tazama vijana wa chama na upuuzi wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, Sep 11, 2012.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Nasema upuuzi wa vijana wa ndani ya chama umekua kiasi kwamba hawajitambui tena, naona katika mitandao wanakesha wakiwaza uchaguzi tu, uchaguzi wa ubunge, udiwani, urais na ndani ya chama, ni sahihi kabisa kwa mwanachama kuwa na malengo ya kuwa kiongozi hata mimi lengo langu kubwa ni kuwa kiongozi wa kisiasa kama nilivyo huku katika idara yangu ya utumishi.

  Ila ukweli ni kwamba kwa sasa vijana wengi wa chama chetu kutwa kucha wanajadili nani awe mwenyekti wa chama na nani awe mgombea ubunge eneo fulani. Hali hii imewapelekea wawe watu wasio na upeo wa kutafakari mambo na kuchambua hoja, wamelegea na kuridhika na upepo wa kisiasa uliopo na kuiona ikulu au ukumbi wa bunge kabla ya uchaguzi miaka 3 mbele.

  Ni hatari sana hii, nawaona wengi mitaani na kwenye mitandao na wengine wakianza kutangaza nia hadharani, hali inayopelekea kuishiwa uwezo wao wa kufikiri na kuwa masanamu yanasubiri kulaani tu na kutoa matamko au vitisho kwa jeshi la polisi na kwa viongozi wa serikali...

  hata ndani ya mtando huu na mingine kuna hao masanamu wanadhani wao wanahaki zaidi ya wanachama wengine, wanataja majina ya wagombea urais na uwenyekti wa chama ni upumbavu mtupu na kuishiwa uwezo wa kufukiri, kuwataja watu kuwa watawania nafasi fulani ni kuhamisha nia ya pamoja ya kushughulika na chama kwanza kukiimarisha..wao wamekuwa majuha wa kuwaza mitafaruku t
  u.

  Watu wapuuzi huwaza upuuzi mara zote,wapuuzi hawa huwatafuta wapuuzi wenzao kwa gaharama yoyote ili wajadili upuuzi wao, usifungwe katika genge la kujadili upuuzi.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kama vijana watajikita katika kutaka uongozi basi ni hatari kinachotakiwa ni royalty kwa chama kujenga chama kama lipo basi mwenyekiti aliangalie vimfimevyo hali hiyo inaweza kuleta balaa huko mbele lakini Nyakarungu ana haira sana kwa nini unaita wenzio masanamu
   
 3. N

  Noboka JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,145
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Ni kweli lugha ya kuita wengine masamanu si njema ingawa mleta uzi ana hoja. Kiukweli vijana huko CDM wadhibitiwe siasa za vyuoni si sawa na za huku uraiani wanahitaji kupunguza mihemuko
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni Vijana... Umewaona wa CCM? Makundi na PRINCE Ndani... Wanavurugana hadi Ma-PISTOL?
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  Kwani lengo la chadema si kuiomdoa ccm?ama unataka wawe wanafikiria kuwaacha ccm madarakani?mkuu fikiri kabla ya kuanzisha thread na kupoteza muda wa watu just because kuna uhuru wa kubandika hata pumba.
   
 6. C

  CRITO Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimewahi kukutana na nyakarungu na kufanya naye maongezi ni smart.

  Lakini linapokuja swala la chama kwa maana ya CHADEMA, Nyakarungu hayuko smart. Bila kurejea kwenye makosa yake binafsi yanayofanana na hicho alichokiita upuuzi, post yake hii yenyewe haina maslahi kwa chama. Ukiitazama, inatoa lawama kwa baadhi ya viongozi wa BAVICHA.

  Nadhani inafahamika juu ya nani anatajwa kugombea urais na uenyekiti, nikiwa muwazi zaidi ni Zitto, sasa Nyakarungu hataki watu wamkemee Zitto juu ya sarakasi zake.

  Nakubaliana naye juu ya kasoro kubwa ya vijana wengi wa CHADEMA (yeye akiwemo), kufikiria kuwa vijana wanaweza na ndiyo kila kitu, huu ni upuuzi.

  Zaidi namwomba Nyakarungu a-purify mind yake dhidi ya viongozi wa chama chake, vinginevyo yeye atakuwa ni zaidi ya wapuuzi wa vijana anaowasema
   
 7. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna hadi wazee wapuuzi wengi tu wanafanya kila siku maandamano na kutoa matamko mengi ya kipuuzi
   
 8. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewe kweli ni GT, asante kwa kutuonya, hakika mungu awe nawe kwa busara hii, tumekosa hoja, tunajadili watu, matukio na sio tena idea, sasa nyakarungu tufanyeje ili hawa vijana wa chama chetu wawe na another perspective? pls tunatokaje hapa tena?
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuelekea uchaguzi mkuu tutasikia mengi.
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nyakarungu una hoja ya msingi pamoja na kwamba unatumia lugha isiyokuwa ya kistaarabu kwa wenzako.

  Lakini ningetaka kukuona wewe mwenyewe ukionyesha mfano kwa hao unaowasema kwakuwa ni mmoja kati ya vijana wanaokesha kwenye mitandao ukipiga porojo za uchaguzi ndani ya chama pamoja na uchaguzi mkuu ujao.

  Inawezekana umegundua ugumu wa wewe ama kundi lako kukosa nafasi ya kufikia malengo ya kujipatia nafasi za uongozi ambazo mmekuwa mkiziota na kuzipigania muda mrefu. Lakini pia inawezekana sasa umekuwa na busara unaamua kutoa ushauri kwa vijana wenzako wanaoonekana kupoteza mwelekeo.

  Natarajia sasa kukuona ukiongoza vijana wenzako kuwa na mtazamo mpya wa ujenzi wa chama na kuacha porojo na makundi ya maslahi binafsi mitandaoni.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Power mongering.
  Power lust.
  Kiarusha hawa tunaita wasoma ramani. Fikra zao zinawatuma kuwa with the coming elections and the fate of cdm, huenda wakapiga bao...upumbavu huu!
  Ukitazama so far wanakifanyia nini chama utakuta hawana lolote zaidi ya kuwa na kadi ya chama iliyotolewa kwa mtindo wa papo kwa papo!
  Hata cdm ikikamata dola kesho, watakaoiua na kuisababishia iondolewe ni hawahawa, maana hawana cha kudeliver.
  Wizi mtupu!!
   
 12. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Sina budi kuwashukuru wote mliosema kuwa nami nina tabia kama ninayoikosoa, sipendi nidhihirishe tabia hiyo kwa kuwajibu majibu kama ya baadhi walivyoniita kuwa nina hila, ni sawa acha niiache hila yangu na nikubali makosa haya, na wewe usemaye nina kundi pia nakubali kwa mujibu wako unalijua kundi hilo wewe nalo nakubali ila natoa wito kwa vijana kuachana na mitazamo hiyo ya kijinga na kujadili hoja na issues zipo nyingi sana, kuliko kujikita kwenye upuuzi wa kujadili watu na uongoziwa miaka 3 mbele, hii itatuondoa kwenye mada na wazee wataendelea kutudharau na kuthibitisha kuwa hatuwezi kuongoza na tunapojaa ushabiki sana uwezo wa kufiri hupungua, kuhusu usmart kwenye chama, mimi niko tofauti sana na unidhaniavyo ndgu yangu, mimi sina dalili ya ushabiki usio na mbele wala nyuma, nadhani unaesema kuwa siko smart kuhusu chama, ni pale ninapokutana na mtu anataka tuanze kuwajadili viongozi mwanzo mwisho, hilo kwangu si kitu kabisa ila kuwakosoa huwa nawakosoa kwa simu zao. kuanzia mwenyekti, katbu mkuu hadi kiongozi wa chini kabisa, kuwaita watu wapuuuzi ni sahihi kwani tabia ndio inathibitisha mhusika wa jina hilo, hata mimi naweza kuwa mpuuzi kwa matendo ya kipuuzi
   
 13. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  vijana wanatakiwa waonywe juu ya tabia hizi, kisha waundishwe namna ya kujadli ajenda na namna ya kuongea na kila rika la wananchi, waelezwe kuwa kila mwanachama ana wajibu wa kuwabadilisha wananchi kifra na kuwaelekeza penye ukweli na haki, vijana waambiwe dawa ya tusi sio tusi, bali hekima, dawa ya mwenye hila sio uzushi bali elimu na dawa ya ubovu sio upuuzi bali ni elimu akili, vijana tuanze kutoa njia mbadala za utatuzi wa matatizo yanayoikabilijamii, naona kila kijana anahutubia akitoa laana kwa viongozi tu bila wao kujua njia mbadala ya matatizo yanayosababishwa na viongozi hawa, nawaona vijana wengi wakitoa vitisho butu kwa serikalieti kuwa wataandamana na mwisho hakuna hitimisho la njia mbadala zaidi sana utasikia wakisema chedema ndo njia mbadala. sasa ukiwauliza (wengi wao sio wote) njia mbadala ya kukabiliana na hayo pindi tukishika madaraka, utashangaa hutapatajibu. tafadhari tujipime sana na kujifunza sana.....
   
 14. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280

  Natafuta unachotaka kusema sikioni!!! wewe kama kijana kwa umri wako huu na kwa uandishi wako huu tungekupa nchi kama alivyopewa Nyerere at that age sijui leo tungekuwa wapi!

  Wewe ni kibaraka na hutaki kubadilika,hapa viongozi hujadiliwa kutokana na matukio na huwezi kuzuia hilo kijana! toa mfano kwanza hapa kwa kuweka mada za kujenga Chama na nchi na si za kulipuka kama hizi sababu majuzi kuna mtu wako kaguswa humu!

  Kuna kijana wa makundi ya Urais CDM kuliko wewe Nyakarungu? Toka ushindwe Bavicha umebaki na roho kwatu,kwa kijana wa umri wako na visasi vya kipuuzi hutofanikiwa kabisa maana hata hujalitumikia Taifa kwa kiwango cha umma kukutambua tayari unaanza fitna zisizo na kichwa wala miguu!

  Badilika ndugu yangu tujenge nchi na si kujenga matamanio binafsi!!!
   
 15. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280

  Ningefurahi kama ungemwambia straight Zitto maneno haya kipindi analeta hoja za Urais lakini hukusema wala kuandika chochote zaidi ya kumtetea sana tu alafu leo unakuja eti kuwafunza vijana! alafu elimu yenyewe inatolewa na wewe!
   
 16. eddo

  eddo JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 16, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nachokiona,kweli viongozi wakuu wa cdm wawe makini sana na kundi hili kubwa la vijana ambao wanataka madaraka.cdm waanzishe strategy za kuwaandaa vijana ktk uongozi.busara kubwa sana itumike hapa
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Amewaita wapuuzi , hii sio lugha mbaya. Angewaita wapumbavu ingekuwa mbaya.
   
 18. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  lo! kazi ipo
   
 19. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nyakarungu una uharo tu umekubana na naona umeona JF ndo
  sehemu ya kuutolea.

  Kama umepigwa bao kaa kimya,huna lolote na hujawahi kuwa na lolote
  so far.

  Shut the F*** off
   
 20. C

  CRITO Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo Nyakarungu wewe ulitaka zitto aliposema atagombea urais publicly ulitaka aachwe tu aharibu chama atakavyo,au shibuda aendeleze upuuzi wake tuuuu,bali vijana wakae kimya eeeh?

  Sasa kuwa wazi kuwa unamsema mwenyekiti wa bavicha kwa kuwa ndiye alitoa tamko kukemea shibuda na kwa hiyo zitto by implication.

  Najua wapo nijana wengine kwenye kundi hilo,lakini mwenyekiti wao ndiyo anasimama kama symbol ya bavicha.sasa hoja yako huoni kuwa inaharibu chama na kesho utakuta magazeti ya uhuru yanaiweka mbele?.

  Na nyakarungu,unajua kuwa wewe umewahi kunukuliwa kuwa chadema siyo mali ya mbowe na slaa wakati ule ulipohisi kuwa kamati ya uchaguzi iliwaonea? mtazamo kama huo siyo kujadili viongozi au mimi ndo sielewi? Acha hizo. Maneno haya ya kujificha kwenye vioja eti vijana wanajadili tu watu,watu ni zitto pekee?

  Mimi nina tatizo na vijana kama nyinyi nyakarungu kwani hamko royal kwa chama na mnadanganyika na umaarufu ambao nao mmeupata kwa sababu chama kimewapa vinafasi muonekane, ndo hayo ya chagulani et al,kafulila,na wewe nadhani.sasa kama nia yako ni ulterior,tutakuona ukibadilika.lakini kama utabaki yule yule niwe nabii wa kwanza kutabiri anguko lako.wewe nyakarungu unadhani unaweza kugombea ubunge kupitia jimbo gani? Au huna ambition ya ubunge?

  Nyinyi kuona kuwa madaraka ya siasa yanawezekana hata kwa jokeli ndo upuuzi wenyewe. Na kwa hili wewe Nyakarungu uko daraja la kwanza
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...