Mwenyekiti, Katibu Mkuu CHADEMA kigugumizi cha nini sakata la Wabunge wa Viti Maalum?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,810
35,802
Mabibi na mabwana inafahamika kuwa safari kuelekea uhuru haijawahi kuwa rahisi.

Wala safari ya kuelekea huko haijawahi na wala haitakuja kupungukiwa wasaliti.

Kwamba pana mbunge bungeni anaendelea kujitanabaisha kuwa ni mbunge wa CHADEMA na mko kimya tu?

Kwamba kuna watu yasemekana wamekiuka utaratibu na kujiwasilisha wenyewe kwa Spika kuapishwa kama wabunge na bado hazijachukuliwa hatua kali kabisa dhidi yao?


Wakuu, kwa mwendo huu mbona mnatuchanganya?

Kama mtaendelea na Kigugumizi hiki tegemeeni kuzinduliwa kwa chama kingine kitakacho kuwa na dhamira ya dhati.

Mheshimiwa Lissu kwa misimamo yako thabiti tafadhali tambua kuwa hauko na hautakuwa peke yako.

Aluta continua!.
 
UNATAKA MBOWE NA MYIKA WAWE WANALOPOKA KAMA JIWE LA CHATO....

Kuweka misimamo wazi siyo kuropoka.

Kwamba kuna mbunge bungeni na haafikiani na msingi mkuu wa chama kuhusiana na haramu ya uchaguzi wa 2020, kumlea huyo ni kulea kansa.

"If you disobey you go."

Hiyo si kuropoka. Huo ni msimamo thabiti!
 
Wameenda bungeni kwa baraka za Mbowe 😂...
Ndio maana Mbowe ametulia kimya, haya nyie nyumbxxxxx endeleeni kuzungusha mikono kwa style nyingine saivi .

"Safari kuelekea haki haijawahi kuwa rahisi wala kukosa wasaliti."

Uliweza kuyaona hayo kwenye mada?

The bad news for you is, "Aluta continua!"
 
Chadema asili wamempindulia meza Lissu

EU iache kuingilia mambo ya Tanzania kwa kuwa ina namna yake ya kumaliza changamoto zake za ndani

Huko Znz naskia na Maalim Seif ameanza ku shave ndevu na kunyoa ma panki yale ya 2010-2015

Kidumu chama cha Mapinduzi
 
Lisu na zitto waanzishe chama tutawafuata. CDM naona wanafuata maslahi yao tu.

Sent using Jamii Forums mobile Hiki ndo ambacho nilikua nakiwaza, nadhani tumemfahamu Tundu Lissu kwa muda mrefu, ni wakati wa kuanzisha chama chake sasa, hakika watu wenye misimamo kama yake tupo na labda itakua ndio njia mpya kuelekea serikali mpya. Ila kwa Chadema i think tumeona sura harisi ya walio wengi kule katika uongozi, tamaa na kutokujiamini na kutochange mbinu vinawamaliza very slowly, God forbid !!!!
 
Hiki ndo ambacho nilikua nakiwaza, nadhani tumemfahamu Tundu Lissu kwa muda mrefu, ni wakati wa kuanzisha chama chake sasa, hakika watu wenye misimamo kama yake tupo na labda itakua ndio njia mpya kuelekea serikali mpya. Ila kwa Chadema i think tumeona sura harisi ya walio wengi kule katika uongozi, tamaa na kutokujiamini na kutochange mbinu vinawamaliza very slowly, God forbid !!!!
 
Chadema asili wamempindulia meza Lissu

EU iache kuingilia mambo ya Tanzania kwa kuwa ina namna yake ya kumaliza changamoto zake za ndani

Huko Znz naskia na Maalim Seif ameanza ku shave ndevu na kunyoa ma panki yale ya 2010-2015

Kidumu chama cha Mapinduzi

CHADEMA asili ni hao washirika wa mashinji waluojipeleka wao kwa supika na njaa zao?

Haiyumkiniki mnatamani ndoto zenu zingekuwa kweli.

Habari mbaya kwenu ni kuwa vita dhidi ya udhalimu ni mkakati ambao ni zaidi mno ya personalities.

Mtasubiri sana.
 
Nyumbu oyeeeeeeeeeee! Wenye saccos yao wamekubali matokeo wengine endeleeni na Hilo beberu lenu Amsterdam.

Mna kiu kubwa sana ya kuhalilisha haramu eeh?

Mtasubiri sana.

Waliondoka kina daktari wa mihogo, kina manywele na wengi wengine. Sembuse kina Iddah?

Hamkuwahi kusikia ya kuvuja kwa pakacha?
 
Joyce Mukya kapata Ubunge?
CHADEMA asili ni hao washirika wa mashinji waluojipeleka wao kwa supika na njaa zao?

Haiyumkiniki mnatamani ndoto zenu zingekuwa kweli.

Habari mbaya kwenu ni kuwa vita dhidi ya udhalimu ni mkakati ambao ni zaidi mno ya personalities.

Mtasubiri sana.
 
Lisu na zitto waanzishe chama tutawafuata. CDM naona wanafuata maslahi yao tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa inatia hasira yaani watu wanapelekwa jela, watu wanajichanga ili kuwatoa halafu wanatusaliti ili waende Kula Bata Dubai pambafu zao mahabithi wajaalana mimi binafsi siwezi kuacha kuifuatilia siasa Kwani Imani yangu inaniambia siasa ndio maisha ya watu. Kibiashara madawa hospitalini bei vyakula sukari cement na mishahara na mengineyo mengi lakini kwa viongozi hawa kidogo naanza kurudi nyuma.
 
Back
Top Bottom