Mwenyekiti Kamati ya Richmond akatiwa maji

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
630
- Mwenyekiti Kamati ya Richmond akatiwa maji (Gazeti la Majira)

Na Rehema Mwakasese

KAMPUNI ya Huduma ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) imemkatia maji aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza Mkataba wa Richmond na kusababisha Waziri Mkuu na mawaziri wengine kujiuzulu, Dkt.Harrison Mwakyembe, baada ya kubainika amejiunganishia maji isivyo halali.

Wengine waliokatiwa maji kwa kushindwa kulipia ankara zao ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Bw. Vicent Mrisho anayedaiwa kiasi cha sh. 600,000, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Bw. Emmanuel ole Naiko anayedaiwa sh. 791,379 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bw. Peniel Lyimo.

Vigogo hao walikatiwa huduma hiyo ya maji Dar es Salaam jana katika operesheni kata maji inayoendeshwa na mafundi wa DAWASCO katika maeneo mbalimbali jijini.

Wengine waliokatiwa maji katika operesheni hiyo mbali na vigogo hao ni Bw. Abubakari Somo, Bw. Stanford Masulube, Bw. Miradji Msuya, Bw. Dominick Palangyo, Bw. Roger Magwaza na Tanzania Christian Church.

Akizungumzia hatua ya Dkt. Mwakyembe ambaye ni mbunge wa Mbeya kukutwa amejiunganishia maji, Ofisa Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Badra Masoud, alisema wiki moja iliyopita mkewe alikwenda katika ofisi za kampuni hiyo kwa lengo la kujaza fomu ya kuomba huduma ya maji ndipo alipoelezwa kuwa wamejiunganishia maji isivyo halali.

Bila kumtaja jina lake, Bi. Masoud alisema walipomkatalia kumpa fomu hizo wakimtaka alipe faini kwanza alikataa.

"Kwa kuwa alikataa ndio maana leo hii (jana) tumekuja kumkatia," alisema Bi. Masoud. Alitaja faini aliyotakiwa kulipa kuwa ni sh. 600,000.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa wale wote ambao wameshindwa kulipia ankara za maji au kujiunganishia maji isivyo halali watafikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.

"Wale wote wasiotaka kulipa tutang'oa mabomba na hatuogopi vitisho vyao kwani watu wenye uwezo ndio wanaoongoza kwa kukwepa kulipia bili za maji," alisema Bi. Masoud.

Kwa upande wake Meneje wa Kituo cha Boko, Bw. Ramadhan Mtendasi, alisema walifika nyumbani kwa Bw. ole Naiko, mara nne kudai ankara za huduma ya maji aliyotumia lakini alishindwa kulipa hadi hatua ya kumkatia inafikiwa jana.

"Maji yakikatika wao ndio wanaokuwa wa kwanza kulalamika wanasahau kuwa bila kulipia ankara zao kampuni hii itakufa," alisisitiza Bi. Masoud. Hatua ya kampuni hiyo kuwakatia vigogo hao huduma ya maji ni mwendelezo wa operesheni yake ya kukata maji kwa wadaiwa sugu.

Wiki hii kampuni hiyo ilikata maji nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Matein Lumbanga, ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania Geniva Uswisi na nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Maokola Majogo.
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,521
It is interesting that we have a law that allows publication of the DAWASCO defaulters, but we have strict penalties on anyone who will make public of Mali za Wakubwa!
 

MwanaHabari

JF-Expert Member
Nov 9, 2006
444
13
It is interesting that we have a law that allows publication of the DAWASCO defaulters, but we have strict penalties on anyone who will make public of Mali za Wakubwa!

mimi nimepigasana principle ya kuanika hawa watu wa maji...kama hawajalipa, kateni maji..tatizo ni huduma ya maji, nini itakufanya ulipe?..the fact kama uko kwenye magazeti au the fact kama huna maji. Huduma ya maji ni mkataba kati ya wateja na Dawasa. sisi haituhusu...and i agree kama wana sheria ya kuanika wasiolipa maji basi waanike mafisadi.

Shame watu wana politicize bill za maji...naona ile report iliwagusa sana, sasa hata pumba wataandika tu ilimradi wale waliowaumbua waaibike...
 

mwanatanu

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
854
126
...... ...and i agree kama wana sheria ya kuanika wasiolipa maji basi waanike mafisadi.

Shame watu wana politicize bill za maji...naona ile report iliwagusa sana, sasa hata pumba wataandika tu ilimradi wale waliowaumbua waaibike...

aha hawa waanikwe mbona wale ambao ndio wahujumu mafisadi wakongwe waandikwe majina tunayo lakini tunahifadhi huoni kama ni double standard
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
tunapoanza na kusema wamekatiwa maji, kesho akikatiwa simu kwa kuwa hhajalipia, tumuanike pia, keshokutwa akienda supermarket akakarudisha vitu alivyotaka kununua kwa kuwa pesa yake haijatimia tumuanike pia!

nahisi sasa waandishi wa habari wapo katika wimbi la kuandika tu chochote kile alimuradi kitauza.

inaaibisha unless hii iwe imetoka kwenye gazeti la udaku
 

Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,228
1,516
tatizo la haka kamama ni kaandishi habari fulani.......sasa kamepata kazi DAWASCO...........kakikatia watu maji kanatuma habari magazetini......."kwa kutumwa"........wee kamama.........ugomvi wa kisiasa usiuingilie......kaa chonjo...........endelea kufanya kazi yako ya kukata maji kwa wale wasiolipa......Godd work though!!! keep it up!!
 

MwanaHabari

JF-Expert Member
Nov 9, 2006
444
13
aha hawa waanikwe mbona wale ambao ndio wahujumu mafisadi wakongwe waandikwe majina tunayo lakini tunahifadhi huoni kama ni double standard

ni double standard kubwa tu na hawa waandishi wetu wanatia aibu kwenye fani ya uandishi...ni waandishi njaa tu
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,010
Agenda 21 at work..... katika kutangaza siyo katika kukatiwa maji. Wao waandishi walijuaje fulani kakatiwa maji au atakatiwa maji bila kutonywa na mtu....?
 

Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,228
1,516
Mwanakijiji,

.......unajua mambo mengine haka kamama......ni bora kanyamaze tu na hiyo Agenda 21 yake.........na afanye kazi yake ili kuliletea shirika uhai (very good effort)..........anajua fika kuwa anatumiwa kisiasa.......na yeye anafikiri.......DAWASCO ni kivuli.........JF is watching you Badra!
 

Tom

JF-Expert Member
May 14, 2007
470
20
Heko kwa kukata maji na naweza sema hivyo kwa sababu tu ni shirika letu, lakini sifa za dhati mtazipata pale shirika litapopata nguvu kiuwezo kwa kutoa huduma bora, na kuwajibika kwa wateja.
Siamini kama siasa inaweza kujitenga na mashirika ya umma tofauti na baadhi ya wachangiaji wangine.
 

Ilongo

JF-Expert Member
Feb 25, 2007
292
8
Heko kwa kukata maji na naweza sema hivyo kwa sababu tu ni shirika letu, lakini sifa za dhati mtazipata pale shirika litapopata nguvu kiuwezo kwa kutoa huduma bora, na kuwajibika kwa wateja.
Siamini kama siasa inaweza kujitenga na mashirika ya umma tofauti na baadhi ya wachangiaji wangine.

Of course, kinachokera hapa siyo kukatiwa maji, ila ni nani kakatiwa maji. Sisi wengine hata hayo maji ya kukatiwa tunatamani tuwe nayo, lakini wapi.

Walipokatiwa mawaziri na viongozi wengine na wakaandikwa magazetini, sikuona aliyekasirika badala yake ilionekana sahihi. Hivi ndivyo tulivyo [Nyani Ngabu].
 

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
931
Good job kwa dawasso, kama tutaendelea kusuck haka kaorganization then tutakwisha wajameni.

Sidhani kama hii ni personal attack kwa Dr.
 

Fisadi Mtoto

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
639
79
Naona magazeti ya Rostam Azizi bado yanaendeleza ugomvi wao na Dr Mwakyembe

Mama nimekwambia muda mrefu sana uache kudandia mambo usioyajua please.RA hajawahi na hajapata kuwa mmiliki wa gazeti la majira...sasa gazeti lamajira kumtuhumu Mwekyembe kama lilivyo mnukuu Badra linamuhusu nini RA.Mwakyembe alijiunganishia maji kinyume cha utaratibu,huo ni wizi na ukosefu wa uadilifu,hakutumwa na RA kufanya hivyo,na siyo wakwanza kukamatwa anafanya hivyo na kutangazwa....msiwe double standard kama mtu amekosea na asemwe.
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
630
Msimamo wangu juu ya hili ni kwamba kosa ni kosa tu, ukifanya kosa hakuna haja ya kutafuta mchawi.

Tunapoongelea double standard ya waandishi wa habari inabidi pia tuongelee double standard ya sisi hapa JF. Mawaziri walipokatiwa maji na kuanikwa magazetini sikuona mtu aliyepinga hapa.

Kosa halina sura, ndivyo ninavyowaambia wanangu na ukikamatwa na kosa jaribu kujifunza na kwenda mbele badala ya kuhangaika kutafuta nani kafanya hilo kosa lijulikane.

Wale wote wanaoongoza mapambano na mafisadi lazima wafanye juhudi kubwa kuhakikisha na wao huko nje wanakuwa wasafi kadri iwezekanavyo kwa mazingira ya TZ. Ni sawa na sisi JF, tutakuwa credible kama yale tunayoyapinga, tutayapinga kwa kila mtu bila kujali chama na kuhaki,kisha sisi wenyewe sio vifisadi wadogo.
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,123
Hawa waandishi wa habari wanaizalilisha fani ukipewa wekundu tuu tayari unahaha mnakuwa kama wanaoandika udaku?
We have a long way to go na hawa waandishi wetu kwa kweli.
Basi wajaribu ata kutuletea majina ya watu ambao wanaendelea kurudisha fedha za EPA?
Tunaomba journalism kama profession ithaminiwe pls
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
hakuna aliyekasirika kwa mwakyembe kuanikwa kwenye magazeti kuwa kakatiwa maji. alifanya kosa na ALIPASWA kukatiwa maji, na asingekatiwa maji basi DAWASCO tungesema wanaupendeleo kwa watu mashuhuri.

watu wanachopigia kelele ni kuanika majina ya walokatiwa maji lakini majina ya mafisadi hawayaaniki.

hivi tutafika ?
 

IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
138
Kweli watanzania tunafanywa wajinga , Mwakiembe anadaiwa sh laki nane , hivi hawa dawasko mbona pale jeshini walikuwa wakidai zaidi ya milion miambili ila walikaa kimya, sasa kwa huyu shujaa wemeona waje hapa waseme, mbona hamjatuambia kule chooni na bafuni mwake katumia maji ujazo gani?
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
630
hakuna aliyekasirika kwa mwakyembe kuanikwa kwenye magazeti kuwa kakatiwa maji. alifanya kosa na ALIPASWA kukatiwa maji, na asingekatiwa maji basi DAWASCO tungesema wanaupendeleo kwa watu mashuhuri.

watu wanachopigia kelele ni kuanika majina ya walokatiwa maji lakini majina ya mafisadi hawayaaniki.

hivi tutafika ?

Inatakiwa tuyaunge mkono magazeti yanapoanika makosa bila ya kujali mkosaji ni nani.

Tofauti hapa ni kwamba hao DAWASCO wametoa hiyo taarifa kwahiyo hata magazeti yakiandika hayawezi kuburuzwa mahakamani.

Kwenye ufisadi mambo mengi bado ni hisia na waandishi waoga huwa wanaogopa
wasije wakaingia matatizoni.

Taarifa ya ufisadi inapotolewa na chombo kingine, wanakuwa mbele kuitangaza. Mfano ni suala la Chenge, walikuwa wanaogopa kumtaja. Lakini gazeti la guardian la UK lilipomtaja, magazeto yote ya TZ yakamtaja pia na kuongeza mbwembwe nyingi tu. Hata hao Gurdian walikuwa hawataji majina mpaka walipopata taarifa ya uhakika kuhusu Chenge.

Somo hapa ni kwetu wote, ukifanya kosa lolote, hakuna haja ya kutafuta mchawi. Timiza wajibu wako, hutaanikwa mahali popote.
 

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,353
1,920
Hata kama nia ya ku-report hii taarifa ni ingine, lakini ni aibu sana na ujinga wa hali ya juu kwa mtunga sheria kuvunja sheria. Ni wapi mwisho wa kuvunja sheria ile nchi. Halafu nashangaa watu mnashupalia mambo mengine wakati kuna clear and utter violation of the law hapa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom