Mwenyekiti James Mbatia msaidie Mwanachama wako mwenye kadi namba moja Mabere Marando arudi nyumbani huko ugenini anapata tabu

Hii mentality ya kuamini kwamba mtu akiwa na siasa za kistaarabu na zenye kutanguliza maslahi ya Taifa anasingiziwa kuwa ni CCM siyo sawa kabisa

Siasa za harakati na uchonganishi wa Taifa letu dhidi Mataifa makubwa hazitatusaidia

NCCR Mageuzi ikirejea kuwa kiongozi wa Mageuzi nchi yetu itafaidika zaidi kuliko ilivyo sasa
Du pole sana
 
Mabere Nyaucho Marando ndiye Mwanachama mwenye kadi namba moja ya NCCR Mageuzi,alizaliwa takribani miaka Sabini iliyopita huko Mkoani Mara

Nguli huyu wa sheria ni miongoni mwa waasisi wa siasa za mageuzi hapa nchini akiwa na wenzako akina Bagenda, Ole Sirikwa,Komu, n.k

Huyu Mbabe wa siasa za upinzani alihamia chadema akawa kiongozi kule baada ya kuvurugana kwenye NCCR Mageuzi,Mwanasiasa huyu hajaonekana hadharani kwa muda mrefu, yuko wapi ?

Mhe. Mbatia kuna dalili kuwa nyumbani kumenoga msaidie nguli huyu arejee apewe heshima yake kama akina Emmanuel Ole Sirikwa na wengine

NCCR Mageuzi kumenoga
Noted
 
Back
Top Bottom