Mwenyekiti halmashauri ya Geita ahamasisha wananchi kuvamia mgodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti halmashauri ya Geita ahamasisha wananchi kuvamia mgodi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Apr 19, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya mkoani Geita ambaye pia ni Diwani wa Nzera kwa tiketi ya CCM, Joseph Musukuma, anawahamasisha wananchi kufanya maandamano na kulala barabarani kuanzia tarehe 29 mwezi huu kupinga uwepo wa mgodi wa dhahabu Geita (GGM). Akihutubia mkutano wa hadhara amesema,

  “Ndugu zangu wana Geita baada ya tarehe 29 mwezi huu (Aprili) tutafanya maandamano kuupinga mgodi wa Geita, nataka niwahakikishie kwamba tukiandamana na kulala barabarani na kuzuia magari yao yanayobeba wafanyakazi wao, lazima watakuja kutusikiliza,” alisema Musukuma.

  Source: Habari leo

  Mbona kiongozi wa serikali anataka kuleta fujo na kufanya serikali isitawalike.
   
 2. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo raslimali zinazowazunguka wananchi haziwasaidii wananchi wa kawaida, bali wawekezaji ambao ni feki kwa kuwa wanatuibia.Hali hiyo inawafanya wananchi kuwachukia wawekezaji, unless waache wizi na wahakikishe wananchi wanaozunguka raslimali hizo wanafaidika nazo.
   
 3. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mshabiki wa maandamano nikiwa naimani ya kwamba anayeandamana anahaki kikatiba ya kufanya hivyo na si mbaya akitumia haki yake bila kuathiri haki ya wengine. Ila sasa hii ya kulala barabarani imevuka ile mipaka ya kutokuingilia haki ya wale wasiotaka kuandamana. Maana kuna watu wataendelea na shughuli zao sasa itakuwaje...? Itakuwa kama ile ya wazee wa Africa Mashariki walioadhibiwa na polisi kwa kigezo cha kuvunja sheria. Huyu Mkiti - CCM -Geita muongoza maandamano alitakiwa atumie busara.
   
 4. Rodcones

  Rodcones JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 16, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama ametumia busara na imeshindikana sasa wataka afanyeje?
   
 5. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo wakubwa zake kwenye chama cha magamba watamvumilia??
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Moja wao akikanyagwa na gari wataondoka barabarani.
   
 7. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Inapendeza kuona pale kiongozi mwenye dhamana anasikiliza na kuguswa na machungu wanayoyapata wapiga kura wake. "Meya" huyu anastahili pongezi kutokana na kauli yake hii na itapendeza kuona wana Geita wakiweza kuyafanya yale wanayokusudia. Matatizo haya ya rasilimali sio mageni duniani yapo sana hapa Tanzania, Congo, Mali, Nigeria, zamani kule nchini Chile, Brazil n.k . Uwekezaji wa mitaji katika uzalishaji wa rasilimali ni lazima uende bega kwa bega na uboreshwaji wa miundo mbinu na huduma zingine muhimu za jamii katika maeneno husika.
  Tatizo kubwa la migodi na visima vya mafuta ni kwamba, wawekezaji huishia kutengeneza nchi tofauti ndani ya nchi au mikoa, wilaya husika. Kule kwenye machimbo huwa kama ni pepo, mzunguko wa fedha huwa mkubwa, huduma muhimu hujitosheleza na kibaya ni kwamba unafuu huu wa maisha huwapitia pembeni wakazi asilia wa maeneo yenye rasilimali. Leo hii ni kitu cha kawaida kusikia makampuni ya migodi yakiagiza mpaka maji ya kunywa kutoka nje badala ya kuwekeza katika mpango madhubuti wa kusambaza maji kwa wote. Ila na pia kutokana na fedha kuwa nyingi katika migodi hii, wawekezaji na wafanyakazi wao (wengi wao kutoka nje ya maeneo husika) huishia kutumbua kwenye anasa zisizojenga jamii na kuchangia kuharibu mila, desturi na afya za jamii zinazozunguka rasilimali hizi.

  Mgawanyo huu onevu wa matunda ya rasimali ni chachu ya manung'uniko katika jamii za karibu na rasilimali hizo
   
 8. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Maandamano ni silaha ya watu wanaoonewa kudai haki zao. Arusha walipofanya maandamano Kikwete anahamishia mikutano DSM na kuwaathri waka za wa Jiji hili kwa foleni. Sasa sijui huko nako atawaadhibu kwa njia gani?
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  Kuandamana sawa ila hili la kuwahimiza walale barabarani lina mshkeli.
   
 10. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kutenda watende wao,tukitenda sisi lawama.Acha waandamane nchi si yao bwana,
   
 11. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Geita,maarufu kwa jina la MSUKUMA ameitisha maandamano kwa ajili ya kuvamia mgodi wa GGM kwa madai kwamba uwepo wake haujasaidia maendeleo katika wilaya hiyo.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Msukuma alisema kuwa mgodi unapaswa kuondoa kero za maji pamoja na kutatatua matatizo mbalimbali ya kijamii yanayoukabili mji huo kutokana na ukweli kwamba Mgodi upo katika mji huo.

  Mwenyekiti huyo kupitia CCM alidai kwamba siku ya jumatano wataandamana kuelekea mgodini na kisha watazuia magari yote ya mgodi yasitoke wala kuingia mgodini hadi watakapopata majibu ya maswali yao kwa ufasaha.Aliongeza kuwa iwapo madai yao hayatatimizwa watazuia Mabasi ya wafanyakazi kupita mitaani kwa ajili ya kupakia wafanyakazi na badala yake watayalazimisha kuingia katika kituo kikuu cha mabasi ili yalipiwe ushuru.

  MAONI YANGU:

  Huyu mwenyekiti kakosa mwelekeo kutokana na ukweli kwamba mgodi hutoa pesa kwa Halimashauri kila mwezi lakini hakuna kinachofanyika.Aliahidi kuwataja MAFISADI wa Halimashauri hadi leo hakuna jina hata moja alilotaja.Pia amesahau kuwa MIKATABA mibovu iliyosainiwa na viongozi wa CCM ndio inayosababisha migodi kutojali wananchi katika eneo husika.Alishindwa kujibu hoja za CHADEMA walipokuja hapa ambazo zilidai kuwa kila mara MGODI unapotaka kusambaza maji huwa wanakataa nakutaka wapewe pesa ili waifanye wenyewe hiyo kazi,wamekuwa kikwazo namba moja pale MGODI unapotaka kusambaza umeme kutoka kwenye kampuni yake ya GEITA POWER, inasemekana kuna reserve ya umeme kubwa sana pale,vilevile wamesababisha kudorora kwa mradi wa barabara unaodhaminiwa na MGODI kwa madai kuwa waanataka wasimamie wao wenyewe.
   
 12. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Wadau mlio mbali na Geita sikilizeni kwa makini.

  Huyu MUSUKUMA kwanza atueleze zile pesa zinazotolewa na GGM Mil 300 wanapeleka wapi kila mwaka?

  Musukuma nataka atueleze ule uzio wa Halmashauri kwa nini umegharimu zaidi ya Mil 700.

  Musukuma tueleze kwa nini viwanja vya Mwatulole vimeuzwa kwa madili, mahali ambapo Makao Makuu ya mkoa mpya yatawekwa, hadi Miliono Tisa watu wametoa. Lisiti lakini inaandikwa laki nane!!!!

  Musukuma hana LOLOTE kituo kipya cha Mabasi (Stendi Mpya) kilichofunguliwa kwa mbwembwe wakati wa Kampeni mbona sasaivi mashimo matupu?

  Musukuma Ameuza viwanja sehemu ambayo ilitakiwa kuwekwa majukwaa ktk uwanja wa GGM, kwa nini wamegawa pale. Huyu ni FISADI na mabasi yake mabovu

  Ninazo data za kutosha sana tu kuhusu Geita,

  Mara ngapi Mgodi umetaka kuleta maji hawa hawa wa Halmashauri wanataka wapewe CASH, Nani awape wezi?

  Hana Lolote,

  Tayari kuna makubaliano na mkandarasi ameshasaini kujenga kwa Lami kipande cha barabari toka round about hadi Geti kuu la Mgodi wa GGM.

  Asiwachanganye!

  Geita ni CDM tupu,

  Tambueni vizuri, Musukuma ni darasa la SITA hata la Saba hakumaliza, upeo ndio unafika hapo.

  Ile X-ray iliyopelekwa na Mgodi pale Hospitali ya wilaya imeibiwa yeye alikuwa wapi?

  Wandugu, hiyo siku akilala chini Lambeni bakora huyo ni mwizi.

  Uliza alifika pale Makamu wa Mkwerrrr ilibidi akusanye wanafunci wa shule ya Msingi na wafanyakazi wa halmashauri

  Kanda ya ziwa iko FULLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLL!
   
 13. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  NIJUAVYO MIMI.

  Bwana Msukuma anapenda cheap popularity, hana dhati yoyote,wakati anataka kupambana na wale aliowaita MAFISADI WA HALMASHAURI YA GEITA aliitwa na madiwani wenziwe na viongozi wa ccm akaonywa na akanywea.
  Walimu wa shule za msingi wapatao 580 walipofanya maandamano kudai fedha zao za kujikimu walizokuwa wakidai kwa takribani miezi mitano,mbele ya Naibu Katibu mkuu TAMISEMI,Bwamna Msukuma alisema walimu hao hawana adabu na kwamba Halmashauri yake itawakataa na kwarudisha aliyewapangia kwenda Geita.

  Leo nashangaa huyu bwana kuwataka wanageita waandamane mbona haelezi kwanini aliamua kuwa kimya wakati wale aliowaita mafisadi wakiwepo Geita kwa raha zao?
   
 14. mwanamapinduko

  mwanamapinduko Senior Member

  #14
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 174
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Resource iliyopo Geita na maendeleo ya mji wenyewe havifanani
  -Hakuna maji ya bomba ya uhakika kwenye mgodi yapo na yanapita geita mjini kuelekea kwenye mgodi.
  -Geita hawapati mgao ila wanapata GAWIO la umeme maana inaweza pita masaa 48 hakuna umeme- mgodi unazalisha umeme mpaka na ziada ambayo hawaitumii
  - Barabara za ndani ya mji hakuna hata yenye ka-lami hata mita moja. Wananchi wanaiona kwenye barabara kuu inayoingia geita ktk mwanza na kupita kuelekea bk na hii imejengwa kwa kodi zetu.
  -Angalia hiyo hospitali ya wilaya ni kama kituo cha afya wananchi hukimbilia sengerema ambako kuna hospitali teule inayomilikiwa na misheni

  Hizi ni sababu tosha za wananchi kujiuliza. Je baraka mungu aliyowajaalia kwenye ardhi yao na jinsi wanavyoishi kuna uwiano? Je nani anapora hiyo neema waliojaaliwa. Jibu ni wazi ni wawekezaji na ndugu zetu wabinafsi wachache walioko huko wanakoita kwamba ndio Tanzania.
  Njia sahihi iliyopo ni kwa wananchi wenyewe wa geita ambao ndio waathirika kujikwamua. Hakuna njia mbadala
   
 15. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hilo nalo neno.
   
 16. 2

  250689 Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli wabongo wanataka chao...watu wameshachoka na usanii wa viongozi wa nchi wanao ifanya nchi kama mtaji wa matumbo yao,la kushangaza hata hawashtuki....
   
 17. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti, kabla ya mkutano wa hadhara je Baraza la Madiwani limeazimia nini? Kwa nini suala nyeti kama hili unalizungumzia kwenye mkutano wa hadhara badala ya Baraza na kuweka maamuzi?

  Huu ni usanii na sifa nyepesi. Litumie Baraza lako kufanya maamuzi ambayo yana tija kwa wananchi na pia kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
   
Loading...