nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 810
- 2,851
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime Vijijini, Simon K pamoja na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya mauaji namba PI RM (MURDER) CASE NO. 4/2021 wameachiwa kwa dhamana hapo jana mjini Musoma. Jambo ambalo limewashangaza watu wengi kwani inajulikana wazi kuwa kesi hiyo haina dhamana.
Hata hivyo mke wa Mwenyekiti huyo alikuwa anajisifia kuwa wametumia milioni zaidi ya 400 hivyo lazima mumewe atoke.
Taarifa zilizopatikana ni kuwa Mwenyekiti huyo amebadilishiwa mashitaka kutoka kesi ya kuua kwa kukusudia hadi kuua bila kukusudia na ndio mwanya waliotumia kumpa dhamana.
Jambo hili ni baya mbele za umma kwani ushahidi wa huyu Mwenyekiti kuua uko wazi. Ni murder case na hakuna kesi ya kuua bila kukusudia.
Kwa kuwa huyo Mwenyekiti ni mfanyabiashara na ana pesa basi sasa watu wanaamini uongozi wa sasa unakumbatia watu wenye pesa na kuwa wenye pesa wako juu ya sheria.
Wanaweza kuua na kuhonga na kuepuka mkono wa sheria.
Hii ni ishara mbaya katika uongozi wa awamu ya sita. Na itabaki hivyo kuwa kama unataka haki basi tafuta pesa za kuhonga.