Mwenyekiti Halmashauri ahamasisha maandamano kupinga mgodi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mwenyekiti Halmashauri ahamasisha maandamano

Imeandikwa na David Azaria, Geita; Tarehe: 18th April 2011 @ 23:40 Imesomwa na watu: 88; Jumla ya maoni: 0








MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya, Joseph Musukuma, amewashawishi wananchi kufanya maandamano ya amani kwa alichokisema ni kupinga uwepo wa mgodi wa dhahabu Geita (GGM) unaokandamiza haki zao.

Musukuma ambaye ni Diwani wa Nzera kwa tiketi ya CCM amesema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa wilaya hiyo, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa.


Alisema umefika wakati wananchi wadai haki yao kwa njia ya maandamano ya pamoja, kwa kuwa kwa muda mrefu, viongozi na watendaji wa Serikali, wakiwamo wa kitaifa wamekuwa wakizungumza na uongozi wa mgodi huo juu ya maendeleo ya wilaya hiyo bila mafanikio.


“Ndugu zangu wana Geita umefika wakati sasa sisi kuandamana au kulala barabarani kudai haki zetu zinazoonekana kuminywa na mgodi wa Geita, nataka niwahakikishie kwamba tukiandamana na kulala barabarani na kuzuia magari yao hayo yanayobeba wafanyakazi wao, lazima watakuja kutusikiliza,” alisema Musukuma.


Aliendelea kusema “baada ya tarehe 29 mwezi huu (Aprili) tunatarajia kufanya maandamano makubwa sana kuupinga mgodi wa Geita, hata sisi tuna haki ya kupata misaada kutoka GGM kama wananchi wenzetu wa maeneo mengine yenye migodi wanavyofanyiwa na migodi

mingine, kwani ina maana GGM wao wana tofauti gani na migodi mingine kama ile ya Nyamongo?’’

Aliwaambia wananchi kwamba hata wananchi wa Nyamongo hawakupata haki yao kirahisi kutoka mgodi wa Nyamongo.


“Yalifanyika mazungumzo ya amani kama ambayo yamekwishafanyika kwa mgodi wa Geita bila mafanikio, baada ya hapo wananchi wa kule waliamua kuingia barabarani kufanya maandamano ya kuutaka ama mgodi ufungwe waendelee kuchimba wao wenyewe au watekeleze matakwa yao”.


Aliendelea na ushawishi kwa kusema maandamano dhidi ya mgodi wa Nyamongo yalizaa mafanikio.


“Kwa hiyo na sisi wananchi wa Geita muda sasa umefika wa kufanya hivyo, ili tupate mema ya nchi, vinginevyo tutaendelea kulia tu huku wageni wakija na kuvuna na kisha kuondoka na kutuacha tukiendelea kutaabika na umasikini,” aliendelea na ushawishi.


Alitolea mfano wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na wa North Mara uliopo Nyamongo inayosimamiwa na kampuni ya African Barrick Gold, kwamba imewajengea wananchi hospitali za kisasa na kuweka vifaa vya matibabu.


Alisema pia migodi hiyo imewajengea wananchi vituo ya Polisi vya kisasa na kutoa usafiri wa uhakika kwa watendaji wa Polisi na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.


“Jamani kwa taarifa tulizonazo tena za uhakika, GGM ndiyo wa kwanza kwa uzalishaji wa dhahabu nyingi katika ukanda wa Afrika


Mashariki, lakini cha ajabu wameshindwa hata kutujengea kituo cha afya, wameshindwa kutujengea hata shule moja ya msingi tofauti na zile walizojenga kwa kuhamisha wananchi, wameshindwa hata kutuvutia maji wakati wana maji ya kutosha, umefika wakati tuseme

hapana, na sasa tuingie barabarani tudai haki zetu,” alisema Musukuma huku akishangiliwa na umati wa watu.

Alisema katika mgodi wa GGM, upo meme wa ziada unaotosheleza wananchi wa mji wa Geita lakini kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa halmashauri, uongozi wa mgodi unasema hauwezi kutoa umeme wa kuchezea.


“Yaani maana yake ni kwamba sisi hatuna thamani, wakati wanachimba dhahabu kwenye ardhi yetu, wanapitisha magari makubwa kwenye barabara zetu ambazo tunatumia pesa zetu kuzitengeneza na kutuharibia wakati wao hawajahi hata kututengenezea kilometa moja ya

barabara,” aliendeleza ushawishi.

Aidha, Mwenyekiti huyo aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ambayo maandamano hayo yataitishwa, ili kushinikiza kupatikana kwa madai yao na kama itashindikana ni bora mgodi huo ufungwe, ili wazawa wachimbe wenyewe kwa kuwa tangu kuanzishwa, miaka 10 iliyopita, hawaoni faida yake.


Alisema kwamba yuko tayari kuonekana mbaya kwa wawekezaji kuliko kuonekana mbaya kwa wananchi na nchi yake.


 
PHP:
Musukuma ambaye ni Diwani wa Nzera kwa tiketi ya CCM  amesema hayo  wakati akihutubia mamia ya wananchi wa wilaya hiyo, kwenye  mkutano wa  hadhara uliofanyika mjini hapa.   
 
Alisema umefika wakati wananchi wadai haki yao kwa njia ya  maandamano  ya pamoja, kwa kuwa kwa muda mrefu, viongozi na watendaji wa  Serikali,  wakiwamo wa kitaifa wamekuwa wakizungumza na uongozi wa mgodi  huo juu  ya maendeleo ya wilaya hiyo bila mafanikio.

CCM in crossfire...................................
 
Back
Top Bottom