Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Bwana JOSEPH NDALAMA, amepongeza hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuahidi kuyalipa madeni ya walimu wanayodai, ambayo yamefikia zaidi ya shilingi milioni 800.
Hata hivyo ameitaka serikali itekeleze ahadi hiyo mapema iwezekanavyo, ili kuinua ari ya walimu katika kutekeleza majukumu yao ya ufundishaji, kwani wanaishi katika mazingira magumu.
Kwa upande wake Katibu wa chama hicho Bwana PETER SIMWANZA, amewaonya walimu hao wasichanganye utetezi wa walimu na mambo ya kisiasa, hali ambayo amesema inaleta mihemko inayochangia uvunjifu wa amani.
Chanzo: ITV