Mwenyekiti CHADEMA taifa Freeman Mbowe akikagua uhai wa chama Mkoa wa Lindi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akisalimiana na viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi vitongoji mpaka Jimbo waliofika katika kata ya Nambambo Jimbo la Nachingwea Mkoa wa Lindi.

Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akisaini kitabu cha wageni katika kata ya Nambambo Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi na Kushiriki kikao cha ndani chenye lengo la kukagua uhai wa chama na kuwashirikisha viongozi wa chama ngazi ya vitongoji mpaka ngazi ya Jimbo pamoja na kuwashirikisha viongozi wa kiserikali waliotokana na CHADEMA.

Akifungua kikao cha ndani Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini, Mhe. Namangaya amemueleza Mwenyekiti wa chama Taifa ikiwa ni pamoja na kuonyesha jinsi mwamko mkubwa wa watu wa Mkoa wa Lindi wanavyoyataka mabadiliko.

Huku Mbunge wa Ndanda Mhe. Cecil Mwambe akiwahakikishi viongozi wa kichama kuanzia ngazi ya vitongoji mpaka Jimbo waliofika kwenye kikao hicho kushirikiana nao ili kubadilishana uzoefu ambao utapelekea kupata mafanikio kama walivyopata watu wa Ndanda kwa kumchagua na kuwatumikia na kuwaahidi kutumikia watu wa Mkoa wa Lindi kama anavyowatumikia watu wa Mkoa wa Mtwara.
IMG-20161125-WA0068.jpg
IMG-20161125-WA0064.jpg
IMG-20161125-WA0063.jpg
IMG-20161125-WA0062.jpg
 
Huko Nachingwea na kusini kwa ujumla wanajisumbua bure. Kwa sasa hawataki kabisa kusikia kuhusu CHADEMA. Labda Ndanda kidogo
 
Siasa za kimya huwa kisiasa hatari zaidi kuliko siasa za majukwaani. Hizi ndizo zinaitwa siasa za kimkakati ambazo huakikisha ushindi. Ndio maana huwa namkubali mashinji zaidi ya slaa.
Ktk vita jeshi muhimu kabisa huwa ni jeshi LA ardhini si la angani. Huu ndio uzoefu MPYA aliouleta lowassa cdm
 
Enzi hizo shamrashamra watu mitaani na picha za Mapokezi nyomi la kufa mtu. Sikuhizi kimya kimya kama wanaogopa kufumaniwa.

Jamii forums wenyewe wamebaki wawili tu. Akiacha kutoa update za Chadema Mwanahabari Huru na Francis12 basi tena chama kitajifia.
 
Back
Top Bottom