Mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Njombe ahamia CCM

Ameamua kugeuka
Screenshot_2019-10-05-09-20-24.jpeg
 
Aisee
*MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA NJOMBE AJIUNGA NA CCM ASEMA RAIS MAGUFULI ANASTAHILI KULINDWA*

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Njombe Ndg, Edwin Swalle na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Jimbo la Lupembe Mkoani Njombe Ndg, Msafiri Mpolo wametangaza kukihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Ndg, Edwin Swalle na Ndg, Msafiri wametangaza uamuzi huo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe, na kupokelewa na Viongozi wa CCM wakiwemo Madiwani kutoka Kata mbalimbali Wilayani Njombe waliokuwa wakiendelea na Kikao chao na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi, Ruth Msafiri.

Licha ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Edwin Swalle ni Wakili Msomi na alikuwa Mwanasheria wa Chama hicho pia ni Miongoni mwa Wagombea nafasi ya Ubunge Mwaka 2015 katika Jimbo la Lupembe kupitia CHADEMA akishindana na Mbunge wa Jimbo hilo aliyeibuka Mshindi kupitia CCM Mhe, Joramu Hongoli.

Akitangaza Kuihama CHADEMA na Kujiunga na CCM Wakili Swalle amesema hana Chuki na Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mhe, Joramu hongoli badala yake atatumia Taaluma aliyonayo kuhakikisha anamsaidia Mbunge huyo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli katika Kutekeleza Majukumu yao.

“Bahati Pekee ambayo Tanzania tumeipata ni hii ya kumpata Rais Magufuli, hatakiwi kutukanwa bali anahitaji kuungwa Mkono, haitaji Kukosolewa ila anahitaji kulindwa na kushauriwa ili azidi kututumikia Watanzania, tumeona Soko la Kisasa, Stendi kubwa na Hospitali kubwa Imejengwa Njombe ” Bw, Swalle.

Hatahivyo amesema Ameamua Kujiunga na CCM bila kushauriwa na Mtu yeyote ni Baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho unaofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli ambae ameamua kuirudisha Heshima ya Chama Cha Mapinduzi Nchini.

“Nilikuwa Nchini Afrika Kusini ilipotua Ndege ya Tanzania Wenzetu kule wanasema Magufuli anaingia Nchini nikatafakari sana na kuona kweli Rais Wang ni mtu wa kuungwa Mkono na kila Raia mwema wa Tanzania mwenye nia ya kutaka Taifa hili lizidi kupaa kiuchumi” Ameeleza Wakili Msomi Edwin Swalle.

Msafiri Mpolo alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Jimbo la Lupembe amesema kwasasa vyama vya Upinzani ikiwemo CHADEMA havina tena Ajenda zitakazo wasaidia kuikosoa CCM kwakuwa chama hicho kupitia Serikali yake iliyoko Madarakani kimemaliza hoja zote za Upinzani.

“Nataka niwaeleze Vijana wenzangu wa Njombe sasa Vyama hivi vya Upinzani havina tena Hoja ya kuikosoa CCM, nyakati zimebadilika Chama hiki tulichokuwa tunakikosoa kimeamua kubadilika kimemaliza hoja zote za Upinzani hivyo haina haja ya kuendelea kushangaa naomba katika kipindi hiki kifupi tutumie nafasi hii kubadilika” Msafiri Mpolo.

Mbunge wa Jimbo la Lupembe kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe, Joramu Hongoli amempongeza Wakili Swalle kwa kuamua kujiunga na CCM na kusema, anaamini watashirikiana katika kuwatumikia Wananchi wa Lupembe na Mkoa wa Njombe kwa ujumla.

Baada ya kujiunga na CCM Wanachama hao kutoka CHADEMA Wamekabidhiwa Kadi za Chama Cha Mapinduzi na kula Kiapo cha Uadilifu ndani ya Chama mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Ndg, Edward Mgaya, ambae amewakaribisha ndani ya Chama hicho na kuahidi kuwa CCM itawapa ushirikiano wa karibu.

Awali Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe Ndg, Hanafi Msabaha alisema, Wakili Swalle aliandika Barua na kuikabidhi Ofisini kwake akiomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi Ombi ambalo CCM kupitia Vikao vyake iliona ni vyema kumpokea kwakuwa ni Kijana Msomi ambae atakuwa Msaada ndani ya Chama na Serikali.

*KAZI NI KIPIMO CHA UTU, CHAPA KAZI TULINDE UHURU NA UTAIFA WETU, Imetolewa na Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.*
 
Sasa naelewa kwanini Mbowe anaendelea kuwa Mwenyekiti.Vijana wenye uchu wa madaraka ni rahisi kupoteza uaminifu kwa chama
 
Leo nimesikitishwa, Leo nimepitia YouTube nikiangalia ziara ya mh. Rais Kule Songwe, rais ameonyesha ubaguzi mkubwa sana kwa wananchi kisa tu walichagua mbunge na madiwani Wa chadema badala ya ccm.rais anashindwa kutatua kero za watu kisa walichagua upinzani, hivi rais anawabagua watu kisa walichagua upinzani huku Kodi zao wanachukua, rais ukishachaguliwa wewe ni Wa wote, wale waliokuchagua na wasiokuchagua.Rais anapaswa kushirikiana na viongozi wote bila kujali vyama vyao.mambo ya uchaguzi yakishapita tusonge Mbele.Vyama Ni makundi tu, lakini rais akumbuke sisi sote ni watanzania.
 
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe wakili msomi Edwin Swale akiambatana na mwenyekiti wa Bavicha wameiacha Chadema na kujiunga na CCM.

Wakili Swale amesema kwa sasa hakuna mtanzania mwenye akili timamu ambaye ataendelea kumpinga Rais Magufuli kwa sababu Maendeleo anayoyaleta yanaonekana.
Amesisitiza kuwa kwa sasa kupingapinga kila jambo ni ushamba.

Chanzo: Channel ten tv!
 
middle class aliyetosheka na maisha ,anakaa na kuja na uzi kama huu,but anaelewa kuwa positive progress yeyote ile inaletwa na mambo mengi including kuwa na ushindani,na bila shaka mtoa hoja analijua hili kuwa katika maisha ushindani ni muhimu mno,siku ambayo working class yetu itakapotambua hili nchi itasogea mbele,for now ni ulazimishaji wa mambo,mpangaji wa magogoni ana nguvu za nusu Mungu,he can over run kila kitu ndani ya nchi yetu!na sisi tunapiga makofi tu reason behind njaa ya matumbo yetu.
 
Kama angebaki angeweza kuzungumza mengi ikiwepo ajira, kilimo, deni la taifa, demokrasia nk. Mtu asiyejua siasa tu ndio atakosa cha kuongea.
Kinachowafanya watu kuhama au kuunga mkono juhudi ni uchu wa Madaraka.
Jamaa wamemchezea kekundu kaunga mkono juhudi halafu wenyeji wake wamesepa wamemuacha mpweke heshima aliyokuwa anapata Chadema haipo tena.Asipozichanga karata vizuri ndo Mwisho wake wa siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom