Mwenyekiti, CHADEMA asili tunakuangalia

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,330
21,419
Ndugu watanzania
Chadema asili mwaka juzi tulitoa tamko letu kuwa haturidhiki na mwenendo wa mwenyekiti wetu ,

jinsi anavyokiratibu chama na kusahau misingi ya chama ambayo ni uanaharakati na kutuletea watu waoga wa maamuzi kwenye chama,

Leo hii tupo tena hapa kumueleza mwenyekiti wetu ndugu mbowe kamanda mkuu,hivi sasa kuna mapungufu mengi sana ya kimaamuzi tangu aingie huyu katibu mkuu kama vile hayupo

vilevile john mnyika amepotea kabisa,hapa tatizo kubwa mwenyekiti wetu ni suala la uchaguzi wa kanda unaoendelea tumeshuhudia vituko vingi na kidogo ni hivi

kanda ya nyasa umeingilia uchaguzi kaskazini uchaguzi umeuharisha bila ya kuainisha sababu zake hatujui hiyo pesa ya marudio ambayo ilitakiwa ijenge chama itachezewa bila ya sababu .

Kule kusini viongozi wamevuliwa vyeo ,na kanda ya pwani ndugu mwenyekiti umetuletea mlemavu wa siasa ambaye anakurupuka kipindi cha matukio na ukijua ukitoka kaskazini hii kanda ya pwani ndio inayofuatia kwa shughuli nzito ,

alitakiwa apatikane mtu kweli sio bora mtu na kwani lazima alikuwa apewe cheo angebaki kuwa mshauri tu,jingine ni hili la ubunge wa afrika mashariki jana tumepata mshtuko mkubwa kusikia chama chetu kimekosea taratibu za kuwakilisha majina wakati tayari ni wazoefu katika hilo pengine nimalize kumwambia mwenyekiti mbona chadema ina hazina kubwa ya watu kwani ilikuwa ni lazima ya masha na wenje .

Wao wangebaki kujenga chama tu na la mwisho tunampa pongezi kamanda wa kweli aliobaki lissu kwa kuchaguliwa urais TLS na tumpe pole kamanda lema kwa mengi yaliomkuta lakini tupo nyuma yake!

Aksanteni

Chadema vyema sumu sumu kazi ngumu hatupigi ila tunaua kwa nini kwa sera!
copy kwa dkt slaa!
 
Mleta mada ni mamluki na pandikizi la ccm kama yupo cdm!
Huyu kiumbe kama yupo cdm atimuliwe mara moja maana anataka kuleta mpasuko ndani ya chama..
Cdm kipo imara na hakitatereka!
 
Mleta mada ni mamluki na pandikizi la ccm kama yupo cdm!
Huyu kiumbe kama yupo cdm atimuliwe mara moja maana anataka kuleta mpasuko ndani ya chama..
Cdm kipo imara na hakitatereka!
Kila anae sema ukweli ni mamluki eeh wacha woga!
 
Back
Top Bottom