Mwenyekiti CCM Mwanga ashindwa, Hai na Siha wapeta

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,773
21,325
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro Jaffar Kandege ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya wajumbe wa mkutano mkuu kumbwaga

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Oktoba 1, 2022, Msimamizi wa uchaguzi, Hamisa Chacha amemtangaza Ibrahim Mnzava kuibuka mshindi kwa kupata kura 396.

Amesema katika nafasi hiyo walioshindwa ni Mamboleo Mshana aliyepata kura 166, huku Kandege akipata kura 95.

Katika Wilaya ya Hai, Msimamizi wa Uchaguzi, Zuhura Chikira amemtangaza mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa Wilaya kuwa ni Wang’uba Maganda ambapo ametetea nafasi yake kwa kupata kura 335.

Amewataja wengine waliokuwa wakigombea katika nafasi hiyo na kura zao kwenye mabano kuwa ni Ibrahim Ndossa (235) Sophia Viggo (39) na Christopher Madulu (14) ambapo kura zilizopigwa zilikuwa 627, zilizoharibika 4 huku halali zikiwa 623.

Aidha Chikira amewatangaza washindi wa nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu Taifa, katika Wilaya ya Hai na kura zao kwenye mabano kuwa ni Mkuu wa Wilaya hiyo Juma Irando (411) Aikande Raymond Mushi (396) na Rusma Ndosi (388).

Katika Wilaya ya Siha, Msimamizi wa uchaguzi Ramadhan Mahanyu amemtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti, kuwa ni Wilfred Mossi ambapo ametetea nafasi yake kwa kupata kura 429, huku wagombea wenzake Luca Laizer akipata kura 17 na Edina Lukumai akipata kura 10.

Chanzo: Mwananchi
 
Uchaguzi wa HAI ULIKUWA WIZI MTUPU. Jumla ya wapiga kura wa mkutano mkuu wa Taifa walikuwa 2500 jambo ambalo sio kweli.
Chogolo fika HAI hali sio shari
 
Back
Top Bottom