Mwenyekiti CCM mahakamani kumdai rushwa Padri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti CCM mahakamani kumdai rushwa Padri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 1, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Aldo Kaduma, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Iringa, akituhumiwa kujifanya Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Kada huyo anadaiwa kuomba rushwa ya Sh. 400,000 kutoka kwa Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ihemi, Iringa Vijijini.

  Kaduma, Mwenyekiti wa CCM Mtaa wa Kiodombi, Iringa Vijijini, anadaiwa kupokea rushwa ya Sh. 150,000 kati ya Sh. 400,000 alizoomba kupatiwa, akijifanya Ofisa wa Takukuru ili asifichue na kushughulikia taarifa za kuwepo kwa tukio la mwanafunzi wa kike wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Ihemi kutoroshwa na kuwekwa kinyumba na mfanyakazi wa padri huyo. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alimtishia Padri Pio Callegarri, raia wa Italia kwamba iwapo asingempa dau hilo, angehakikisha anafukuzwa nchini ndani ya saa 24.

  Mwendesha Mashitaka wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Imani Nitume, akisaidiana na Restituta Kessy, walidai kuwa mtuhumiwa huyo aliwatishia pia walimu wawili wa Shule ya Msingi Ihemi, baba mzazi wa mwanafunzi na kijana anayedaiwa kumuweka kinyumba mwanafunzi huyo wa miaka (17) kwamba wangefungwa miaka 30 kila mmoja iwapo asingepewa fedha hiyo. Ilidaiwa kwamba waliotishiwa kufungwa miaka 30 kwa kumuoza mwanafunzi huyo kinyume cha sheria kama wasingempa rushwa hiyo ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ihemi, Chungueni Kiyao (32) na Mwalimu Mkuu Msaidizi, Edga Mkwama (30). Wengine ni baba mzazi wa mwanafunzi huyo Vallence Mnyenyelwa (44), Msaidizi wa Padri, Anthony Maginga (37) na Tony Kapinga (35) kijana anayedaiwa ndiye aliyemuweka kinyumba mwanafunzi huyo kama mkewe.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mapadri wa siku hizi nao vipi? Kama hahusiki na uzinzi huo kwa nini asikatae kutoa rushwa. Tena kwa bahati nzuri ni raia wa kigeni ambaye polisi wasingeweza kumtendea kama wanavyotutendea sisi. Hakupaswa kuwa mwoga! Hii ni dalili ya kuhusika.
  Siku hizi mapadre kuzini na vibinti vya shule imekuwa mtindo na kanisa linakaa kimya!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Huyo padre hahusiki, ila mtumishi wake ndiye mhusika, na huyo mwenyekiti alijua mhusika hana uwezo wa kumpa pesa na akajua yule padre ni wa taifa la nje ambaye ni mzungu, alitumia utashi wake wa chama kushika hatamu kumtishia kiongozi wa kiroho ampe cho chote ili kumnusuru mtumishi wake, lakini dhamiri ya padre imepelekea shauri hilo kufichuka na sasa ndo hivyo kada wa CCM yuko kizimbani kwa matakwa ya kupingana na sheria ya Mungu ya kaizari mpeni kaizari na ya Mungu mpeni Mungu.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  huyu bwana mwenyekiti wa ccm baada ya kusikia kuna denti kawekwa kinyumba alienda kwa padre huyo na kumtishi kuwa yeye ni afisa wa takukuru na hivyo anataka apewe hiyo pesa ili azime msala uliompata mfanyakazi wa padre huyo.....huyo pader akakubali ila akamuahidi siku ya kwenda kuchukua....baada ya hapo padre alienda iringa mjini ofc za takukuru na kuulza kama kuna mtu wa jina hilo pale ofcn ....ndipo aaambiwa hakuna naakaeleza kila kitu na hapo ndipo mtego ulitegwa.......yule mwenyekiti mwizi wa chama cha magamba alipigiwa simu na padre na kuelekezwa mahali ili aende akapewe hiyo pesa kwa ahadi kuwa pesa nyinge atapewa baada ya siku mbili ila leo anapunguza......

  ndipo kada wa magamba akajipeleka na tumbo lake hadi kule akashikishwa mlungula ule na papo hapo akatiwa kimiani na maofisa wa takukuru
   
 5. e

  ebrah JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Safi sana, sasa njia kama hizi na nyingine kubwa tuzitumie kwa hawa wakubwa wao wanaoomba 10% za mikataba daily!
   
 6. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  njaa inasumbua jamani..posho posho posho si mnajua sasa hv vikao havipo,rushwa za wagombea etc?. siyo kosa lake..ni kosa la mfumo anaoutumikia!
   
Loading...