Mwenyekiti BAWACHA Segerea Agnesta Lambert: Naomba radhi usumbufu mlioupata viongozi wa chama na watanzania wote

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
NAOMBENI RADHI KWA USUMBUFU MLIOUPATA VIONGOZI WANGU WA CHAMA NA WATANZANIA WOTE HUSUSAN WANACHAMA WENZANGU..

KWANZA kabisa namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa uzima na afya aliyonikrimia mpaka sasa!!

PILI nitumie nafasi yangu kuwaomba radhi viongozi wangu wote kwa usumbufu mlioupata kupitia andiko ovu dhidi yenu lililopostiwa kwenye ukurasa wangu wa Facebook jana jioni,andiko ambalo sihusiki kabisa kuliandika wala kumtuma yeyote aliandike na kulisambaza!!Sambamba na hilo niwambe sana radhi wafuasi wangu kupitia Facebook na mitandao mingine ambayo andiko hili limefika,najua mmefadhaika sana maana mnanifahamu vema nilivyo kwa chama changu na viongozi wote....Ukweli ni kwamba sihusiki!!!

Account yangu imekuwa hacked jana jioni,na kwa kuwa sijaingia Facebook kwa takribani week tatu sikujua kinachoendelea mpaka pale nilipopigiwa simu na baadhi ya watu wakiniambia account imekuwa hacked....Nilifanya haraka kuingia kwenye account yangu lkn bahati mbaya nilikuta wameishachange kila kitu....Sikuweza kuingia!!

Kwako mwenyekiti wangu TAIFA (mhe Mbowe)ktk uhai wangu duniani sitakuja kukukosea adabu kwa njia yote ile maana najua ni vipi unalipigania taifa hili bila kujali unayopitia...Mimi ni kati ya VIONGOZI/wanachama walio tayari kupigana pamoja nawe ktk vita hii ya ukombozi wa kweli,nakuomba sana endelea kupuuza hawa watu waliochoka mapambano!!!Watu ambao badala ya kuwaza kupambana na udicteta uchwara wanawaza UENYEKITI taifa!!

Katibu wangu Taifa (Dr Mashinji)naomba endelea kuwapuuza hawa ambao kimsingi uenda hakufurahishwa na ww kuwa katibu (wivu)na sasa wanatafuta wafuasi kupitia jina langu!!Wamepotea njia!!

Mwenyekiti wangu BAWACHA Taifa, (MHE Halima Mdee)ww ni Kiongozi wangu,unanijua vema,dhamira yangu njema kwako unaijua, hao walikuandika wanatafuta kick,Wanatafuta kuzima nyota yako kali,kukuchonganisha Na viongozi wako wanaokutakia heri nk...Wanajua jinsi ambavyo kupitia ww baraza la WANAWAKE CHADEMA limekimbiza Mpaka UWT haisikiki tena,hii ni vita ya uchaguzi mkuu,endelea kuwapuuza!!!Binafsi bila ww nisingekuwa imara kama nilivyo sasa,hivyo kukugusa siwezi!!Na pia siwezi kumstahi anayekugusa kwa lengo la kukuchafua!!

Mhe Peter Msigwa naomba endelea kupuuza hawa vibaka, wamekutafuta kitambo wakachemka sasa wamekuja kwa njia nyingine japo ni dhaifu.....Unanijua pia,na unajua vema siwezi kufanya ujinga huu....

Mhe John Mrema uzuri ww umepitia mengi,hili ni cha utoto,kiongozi wangu,Agnesta Lambert unayemjua kamwe hawezi kuandika ujinga ule...

Mhe Hawa, najua ulipoona hilo andiko ukiwa nawe umetajwa uliishia kucheka kama alivyocheka mhe MDEE!!hii ni vita ya uchaguzi mkuu!!Lkn ni vita dhidi yangu ili nirudi nyuma,lkn ili viongozi wangu wakose imani na Mimi.. .Sitorudi nyuma....!!

Mwenyekiti Kanda ya Pwani(mhe Sumaye)ww pia wanijua vema kwa kipindi hiki ambacho umeniongoza,kamwe siwezi kuandika wala kuamini huo ujinga...

Katibu wangu Kanda ya Pwani (mhe Mabina)naomba kiongozi wangu puuza huo ujinga,sihusiki kabisa!!

Dada zangu (mhe Matiko na mhe Mwakagenda)Ukweli wa hiki mnaujua, naomba endeleeni kupuuza huu ujinga!!Mimi sihusiki!!!

Mwisho kabisa niwashukuru sana wale wote mliosaidia kwa njia moja ama nyingine kusambaza kanusho langu ili kuwajulisha wengine wajue...Nilichojifunza WANACHAMA wenzangu na watanzania kiujumla mna imani kubwa na mm,imani hii sitaichezea kamwe!!Naomba tuendelee kukijenga chama chetu,tuendelee kuwasapoti viongozi ili waweze kutufikisha panapostahili
1f64f_1f3fb.png
.

AGNESTA LAMBERT
Mwenyekiti BAWACHA Jimbo La SEGEREA
 
Uvccm wana uwezo mdogo sana wa kujenga hoja hata sisi wananchi tuliwapuuza na tutaendelea kuwapuuza
 
Mi naomba kuuliza tu....Amesema watu wamekwamnia Account yako imekuwa hacked.... yani badala ya ww kujua imekuwa hacked hao waliojua wamejuaje kwani naamini hata wewe unaakili timamu unaweza kupost ule ujumbe....Ila ok mi nashukuru kwa kuukana siasa za kipuuzi hizi zakuwalisha watu maneno na ku hack Account za watu...hahahahaha
 
UVccm ni ugonjwa hatari ambao mpaka sasa nalishangaa shirika LA afya duniani halijautangaza au wametishiwaaaaaa.pole sana waovu huwa hawafinikiwi sababu wamekosa baraka za Mungu.
 
Nimewazoea wanasiasa uchwara wakiwa na nyongo wanatapika wakimaliza wanaomba radhi kwa kisingizio Cha akaunti ilikuwa hacked ila Meseji inakuwa imemfikia mlengwa hahahhaaa watakusamehe tu wewe sio wa kwanza maana nyongo unayo, kibarua unakitaka huna jinsi mkuu omba msamaha maisha yaendelee
 
Back
Top Bottom