Mwenyekiti atishia kwenda kwa Rais mbele ya Waziri Lukuvi

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,827
2,000
3 Mar 2021
Mtoto wa Muasisi wa TANU uso kwa uso na Mh. Lukuvi, matatizo ya ardhi jijini Mwanza


Leo March 03, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Makazi William Lukuvi amekutana na Watumishi wa Jiji la Mwanza idara ya ardhi na wengine, Waziri Lukuvi akiendelea na kikao nje kukawa na Wananchi wenye migogoro wakiwa na mafaili yao wakimgoja

Source: Millard Ayo
huyo mhe. lukuvi nae si msikilizaji mzuri huyo mzee anakitu sema namna yk ya uwasilishi ni mzunguko ...aende tu huko kwa rais :p :p :p
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,718
2,000
Mimi naona waziri yupo sahihi kwasababu huyo mzee ameanza kuweka title ya mzee wake ili asikilizwe, badala ya kuweka taarifa zinazoonesha anastahili hiyo ardhi.

kwanini aanze mimi ni mtoto wa muasisi wa Tanu?....Waziri ameogopa kuonekana anapendelea watu ambao ni waasisi wa nchi.

Waziri yupo sahihi japo kuna sehemu amekosea anaelekezwa anakuwa kama hataki kusikiliza hiyo inatokana na jamaa kuwa kama amemdharau
Kiongozi ni mtu ambaye unatakiwa umheshimu Japokuwa hiyo haifanyi kiongozi naye asiheshimu wengine.

Jamaa alitakiwa kuwa mpole na asigie kabisa neno baba yake alikuwa muasisi sijui nini.

Muasisi keshakufa usiishi kwa tittle ya baba ako
 

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
2,609
2,000
Kiongozi ni mtu ambaye unatakiwa umheshimu Japokuwa hiyo haifanyi kiongozi naye asiheshimu wengine.

Jamaa alitakiwa kuwa mpole na asigie kabisa neno baba yake alikuwa muasisi sijui nini.

Muasisi keshakufa usiishi kwa tittle ya baba ako
kweli mkuu hakutumia hekima na alitumia approach mbaya kumtaja baba ake (muasisi wa nchi hii) mbele ya waandishi wa habari na watu wengine,

Pia inamaana Lukuvi angemnyenyekea habari ingeonekana kuna watu wanapendelewa sababu ya wazee wao....

nafasi kama hizo ni adimu kuzipata na inabidi kutumia maneno yasiyoudhi na jazba.....mtu unamuomba msaada akusaidie ila unamuomba kwa jazba na kujimwambafai, hawezi kukusaidia maana kila mtu anapenda aheshimiwe.
 

cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
21,784
2,000
Ukiitizama hii video kwa makini ukiwa neutral kabisa utagundua huyo mwananchi ana changamoto kidogo ktk akili yake,hana utulivu kabisa.
Ndg Lukuvi alipaswa kuwa mtulivu kwa kuliona hilo angeahirisha kumsikiliza kwa kumuambia tu kwa utulivu wewe jambo lako ni zito tuonane pale ofisini.

Akija ofisini unachukua mabarua yake hayo unamuambia kaa hapo kunywa chai usizungumze,unazisoma ukielewa unatoa uamuzi.
Uongozi ni pamoja na uvumilivu wa kumudu personality za Watu.
Hakika kabisa, ila huyu waziri kakosa kabisa ustahimilivu, hafai kua kiongozi wa umma.
 

nsalu

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
833
1,000
Anyways, sishangai anavyomjibu Mh. Lukivi, nashangaa jinsi wanavyohemeana walivyo lundikana na Corona hii na hakuna aliyevaa barakoa hata mmoja.

Please watanzania, tuache utani, people are dying!!
Na mimi.nimeshangaa Sana, halafu Dr Kitima aliongelea watu kuchukua tahadhari anatukananwa
 

cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
21,784
2,000
..hiyo ya kumtaja baba yake nadhani ni kutokana na usumbufu aliopitia, na machungu aliyokuwa nayo.

..na pia anataja uasisi wa baba yake kwasababu ardhi "iliyodhulumiwa" ilikuwa mali ya muasisi.

..nadhani mlalamikaji alitaka kuonyesha jinsi watu wanaodhulumu walivyoota "mapembe" kwamba hawaogopi mali za mtu yeyote yule.

..binafsi sielewi kwanini Waziri Lukuvi alichukia baada ya mlalamikaji kusema yeye ni mtoto wa muasisi wa tanu. kwa kweli I dont see anything wrong kwa mtu kuwa mtoto wa muasisi. Sio dhambi.

..kingine kilichoonekana kumkera Waziri Lukuvi ni mlalamikaji kumtaja Edward Lowassa kwamba aliwahi kulitolea maamuzi suala lake. Inawezekana Waziri Lukuvi alidhani Edward Lowassa bado yuko Chadema.
Wee ndo umeongea ukweli sasa.
 

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
6,067
2,000
Huyu mwananchi alikosea sana kutanguliza kuwa yeye ni mtoto wa muasisi wa Taifa hili, hiyo haikuwa shida yake, shida yake ni kudhulumiwa ardhi, alitakiwa kulenga point yake na sio kutanguliza ujuaji mbele.
Kumwambia Lukuvi kuwa atakwenda kwa Rais ni kujitia kiburi kisicho na faida, hawezi onana na Rais kwa mbwembwe zile, ikitokea miujiza akaonana na Rais basi atarudishwa kwa Lukuvi na atarudi akiwa mpole mno au aamue kuachilia mbali hilo eneo.
 

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
650
1,000
Hebu jiite bas faster tuwe pacha tusiofanana,
sitaki kulibadili maana kila mtu atalijua wakat mi nataka ulijue peke yako tu na kuanzia leo mi jina langu naitwa Fantastic kwajili yako...mi pacha wako wa hiarai.. I hope umenielewa pacha.
 

Gobole

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
1,012
2,000
dah nimechekaa ulimjibu kibabe
Bro sio wote tunachukulia poa kua undermined or kua intimidated for no reasons at all...kuna ka shetani fulani ka umaskini jeuri hua kanaamka kanakunong'oneza huyu anakuchukulia poa ndo mana anakutisha...
kwanza Waziri kajitahidi sana kumpa round 3 za kumuomba ajieleze vzuri ila still jamaa akaendeleza swaga za uasisi wa babake or ile ya ntamwambia raisi hii yote akitaka kumtisha waziri na kutaka special privileges...mimi alivyoanza tu ningesepa nikamuacha hapo. Waziri ni muwakilishi wa Raisi km humuheshim means hujamuheshim Raisi, sidhani km angekua Raisi angemuongelesha kwa tone ile.
 

cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
21,784
2,000
sitaki kulibadili maana kila mtu atalijua wakat mi nataka ulijue peke yako tu na kuanzia leo mi jina langu naitwa Fantastic kwajili yako...mi pacha wako wa hiarai.. I hope umenielewa pacha.
Imeisha hiyooooh
 

Jaby'z

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
4,111
2,000
Ukiitizama hii video kwa makini ukiwa neutral kabisa utagundua huyo mwananchi ana changamoto kidogo ktk akili yake,hana utulivu kabisa.
Ndg Lukuvi alipaswa kuwa mtulivu kwa kuliona hilo angeahirisha kumsikiliza kwa kumuambia tu kwa utulivu wewe jambo lako ni zito tuonane pale ofisini.

Akija ofisini unachukua mabarua yake hayo unamuambia kaa hapo kunywa chai usizungumze,unazisoma ukielewa unatoa uamuzi.
Uongozi ni pamoja na uvumilivu wa kumudu personality za Watu.
You are very bright sir.
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,022
2,000
Huu ndio kweli wenyewe, hawa viongozi wakiwa mawaziri,wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanawatumia hawa maofisa wa Ardhi kupata viwanja na mashamaba sehemu wanakoongoza!! Inakuwa vigumu sana kuwathibiti maofisa ardhi pale wanapokiuka taratibu na kuwadhulumu wananchi!! Lukuvi is no exception; ana viwanja Mwanza, Arusha ,Dar, Dodoma na mashamba Kilosa!!!! Kwa mtindo huo anatupiga dongo la macho tu pale anapokuwa kwenye TV akiwakaripia maofisa ardhi!!!
Pale Iringa alipima viwanja vingi, zaidi ya 12. Sijui anataka vya nini! Anaowatumia watupa taarifa mitaani. halafu anajidai kutatua migogoro Mwanza wakati anafuatilia maeneo ya kupata viwanja!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom