Mwenyekiti atishia kwenda kwa Rais mbele ya Waziri Lukuvi

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,774
2,000
Jamaa ana kiburi. Utoto wake wa mwasisi unatuhusu nini sisi? Angesema tu mimi ni mwananchi mwenye tatizo ABC. simple like that. But kujimwambafy kwingi na mikwara mwishoni anaonekana anafanga fujo. Na anaonekana amesoma. You hit the point. Then unapoulizwa maswali mengine ndo unatoa maelezo. Unaposema mwenzako XXX alisema au alifanya hivi. Unakosea pia. Huyu ni Lukuvi na yule ni lowassa. Hapa hata kama humpendi Lukuvi ila si sahihi mtu adhalilishwe hivi kwa kisingizio cha utoto wa mwasisi. Asonge mbele.
 

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
2,838
2,000
Jamaa ana kiburi. Utoto wake wa mwasisi unatuhusu nini sisi? Angesema tu mimi ni mwananchi mwenye tatizo ABC. simple like that. But kujimwambafy kwingi na mikwara mwishoni anaonekana anafanga fujo. Na anaonekana amesoma. You hit the point. Then unapoulizwa maswali mengine ndo unatoa maelezo. Unaposema mwenzako XXX alisema au alifanya hivi. Unakosea pia. Huyu ni Lukuvi na yule ni lowassa. Hapa hata kama humpendi Lukuvi ila si sahihi mtu adhalilishwe hivi kwa kisingizio cha utoto wa mwasisi. Asonge mbele.
Hana adabu Yule mzee kabisa, lukuvi angemsaidia ningeshangaa sana ,eti mwenzako kah,
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,161
2,000
Supreme power ya waziri haionekani
Nadhani kuna gap mihimili isije kuingiliana hapa
Yeye anasema rais hajui kuwa waziri anamwakilisha rais
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,395
2,000
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.

Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.

Mitano tena!
hapana zile ni hasira mkuu.
imagine mtu unaendesha kesi kwa miaka 30 bado unapigwa danadana tu lazima ujitoe ufahamu.
 

Kiraka

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
3,483
2,000
Nadhani Waziri kakosea, alipaswa awaachie hata wasaidizi wake waongee naye.

Shida Waziri anataka sifa kwa rais, ndio maana anataka majibu rahisi tu kwenye kamera aonekane katatua shida, mambo yakiwa na mkanganyiko kidogo ana panic. Raia nae anaona kabisa huyu Waziri hawezi kunisaidia mpaka niende kwa rais. Na pengine labda anajua historia fulani kuhusu huyo waziri katika miaka yake 30 ya kupambana na hiyo kesi.
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,395
2,000
Mimi naona waziri yupo sahihi kwasababu huyo mzee ameanza kuweka title ya mzee wake ili asikilizwe, badala ya kuweka taarifa zinazoonesha anastahili hiyo ardhi.

kwanini aanze mimi ni mtoto wa muasisi wa Tanu?....Waziri ameogopa kuonekana anapendelea watu ambao ni waasisi wa nchi.

Waziri yupo sahihi japo kuna sehemu amekosea anaelekezwa anakuwa kama hataki kusikiliza hiyo inatokana na jamaa kuwa kama amemdharau
ile ni jazba ya kudhulumiwa haki na inaweza kumkuta mtu yeyote.
Imagine leo hii uambiwe nyumba unayoitegemea kuishi inatakiwa ibomolewe pajengwe soko,au udhulumiwe uambiwe hustahili kukaa hapo.
Lazima ufahamu uruke mzee baba usifanye masihara
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
12,617
2,000
Eti mtoto wa muasisi wa TANU that's nosense...!!?
wazili anamwambia aende kwenye point yy analeta longo longo na jazba utadhani lukuvi ndio amempora ardhi?
ningekuwa mm ndio waziri huyo Bwana majazba ningemtandika kibao cha usoni...
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,395
2,000
Ukiitizama hii video kwa makini ukiwa neutral kabisa utagundua huyo mwananchi ana changamoto kidogo ktk akili yake,hana utulivu kabisa.
Ndg Lukuvi alipaswa kuwa mtulivu kwa kuliona hilo angeahirisha kumsikiliza kwa kumuambia tu kwa utulivu wewe jambo lako ni zito tuonane pale ofisini.

Akija ofisini unachukua mabarua yake hayo unamuambia kaa hapo kunywa chai usizungumze,unazisoma ukielewa unatoa uamuzi.
Uongozi ni pamoja na uvumilivu wa kumudu personality za Watu.
uko sahihi kabisa mkuu,ilikuwa ishu ndogo sana.
Mtu ukishamjua ana matatizo mpe kichwa atatulia tu.
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,395
2,000
Mi mwenyewe hizi swaga za mimi fulani or usipofanya ntamuambia boss wako hua siziwezi aisee...
kuna siku PS wa director pc yake ilizingua akanipigia simu bt at the time nlikua nna issue nyingine, nikamwambia weka request yako kwenye helpdesk wengine waje kukusaidia or nikimaliza ntakuja kukusaidia akanipa swaga za ntaenda kuchukua laptop ya director nitumie hadi utakapokuja just to intimidate me...nikamwambia kachukue ila ukienda kuchukua siji kabisa maana utakua ushapata laptop ya kufanyia kazi nikakata simu nikendelea na issue zangu..kuna watu we don't work well na vitisho...
uko kama mimi aisee
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,395
2,000
Sikuwahi jua huyu Waziri ana kiburi na dharau hivi. Khaaah.
Rais amtumbue huyu waziri hafai kabisa.
Afu anajibu kijeuri "nenda kamuone Rais" jamani hata mshipa wa aibu hana.

nimecheka huyo mama anamlazimisha mlinzi amtoe nje huyo m/kiti,
M/kiti nae anajibu "wee mama usiseme hivo je angekua Rais hapa unaweza sema hivyo?"
walikutana pipa na mfuniko
 

Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
741
1,000
Haijalishi bado anahaki ya kusikilizwa sio kupuuzwa

Watu hatufanani na uasili hatufanani pia.

Kila mtu ana haiba na silika yake.

Huyu ndivo alivoumbwa.
Jee, hiyo haki ya kusikilizwa inatokana na yeye kuwa mtoto wa muasisi wa TANU akiwa na Nyerere? Ina maana watoto wa watu wa kawaida tu wasisikilizwe? Hili ndilo suala lililomghasi Lukuvi akadiriki kumpa nafasi mlalamikaji mara tatu ajikite kwenye tatizo lake. Mlalamikaji alishindwa mara zote tatu na ndipo Lukuvi akaamua kuachana naye. Nakubaliana na uamuzi huo. Tusisikilize mtu kwa kuwa tu yeye ni fulani bali tuangalie tatizo lenyewe.
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
14,004
2,000
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.

Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.

Mitano tena!
Tulianza na msemo wa serikali ya viwanda,ilipoishia hatujui hadi leo. Ikaja serikali ya Magu , ikaja serikali ya mi tena, hatujakaa sawa sawa ikaja serikali ya kujifukiza! Kwa sasa tupo kwenye serikali ya makaripio mipasho na onyo. Full comedy.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom