Mwenyekiti arejesha saruji aliyoichukua bila utaratibu

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Mwenyekiti wa Kijiji cha Namunda kilichopo kata ya Kitama kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Suleiman Mkubulu amerejesha mifuko 24 aliyoitumia kinyume na utaratibu kama alivyohaidi kuirudisha baada ya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu kugundua upotevu wa mifuko hiyo alipokuwa akifuatilia kwa makini ujenzi wa miradi ya maendeleo kijijini hapo.

Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Diwani kata ya Kitama, Mtendaji kata Kitama, Mtendaji Kijiji Namunda, Wajumbe Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi.

Akizungumza mara baada ya mifuko hiyo kukabidhiwa kimaandishi kwa Mtendaji wa Kijiji na kamati ya ujenzi, Gavana Shilatu aliwasihi sana viongozi kuelewa dhana ya utumishi na uongozi ni dhamana ya Wananchi na si mwanya wa kujitajirisha, kudhulumu au kuonea wengine kinyume na sheria.

*"Pasipo usimamizi imara, hii mifuko 24 ya saruji ingepotea. Ni lazima tutambue uongozi ni dhamana na si fursa ya kujitajirisha au kuonea wengine."* Alisema Gavana Shilatu

Tangu awali alipopata taarifa ya upotevu, Gavana Shilatu alisimama kidete hadi saruji hiyo kurejeshwa kwa ajili ujenzi wa miradi ya maendeleo ya ofisi ya Kijiji na Madarasa mawili na ofisi moja ya Walimu ya Shule ya msingi Namunda.
IMG-20190620-WA0835.jpeg
 
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Mwenyekiti wa Kijiji cha Namunda kilichopo kata ya Kitama kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Suleiman Mkubulu amerejesha mifuko 24 aliyoitumia kinyume na utaratibu kama alivyohaidi kuirudisha baada ya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu kugundua upotevu wa mifuko hiyo alipokuwa akifuatilia kwa makini ujenzi wa miradi ya maendeleo kijijini hapo.

Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Diwani kata ya Kitama, Mtendaji kata Kitama, Mtendaji Kijiji Namunda, Wajumbe Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi.

Akizungumza mara baada ya mifuko hiyo kukabidhiwa kimaandishi kwa Mtendaji wa Kijiji na kamati ya ujenzi, Gavana Shilatu aliwasihi sana viongozi kuelewa dhana ya utumishi na uongozi ni dhamana ya Wananchi na si mwanya wa kujitajirisha, kudhulumu au kuonea wengine kinyume na sheria.

*"Pasipo usimamizi imara, hii mifuko 24 ya saruji ingepotea. Ni lazima tutambue uongozi ni dhamana na si fursa ya kujitajirisha au kuonea wengine."* Alisema Gavana Shilatu

Tangu awali alipopata taarifa ya upotevu, Gavana Shilatu alisimama kidete hadi saruji hiyo kurejeshwa kwa ajili ujenzi wa miradi ya maendeleo ya ofisi ya Kijiji na Madarasa mawili na ofisi moja ya Walimu ya Shule ya msingi Namunda.View attachment 1132922
Hahahaa...... Nilidhani Mwenyekiti wa Chadema!

Natania tu.
 
mkuu, mwnykt was chadema hawezi kuthubutu kwnza ni MTU wa Mungu, na kila siku tunamuona madhabahuni akimuomba Mungu, labda kama unamsemea yule nkonki anaetakaga kuombewa kutwa ili atuibie vizuri😂😂
 
Back
Top Bottom