Mwenyekiti aliyezushiwa kujizuru na akina january makamba ,mkutano wake jana wafurika wananchi

PHILIPLULINDA

Senior Member
Jun 1, 2013
181
89
Mwenyekiti wa Chadema kijjiji cha Kwekitui jana alikiponda Chama cha Ccm kwa kusema ni chama mfilisi kwa sera kwani walimtishia kifo, lakini kwa sasa ameamua kuwatumikia Wananchi wa Kijiji hicho kwa tiketi ya CHADEMA, Akiongea mbele ya Mkutano Mkubwa wa Hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kwekitui,Alipokuwa akiwashukuru wananchi wake kwa kumpa kura za kishindo kwa tiketi ya CHADEMA.

Akiongea kwa kujiamini na Hali njema kabisa Anataka Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Athuman Kiberiti apandishwe Mahakamani kwa kuandika Barua feki na Kuisoma kwa ndugu January Makamba kwamba yeye eti kajiuzuru,

Ndugu Kasimu Miraji ambae ni Mwenyekiti wa Kijiji cha KWEKITUI JIMBO LA BUMBULI LUSHOTO TANGA, alikimbia kijijini miezi miwili iliyopita na kuzushiwa kwamba kajiuzuru.

Na Barua yake kusomwa mbele ya January alipokuwa ziarani Bumbuli na kwekitui.
Hapo jana Mwenyekiti huyo wa CHADEMA aliyeshinda uchaguzi mdogo uliofanyika miezi michache iliyopita,
alisema CCM hawana jipya na mwaka 2015 ,Wataona wembe Kuanzia kwa January na wagombea wote wa Ubunge wasijisumbue kuja Bumbuli , Bumbuli ni Jimbo la CHADEMA mwaka 2015.

Akiongea huku akishangiliwa na wafuasi na wananchi waliohuzuria Mkutanoni hapo.Wananchi hao walihoji JANUARY MAKAMBA ni nani? Huku wengine wakibeza kwa kusema JANUARY MAKAMBA ni mbunge aliyeingia madarakani k,upitia pesa chafu za RICHMOND NA EPA.

Kasimu alisema yeye ni chaguo la Wananchi wa Kwekitui baada ya uchaguzi kufanyika zaidi ya Mara mbili CHADEMA ikishinda lakini viongozi wa ccm wakawa wanadai eti Uchaguzi eti urudiwe na kila uliporudiwa Ndugu kasim alikuwa anaibuka kidedea.
 
Saaafi saaaaaana,nili mtweet january ili anipe ukweli wa suala la mwenyekiti huyo akaishia kurusha matusi,ngoja nimtafute tena!! Nimtaarifu
 
Afadhali ameshinda kesi ya nyani wanaotaka kukaa madarakani kwa lazima. Hongera kasimu na endelea kuwatumikia wananchi.
Pia mwenye taarifa yule mwenyekiti wa Ruaha wilayani kilosa mambo yake yanaendeleaje?.
 
Safi sana!
Hawa viongozi wa ccm sijui wakoje!
Hawa akina Mwigulu, Nape, Makamba mwenyenzi Mungu aliwajalia sauti, lakini aliwanyima akili!
Tanzania for CHADEMA in 2015!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ama kweli nimeamini magamba wana viwanda vya kuzalisha uongo, walikuja hapa kwa papara kubwa kumbe upuuzi mtupu! Mungu amjalie uzima na afya njema Mwenyekiti wetu!
 
Du walisema chama cha kikristu, ukanda ukabila, ugaidi nk.Kumbe hawajitambui ya kuwa walikuwa wanapiga promo,hapa Ritz,pil chama nk huwaoni wataingia tu na kutoka kama wapo lindoni.
 
Mwenyekiti wa Chadema kijjiji cha Kwekitui jana alikiponda Chama cha Ccm kwa kusema ni chama mfilisi kwa sera kwani walimtishia kifo, lakini kwa sasa ameamua kuwatumikia Wananchi wa Kijiji hicho kwa tiketi ya CHADEMA, Akiongea mbele ya Mkutano Mkubwa wa Hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kwekitui,Alipokuwa akiwashukuru wananchi wake kwa kumpa kura za kishindo kwa tiketi ya CHADEMA.

Akiongea kwa kujiamini na Hali njema kabisa Anataka Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Athuman Kiberiti apandishwe Mahakamani kwa kuandika Barua feki na Kuisoma kwa ndugu January Makamba kwamba yeye eti kajiuzuru,

Ndugu Kasimu Miraji ambae ni Mwenyekiti wa Kijiji cha KWEKITUI JIMBO LA BUMBULI LUSHOTO TANGA, alikimbia kijijini miezi miwili iliyopita na kuzushiwa kwamba kajiuzuru.

Na Barua yake kusomwa mbele ya January alipokuwa ziarani Bumbuli na kwekitui.
Hapo jana Mwenyekiti huyo wa CHADEMA aliyeshinda uchaguzi mdogo uliofanyika miezi michache iliyopita,
alisema CCM hawana jipya na mwaka 2015 ,Wataona wembe Kuanzia kwa January na wagombea wote wa Ubunge wasijisumbue kuja Bumbuli , Bumbuli ni Jimbo la CHADEMA mwaka 2015.

Akiongea huku akishangiliwa na wafuasi na wananchi waliohuzuria Mkutanoni hapo.Wananchi hao walihoji JANUARY MAKAMBA ni nani? Huku wengine wakibeza kwa kusema JANUARY MAKAMBA ni mbunge aliyeingia madarakani k,upitia pesa chafu za RICHMOND NA EPA.

Kasimu alisema yeye ni chaguo la Wananchi wa Kwekitui baada ya uchaguzi kufanyika zaidi ya Mara mbili CHADEMA ikishinda lakini viongozi wa ccm wakawa wanadai eti Uchaguzi eti urudiwe na kila uliporudiwa Ndugu kasim alikuwa anaibuka kidedea.

Woga hofu na mashaka ni adui wa Mungu,lakini upendo ujasiri na matumaini ni rafiki wa Mungu.TUSHIKE KIKAMANDA MANENO HAYA ILI TUMSUPPORT M/KITI KWA KILA JITIHADA.
 
Back
Top Bottom