Mwenye vyeti halisi anaweza kuwa hana tija, na wa aina hiyo ni wengi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Nimekuwa nikifuatilia hizi habari za serikali ya awamu ya tano kulishikia bango suala la elimu za wafanyakazi wa sekta nyingi nyeti. Kinachotafutwa ni mtu kula kwa jasho lake. Kinachotafutwa ni fairness katika suala zima la mtu kuajiriwa.

Lakini upo upungufu mwingi Tanzania kwenye suala la tija ya mfanyakazi mmoja mmoja (productivity). Mtu anaweza kuwa na vyeti original kabisa, vyenye kukubalika lakini akakosa uwezo wa kuongeza kitu kipya kazini kwake. Kuna wenye vyeti original ambao jinsi wanavyovipata, hali inakuwa haina tofauti na wale wenye vya kufoji.

Ipo haja kwa vyuo vikuu na vyenyewe kujenga mazingira ambayo hakutakuwa na ukaribu kati ya maprofesa na wanafunzi wao, haswa wale wanaosoma wakitokea makazini. Huu ukaribu unachangia katika taifa kuwa na wenye elimu ambao tija yao kama ipo basi ni ndogo sana.

Vyeti feki vilianza kuzaga baada ya internet cafes kuanza kuongezeka nchini, tatizo hili halikuwepo enzi zile za awamu ya kwanza na ya pili. Limekuwa ni tatizo kubwa kuanzia miaka ya Mzee Mkapa. Na kabla ya uwepo wa tatizo hili, nchi ilikuwa na wenye elimu waliozitokea jasho.

Ni vita ambayo ilikuwa kama sio leo basi kesho ianze kupiganwa, lilikuwa ni suala la muda tu. Natumaini mwanzo alioanza nao Profesa Ndalichako, utaendelea katika hali hii kwa miezi mingi ijayo. Jeuri ilizidi mitaani, dharau ilizidi, dhuluma ilizidi, uzembe ulizidi.

Lakini lililo muhimu ni kwa wizara ya elimu kuangalia mianya inayoweza kutengeneza wenye elimu wasio na tija nchini.
 
Umepika sehemu wapo wengi wana veti halisi lakini taaluma yenyewe hamna. Mtu anafeli ile inayoitwa "DISCO" anabadilishiwa kusup tatu ana fanya moja MSAJILI anaamuwa wahitimu wote wape veti. HIVI SIO VYA UFAULI ILA VYA KUHITIMU
 
Mkuu umesema kweli kabisa, ndio maana miaka ya nyuma nchi ilikuwa ikiingia mikataba mingi bila ya wenye elimu wetu kuelewa impact ya muda mrefu ujao ya wao kutia saini kichwakichwa. Elimu inatafutwa kwa juhudi kubwa ni lazima iheshimiwe.
 
Nimekuwa nikifuatilia hizi habari za serikali ya awamu ya tano kulishikia bango suala la elimu za wafanyakazi wa sekta nyingi nyeti. Kinachotafutwa ni mtu kula kwa jasho lake. Kinachotafutwa ni fairness katika suala zima la mtu kuajiriwa.

Lakini upo upungufu mwingi Tanzania kwenye suala la tija ya mfanyakazi mmoja mmoja (productivity). Mtu anaweza kuwa na vyeti original kabisa, vyenye kukubalika lakini akakosa uwezo wa kuongeza kitu kipya kazini kwake. Kuna wenye vyeti original ambao jinsi wanavyovipata, hali inakuwa haina tofauti na wale wenye vya kufoji.

Ipo haja kwa vyuo vikuu na vyenyewe kujenga mazingira ambayo hakutakuwa na ukaribu kati ya maprofesa na wanafunzi wao, haswa wale wanaosoma wakitokea makazini. Huu ukaribu unachangia katika taifa kuwa na wenye elimu ambao tija yao kama ipo basi ni ndogo sana.

Vyeti feki vilianza kuzaga baada ya internet cafes kuanza kuongezeka nchini, tatizo hili halikuwepo enzi zile za awamu ya kwanza na ya pili. Limekuwa ni tatizo kubwa kuanzia miaka ya Mzee Mkapa. Na kabla ya uwepo wa tatizo hili, nchi ilikuwa na wenye elimu waliozitokea jasho.

Ni vita ambayo ilikuwa kama sio leo basi kesho ianze kupiganwa, lilikuwa ni suala la muda tu. Natumaini mwanzo alioanza nao Profesa Ndalichako, utaendelea katika hali hii kwa miezi mingi ijayo. Jeuri ilizidi mitaani, dharau ilizidi, dhuluma ilizidi, uzembe ulizidi.

Lakini lililo muhimu ni kwa wizara ya elimu kuangalia mianya inayoweza kutengeneza wenye elimu wasio na tija nchini.
tunahitaji vyeti tu,sio porojo. kama kweli ww ni mfanisi kwann hukupeleka vyeti original ie vya kwako kweli ulivyovipigania shuleni? na wengi wenye vyeti feki maneno kibaoooo, utendaji sasa. kumbuka Prof. Ndalichako alikua sabatical leave ya miaka miwili, anajua mengi
 
Mkuu umesema kweli kabisa, ndio maana miaka ya nyuma nchi ilikuwa ikiingia mikataba mingi bila ya wenye elimu wetu kuelewa impact ya muda mrefu ujao ya wao kutia saini kichwakichwa. Elimu inatafutwa kwa juhudi kubwa ni lazima iheshimiwe.
Nchi hi hii au unamaanisha nchi gani?
Nilicheka sana niliposikia mtu mmoja mkubwa na mwenye amri akisema katika elimu vyeo vinatambuliwa kwa watu waliosoma mpaka degree. Aghalabu waliosoma Masters degree wanajifurahisha halikadhalika wale wa PhD wanajiburudisha.
Kiukweli nilitafakali sana nikajiuliza sana kwani kama angenyamaza si angekuwa aneficha aibu yake ya kitaaluma?
Watu inatakiwa wasome wajiendeleze mpaka akili zisaturate ndo innovation & creativity reborn!!
 
tunahitaji vyeti tu,sio porojo. kama kweli ww ni mfanisi kwann hukupeleka vyeti original ie vya kwako kweli ulivyovipigania shuleni? na wengi wenye vyeti feki maneno kibaoooo, utendaji sasa. kumbuka Prof. Ndalichako alikua sabatical leave ya miaka miwili, anajua mengi
Kaka wapo wenye vyeti halisi na halali lakini upatikanaji wake sio halali utawafanyaje hao
 
Nchi hi hii au unamaanisha nchi gani?
Nilicheka sana niliposikia mtu mmoja mkubwa na mwenye amri akisema katika elimu vyeo vinatambuliwa kwa watu waliosoma mpaka degree. Aghalabu waliosoma Masters degree wanajifurahisha halikadhalika wale wa PhD wanajiburudisha.
Kiukweli nilitafakali sana nikajiuliza sana kwani kama angenyamaza si angekuwa aneficha aibu yake ya kitaaluma?
Watu inatakiwa wasome wajiendeleze mpaka akili zisaturate ndo innovation & creativity reborn!!
Tija ni muhimu sana pengine kuliko hata sifa za mtu kuitwa Profesa au Doctor. Kuna kina dada wazuri sana ambao mitihani ikikaribia wanaanza kulegeza macho kwa malecturer wao. Kuna kina kaka wengi tu wenye kujua "kuongea vizuri" na waalimu wao, wote hao kwa ujumla wao wanaingiza kwenye mfumo wa ajira, ile aina ya utendaji kazi usiokuwa na tija. Na ni kwa hasara ya nchi nzima.
 
Unajichanganya mkuu, kwa hiyo unaafiki au unakataa kuhusu vyeti feki?

Ufeki wa cheti na ufaulu ni vitu viwili tofauti. Kama mtu cheti chake kilikuwa cha ufaulu wa Daraja D, akabadili na kujiwekea Daraja B...hiyo ni mojawapo ya aina za vyeti feki. Sasa kama una akili timamu, utapiga vita vyeti feki na mianya yake na sio kushauri kazi wapewe wasio na vyeti kabisa.
 
du mleta hoja anataka waajiriwe wasio na vyeti
No, hujaelewa kabisa hoja yangu. Naongelea umuhimu wa kuwepo kwa umakini kwenye vyuo vyetu vyote. Kutokuwepo kwa seriousness katika upatikanaji wa wenye elimu kubwa ni kwa hasara ya hatima ya Tanzania ya leo na ya kesho.
 
Unajichanganya mkuu, kwa hiyo unaafiki au unakataa kuhusu vyeti feki?

Ufeki wa cheti na ufaulu ni vitu viwili tofauti. Kama mtu cheti chake kilikuwa cha ufaulu wa Daraja D, akabadili na kujiwekea Daraja B...hiyo ni mojawapo ya aina za vyeti feki. Sasa kama una akili timamu, utapiga vita vyeti feki na mianya yake na sio kushauri kazi wapewe wasio na vyeti kabisa.
Hujaelewa hoja yangu. Naongelea umakini vyuoni ili hata hao wanaojulikana kuwa na vyeti halisi basi wawe na tija kwa taifa. Hujawahi kusikia mwanafunzi anafanyiwa mitihani na waalimu wake?. Huzifahamu shahada za underwear?. Yota hayo ni matunda ya kujiendeshea elimu yetu kienyeji bila ya kuzingatia maadili na viwango sahihi vya elimu.
 
Tija itafutwe kwa wenye vyeti halisi full stop. Hakuna namna ya ku justify wenye vyeti fake. No way! Ni kweli wenye vyeti fake (baadhi) wanaweza kuwa na tija lakini isiwe sababu ya kuhalalisha vyeti vyao fake.
 
Back
Top Bottom