Mwenye Uzoefu Wa Kuagiza Simu/ Vifaa Vya Electronics Kutoka Nje Ya Nchi Kwa Bei Ya Jumla

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
279
Salamu ndugu wa Jukwaa.

Nimepata wazo la kufanya biashara ya kununua vitu vya ki electronics ikiwemo SIMU, TV, FLASH, CHAJI, PROTECTOR ZA SIMU kwa bei ya jumla kutoka nchi tofauti (kampuni) yaani nje ya nchi kisha kuutuma mzigo nchini kwa ajili ya kuuza kwa reja reja nchini pia kwa jumla ikiwezekana.

Napenda kufahamu au kuelekezwa yafuatayo kwa wenye uelewa:

1. Namna ya kupata vitu hivo labda kwa njia ya website au vinginevyo.

2. Namna sahii ya mzigo utakavyosafirishwa hadi Nchini na kunifikia.

3. Nitapataje wakala wa kuweza kunisafirishia au kuweza kunifanyia manunuzi kwa nchi au kampuni husika.

4. Changamoto zitokanazo na kuagiza mzigo kuja nchini.

Nitashukuru kama nitafahamishwa yote hayo na kuelewa, mwenye maoni ushauri asisite kunielekeza maana ndo mipango yangu hii mwakani nianze vizuri na nifanikiwe. NITAFURAHI KWA MAONI YENU.

ASANTENI..
 
  • Thanks
Reactions: kyi
Sifahamu zaidi juu ya hili lakini nasikia kuna kampuni maarufu za kimataifa.
Baadhi ni Amazon, Kikuu na Alibaba.
Watafute mtandaoni uwasiliane nao.
Nasikia wanafanya vizuri.
 
Nipo hapa mkuu, nimekuwa nikiagiza moia moja kutoka china bidhaa nyingi sana na kwa bei kama bure.
 
Mwezi ujao nitapokea bidhaa nyingi, zipo kwenye meli zinakuja
 
Hawa ndo wabongo wanakwambia nimekuwa nikiagiza na kiwango cha mzigo walio agiza ila hakwambii changamoto na bei ili uende nunua kwake
 
Back
Top Bottom