Mwenye uzoefu wa hili la kisiasa na uchumi karibu tubadilishane mitazamo

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Nimefanya utafiti karibu nchi nzima ,na utafiti huu una zaidi ya 10,(kumi).

Utafiti huu umefanyika kwenye kaya tajiri,zenye kipato cha kati zenye kipato cha chini na kaya maskini (zenye kubahatisha mlo wa siku).

Swali?
Kwanini kati ya haya madaraja nilotaja ,daraja la tatu kwa maana ya (maskini) familia zao wanaongoza kwa kua na watoto wengi?

Japo kuna pia familia za matajiri na za kati pia baadhi zina watoto wengi pia.

Familia za maskini unakuta anachumba na sebule ,utashangaa ana watoto 7au zaidi na wanafuatana kwa karibukaribu sana, nini tatizo?

Familia za matajiri watoto wachache tena wana interval nzuri na wenye afya.

Nimefanya tafiti hii kama.nilivyosema ,mkoa wa kigoma kwa (ZITTO KABWE) ndio unaoongoza kwa tabia hii. Naomba tubadilishane idea ili kujua kulikoni maskini wanazaa sana kuliko matajiri.

Mimi nilichogundua ni kwamba matajiri wako bize sana na biashara na kazi, maskini hayuko bize akipata mlo kifuatacho ni ng'onyi tu ndio maana wanazaliana kama utitiri.

Mwisho atakae changia uzi huu aweke suluhisho la kulisaidia taifa kuepuka huu mzigo usio wa lazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
thetallest, Moja ya sababu umeitaja hapo.

Mwenye uwezo wa entertainment nyingi ananuchaguzi, kuanzia movies mpaka swimming mpaka kusoma vitabu etc.

Asiye na uchaguzi atafanya burudani za asili, matokeo yake watoto.

Lakini pia elimu inachangia. Kwa sababu hata hiyo burudani ya asiki kuna kufanya kwa uzazi wa mpango.

Hapi utakuta kuna suala la elimu.

Zaidi kuna suala la utamaduni. Kama watu wana utamaduni wa "kila mtoto atakuja na ridhiki yake", ni vigumu kupanga uzazi.
.
Jamii zetu zimetoka kwenye asili ya ukulima na ufugaji kwa kiasi kikubwa.

Katika jamii hizi, watoto ni nguvukazi. Unapokuwa na watoto wengi wanakusaidia kulima na kuchunga mifugo. Hivyo mwenye watoto wengi alikuwa anafaidika.

Ila, sasa maisha yanabadilika kwa kasi kubwa kuliko tunavyoweza kubadili utamaduni huu.

Kikubwa zaidi, kuna watu kama rais Magufuli wanaona hili si tatizo. Wengine wanasema tunahitaji watu zaidi. Magufuli anasema zaeni, nitasomesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
thetallest, Nadhani kwenye hiyo tafiti yako umegundua kuwa hata wenye mentality za umasikini wanapenda sana kuzaana bila mipango. Na muda wote wanawaza ngono tuu, hata wakibahatika kupata nafasi ya kuzungumza wao ni mifano ya ngono tu.

Hivyo mwenyekiti wa chama chako atakuwa na mentality za kimasikini ndio maana pamoja na kukuta taifa lina Sera ya Uzazi wa mpango yeye anapotosha jamii na kuwaambia eti "fyatueni tuu maana sasa hivi hamlipi ada ya shule za msingi"

Hongera kwa utafiti wako, peleka Lumumba labda utawasaidia kubadili mentality ya mwenyekiti wenu kabla hatuja mmwaga asizidi kutupotosha na kutuambuambukiza mawazo ya KIMASIKINI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna sababu mbalimbali zinazofanya familia maskini kuwa na idadi kubwa. Hizi hapa niliwahi kuzifanyia utafiti usio rasmi.

Ukosefu was elimu hasa ya elimu ya uzazi salama.

Imani potofu kwamba kila mtoto anakuja na bahati yake.Hivyo huzaa wakiamini watoto watakuja kuwasaidia maisha yao ya uzeeni.

Wasiwasi wa kupoteza watoto. Maskini wengi huzaa watoto wengi wakihofia wakiwa na watoto wachache wakifariki miongoni mwao watakosa usaidizi uzeeni.

Ndoa za utotoni. Mara nyingi husabisha uzalianaji. Familia nyingi maskini huozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo kukwepa majukumu lakini kuingiza kipato.Mfano anayeolewa ana miaka 15 mpaka kufikia 40 hakosi kuwa na watoto 7-8.

Nguvu kazi. Pia hufanya maskini kuzaana Sana ili kupata vijana watakaosadia kazi hapo nyumbani/kwenye mji.

Ufahari. Wanaume wenye miji maskini wengine huona fahari kuwa na watoto wakiamini huo ndio uanaume.

Dini/Mila. Baadhi ya Mila na dini hukataa suala la upangaji wa uzazi.

Naamini mpaka hapo mkuu utakuwa umepata angalau visababisho vya familia maskini kuwa na idadi kubwa ya watoto.
 
Sababu kubwa ni mbili elimu juu ya uzazi wa mpango na kutokuwa busy zaidi maana wengi wanategemea kilimo na kilimo ni cha musimu.
 
Watu kama nyinyi ndiyo Rais Magufuli huwaita "VILAZA". Kwa hiyo na wewe mtoa mada unaonekana ni KILAZA! Yaani umetumia miaka 10 kufanya utafiti wa jambo ambalo liko wazi kabisa!

Ulishawahi kumuuliza Mwenyekiti wako kwa nini anahamasisha mfyatuane na kwenda kusoma kwenye zile shule za kata? Lengo lake ni kutaka muwepo watu wa aina yako wengi ili iwe rahisi kwenu kutawaliwa milele na pia kubakia kuwa misukule ya Ccm.
 
thetallest,
kuna mawili kwanza masikini wa kiafirika ana mda mwingi wa kuwa idle hivyo mdaa huo anaujazia kwa kujamiana. pili masikini hata uelewa wao wa njia za kuzuwia mimba ni mdogo pia uwezo wa kumudu gharama za zana za kuzuwia mimba ni haupo.

lakini pia kwa sababu ni masikini anakuwa hana uhakika kama watoto watakuwa hivyo anazaa wengi kama bima kwamba wakifa watatu abaki na wawili.
 
Umesema vema. Tatizo kubwa hapo ni mfungamano baina ya kutoelimika na umasikini. Nikisema elimu simaanishi elimu ya darasani, namaanisha yale maarifa anayopata mtu ambayo yatamsaidia kuyakabili mazingira yake.

"Maskini" kwa sehemu kubwa hawajui uhusiano baina ya idadi ya ya watoto/ukubwa wa familia na umasikini wao (viscious circle of poverty/mduara wa umasikini). Wao hudhani watoto ni nguvu kazi (asset) ilhali matajiri wanajua watoto ni liabiliy. Hivyo hata pale ambapo kipato cha familia kinaongezeka, ongezeko hilo humezwa na idadi kubwa ya watoto (chakula, mavazi, maradhi, ada, nk).

Umasikini unavyokubuhu ndivyo maskini anavyozidi kuwa mjinga. Sehemu ya huo ujinga ikiwa ni kudhani kuwa watoto wengi watasaidia kuundoa huo umasikini.

Matajiri wao tayari wameonja uzuri wa maisha ya kuwa na mizigo (liabilities) chache, wakiwamo hao watoto. Hivyo huwa hawataki maisha yao ya kutingwa, starehe, uhuru, nk kuingiliwa na idadi kubwa ya watoto. Kiranga,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani kwa.mchango wako murua
kuna mawili kwanza masikini wa kiafirika ana mda mwingi wa kuwa idle hivyo mdaa huo anaujazia kwa kujamiana. pili masikini hata uelewa wao wa njia za kuzuwia mimba ni mdogo pia uwezo wa kumudu gharama za zana za kuzuwia mimba ni haupo. lakini pia kwa sababu ni masikini anakuwa hana uhakika kama watoto watakuwa hivyo anazaa wengi kama bima kwamba wakifa watatu abaki na wawili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo uzazi wa mpango wenyewe unatakaje, tuzae au tusizae?! Je wao wamepanga tuzae watoto wangapi na kwa interval gani?!

Kuna mtu alitoka China anasema kila familia wameruhusiwa mtoto mmoja, lakini anasema hata hivyo pia bado kuna familia masikini na haziwezi hata kumpa malezi bora huyo mtoto mmoja.

Hivyo ingawa si shauri familia kuwa na watoto wengi, lakini sioni kama hili ni tatizo?! Ni taifa gani kila raia ana degree moja, na ni taifa gani kila raia kaajiriwa?!

Mi nadhani tatizo la umasikini siyo idadi ya watoto, ni uduni wa mawazo na akili bunifu kwa wazazi.

Wote tunakubaliana elimu haileti utajiri?! Hivyo elimu sio chanzo cha umasikini wao.

Kunadhana kwamba zaa wengi hujui nani atakutunza, hizi ndizo fikra mbovu, badala wazazi kujiandalia retirement plan, wanalifanya hili ni jukumu la watoto wao.

Hivyo kuzaa watoto ni kama mchezo wa kubahatisha, unacheza number nyingi kuongoza chances za ushindi.

Lakini pia kumbukeni kuna couples hazikujaaliwa kupata watoto na bado ni masikini.

Hivyo watoto sio chanzo cha umasikini.
 
Back
Top Bottom