Mwenye uzoefu na Kampuni ya Aramex

fokofu

Member
Oct 17, 2012
68
74
Habari zenu wakuu, samahani nilikuwa naomba kufahamu kwa yeyote mwenye uzoefu na kuagiza mizigo kupitia kampuni ya Aramex, nahitaji kujua gharama zao mzigo unapotua Dar es Salaam au na wao wanakodi kubwa kama DHL?
 
kodi kubwa kama DHL
Wanao husika na kodi ni TRA,

Wala sio courier company kama DHL/ARAMEX/FEDEX na kampuni zinginezo.

Tozo la kodi hutokana na invoice value ambayo TRA wameitumia ku_kokotoa hesabu yako ya kodi.

courier company [ Aramex/DHL/Fedex] wao ni kiungo cha kukupa taarifa/documents zako za TRA ili ulipe Tozo la kodi/VAT.
 
Wanao husika na kodi ni TRA,

Wala sio courier company kama DHL/ARAMEX/FEDEX na kampuni zinginezo.

Tozo la kodi hutokana na invoice value ambayo TRA wameitumia ku_kokotoa hesabu yako ya kodi.

courier company [ Aramex/DHL/Fedex] wao ni kiungo cha kukupa taarifa na documents zako za TRA ili ulipe Tozo la kodi/VAT.
Nashukuru mkuu kwa mrejesho, kwa mfano ninaagiza simu ya dollar 50 kutoka USA na shipping cost ya kampuni ya Aramex ni dollar 25 kwa uzoefu wako hapo TRA wanachukua asillimia ngapi?
 
Aramex, nahitaji kujua gharama zao
Aramex ghalama zao ni
  • TZS 35,000 tu iwapo utachukua documents na kwenda kutafuata clearing agent wa kushughulikia mzigo wako.
  • Ni TZS 60,000 Iwapo utawatumia wao ili agents wao ahusike kutoa mzigo wako
Na ghalama zingine zote hulipwa direct kwenye mamlaka husika kama TRA, TBS, Swisport etl

Utapewa hii taarifa kabla ya chochote kufanyika kuhusiana na mzigo wako
1622104214119.png
 
TRA wanachukua asillimia ngapi?
Soma huu uzi utakusaidia kupata makadirio: Kukatwa kodi kwa mizigo

Pata makadilio ya kiasi utakacholipia kwa kutumia huu mfano hapa chini.

A = Bei ya kitu pamoja na ghalama ya kusafirishia.

A X 25%= B ( kiasi utakachotozwa kama IMP )

A + B + (EX + CPF + RDL) = C (itatafutwa asilimia 18 yake)

C X 18% = G ( Ni kiasi cha VAT utakachotozwa ) =

Keywords

- IMP - Import Duty ( 25% ya A )

- EX - Excise Duty ( _% ya A )

- RDL - Railway Development levy ( 1.5% ya A )

- CPF - Customs processing fee ( 0.6% ya A )

- VAT - Value Added Tax ( 18% ya C)

Baadhi ya changamoto zinazojitokeza hapa nchini, soma hizi thread Tatu

#1. Kama ni adhabu ya kutoa mzigo pale airport ni hii, poleni wafanyabiashara

#2. Calculation ya kodi iangaliwe upya

#3. Hili Halijapata Ufumbuzi kuhusu Ununuzi wa Vitu kwa Njia ya Mtandao (Online Purchase) (Angalia posti yangu namba 26)
 
Back
Top Bottom