Mwenye uwezo wa kuwekeza kwenye mawazo yangu yanayohitaji Pesa tu ili yaweze kuwa utajiri na kunisahaulisha machungu ya Elimu yangu iliyouwawa namfumo

Jun 15, 2020
24
90
Mimi ni Kijana wa miaka 26 nikiwa na shahada ya uhandisi wa mitandao na mawasiliano...baada ya kuhangaika sana bila majibu nimeambulia kufahamu fursa nyingi ambazo nimetumia na akili yangu kidogo kuweza kupata mawazo kadhaa ya kibiashara ambazo zenye kuleta matunda chanya kwa muda mfupi sana.

Changamoto kubwa niliyonayo ni pesa ya kuwekeza kwenye mawazo haya kiasi cha kuzidi kukaa na kuilaumu serial yetu na mfumo wake wa elimu ambayo imeishia kunipa cheti kisichokubalika hata kuwekwa kama dhamana ya mm kupata mkopo. Hivyo ukiwa kama mdau wa maendeleo na unauwezo wa kuwaamini vijana kama mm wa kitanzania katika kuwekeza kwenye mawazo yetu naomba tuwasiliane ili niweze kutoa blueprint zoote kuhusiana na Mimi na uhakika wa biashara hizi.

1. Ni Biashara ya Nafaka kutoka mikoani na kuleta Dar es salaam ambako tayari nimeshafanya survey ya masoko na order zake ukusanyaji wake vijijini gharama za usafiri ushuru na kila kitu mpaka faida! Na kugundua kuwa kiasi cha sh. 7M had 10M kinaweza tosha kuanza biashara hii.

2. Kuwekeza moja kwa moja kwenye ujuzi wangu kwa maana muwekezaji kufungua kampuni ya IT solutions and infrastructures akiwa kama CEO namimi pamoja na vijana wenzangu nnaowajua uwezo wao wakufanya kazi tukiwa kama watendaji wakuu kwa maana ya designers na installers tukiwa kama mafundi wa vitu vyoote vya IT kama networking, access control, and security systems installations, programmers kwa maana ya web developers and desingners, Pia tukiwa na baadhi ya mifumo tuliyoiunda wenywe kwa malengo ya kujiuza badae kwenye solo LA Technologia Duniani.

3. Uwekezaji kwenye vyombo vya usafiri kwa maana ya Fuso au tipa za michanga na kokoto au coaster za biashara katika maeneo tofauti niliyoyafanyia research ya kutosha na kuona maslah makubwa na yenye Tija.

NB: Najua kuna watu sana uwezo wa kuweka fixed account zaidi ya Millioni 100 nakusubiri gawio la karibu millioni 10 let's say wakat ndani ya mwaka kama utatumia pesa hiyo kuwekeza kwa vijana kama sisi unaweza tengeneza had 100M nyingne au zaidi. "Sisi ni mavumbi na mavumbini tutarud" ni maneno yanayotukumbusha hizi pesa zoote tutaziacha na watu watauana kwaajili ya hzo hvyo nawaomba wakuu mwenye uwezo tuwasiliane PM ikiwezekana tuonane tuzungumze.

Mimi Niko Dar es salaam eneo LA Mbezi mwisho kwa sasa.

Niwatakie mihangaiko miema.
 
Uko vizuri kujielezea mshikaji wangu. Naona MALENGO yako yameanzia kiasi kikubwa Sana cha hela kitu ambacho kinaweza Fanya usiaminike,na vile umetokea mkoa wa dar ambako unaaminika Kwa utapeli,sijamaanisha we ni tapeli.

Labda Kwa ufupi,unahisi Una kitu chochote ambacho kitamfanya mwenye kukuwezesha aamini hautoingia chaka? Let say,Una nini cha kukudhamini. Nimependa Sana wazo lako la Kwanza Ila ndo Ivo mil 7 kumpa mtu mlokutana JF nayo ni habari nyingine.

Ungeweka mazingira yatakayomfanya mwekezaji akaamini hautokimbia. Dhamana sio lazima wewe ndo iwe nayo,hata kama ni baba na Yuko tayari kuweka nyumba kama dhamana... Nadhan utaaminiwa,lkn hvhv mmmh.
 
Uko vzr kujuelezea mshikaji wangu. Naona MALENGO yako yameanzia kiasi kikubwa Sana cha hela kitu ambacho kinaweza Fanya usiaminike,na vile umetokea mkoa wa dar ambako unaaminika Kwa utapeli,sijamaanisha we ni tapeli. Labda Kwa ufupi,unahisi Una kitu chochote ambacho kitamfanya mwenye kukuwezesha aamini hautoingia chaka? Let say,Una nini cha kukudhamini. Nimependa Sana wazo lako la Kwanza Ila ndo Ivo mil 7 kumpa mtu mlokutana JF nayo ni habari nyingine.
Ungeweka mazingira yatakayomfanya mwekezaji akaamini hautokimbia. Dhamana sio lazima wewe ndo iwe nayo,hata kama ni baba na Yuko tayari kuweka nyumba kama dhamana... Nadhan utaaminiwa,lkn hvhv mmmh

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Asante umenena vyema sana mkuu ila maana yangu kuwa sio MTU aniamini na kunipa million zote hizo wakat hanifahamu ila nnachotaka awe mshiriki pia katika wazo langu huku nikiwa mtendaji...

Hvyo sidhani kama unaweza weka pesa sehemu sasaivi bila kuwepo sehemu husika au MTU wa karibu unaemuamin kukusimamia! Ngependa nipate MTU ambae atshiriki namm hatua kwa hatua mpaka faida inapatikana.
 
Mtoa mada uko sawa kabisa.
Kama kila kitu mtashirikiana hapo hamna harufu ya rushwa ni njia mojawapo ya kuinuana kiuchumi

Hongera kwa wazo zuri
Na Mungu akusimamie
Asante mkuu naimani watu hao wapo sabu sio wote wenye pesa wanaamini kila biashra kwahyo muhimu kuchanganua vzuri MTU akaelewa akathubutu kuweka pesa yake
 
Weka namba yako ya simu...kuna watu wanapita humu bila ya kucomment wakiwa interested watakutafuta.
 
Boss mtarajiwa..
Onyesha kwa hesabu inayoelezeka Ni biashara gani hiyo ya nafaka, kuanzia aina ya zao, Bei ya shamba, kupakia,ushuru,usafiri, usambazaji, na gharama za dharura Kisha tuone faida.
Hela hatutoi Kama simu mfukoni.
 
Nipo tayari kwa hilo wazo la pili.....ninayo kampuni ya IT lakini ik dormant kwa sasa...yaani hakuna watendaji wenye hasira na kazi....niko PM tuzungumze
 
Back
Top Bottom