Mwenye ulemavu wa kuongea amebakwa, namsaidiaje?

maiyanga1

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
988
1,000
Wakuu tukio hili limetokea mwaka jana wakati wa mwezi wa Ramadhani eneo fulani katika mkoa wa Tanga.

Kuna mama wa mtoto mmoja ambaye ni mlemavu wa kuongea ambaye ni maarufu kwa kazi ya ususi ambayo ndiyo inampa maisha yeye na mama yake na mwanae.

Siku hiyo alitoka kumsuka mtu na giza lilikuwa limeshaingia, njiani akakutana na watu wawili wakiwa wamevaa kininja wakambeba na kumwingiza katika nyumba fulani na kumbaka na kumlawiti na pia wakachukua viatu na pesa aliyokuwa nayo.

Baada ya tukio hilo alikwenda kituo cha Afya na kupatiwa matibabu na hakuwa na uwezo wa kumwambia mtu yeyote na hasa ukizingatia changamoto ya kuwaelewa watu wenye ulemavu huo.

Majuzi ndiyo amekutana na mtu wanaefahamina na kwa muda mrefu hawajawahi kuonana na yeye humwelewa kirahisi kidogo, ndipo akamweleza yaliyompata na kwa bahati nzuri nyumba aliyopelekwa (lilipofanyika tukio) anaifahamu.

Katika mazingira haya, lipi linatakiwa lifanyike?
 

Tyrex

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,674
2,000
Ina maana kuandika hawezi? Na matukio hasa yakubaka n.k ninzuri yatolewe taarifa siku iyo iyo ili iwe rahisi uchunguzi kufanyika upesi.
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,725
2,000
Hakuwa na nia ya kulitolea taarifa hilo suala. Mama yake pia hamwelewi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom