Mwenye Ufaham Matumizi ya Petrol Toyota Altezza Toka Tabata Segerea mpaka Posta Kwa siku

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
habarini wana jamii. Nina jamaa yangu ana taka sana kununua Gari Toyota Altezza 6 Cyl engine CC 1,990. Huyu Jamaa anaishi Tabata Segerea anafanya kazi Posta. waswas wake upo kwenye matumizi ya mafuta. kwamba kwa siku atatumia tsh ngapi kwa safari ya kwenda posta na kurudi kwake.

kuna wadau wenye ufaham mzuri wa magari
1. je kuwa na 6 cyl inaweza kuongeza utumiaji wa Petrol ukilinganisha na 4 cyl?
2. kuna uhusiano gani wa CC na matumizi ya mafuta?
3. Kuna ukweli kuwa engine za VVTi zinatumia mafuta pungufu kidogo
4. Kwa safari ya tabata segerea kwenda posta na kurudi Altezza 6cyl CC 1990 inaweza ikatumia lita ngapi kwa siku?

Nawasilisha.
 
Amezungumzia suala hili? La umbal huo? Kama amezungumzia ni vyema ukaweka link
Altezza ni gari ndogo kwa umbo ila kiukweli engine yake ni kubwa na ina power. Iko kundi moja na grand mark II, na hata ulaji wa mafuta haipishani sana na RAV4 kili time.
Kwa route hiyo na kwa foleni, lazima ajiandae Tsh 20,000 kwa safari ya kwenda na kurudi. Lakini ningemshauri aweke mafuta ya Tsh 50,000 kuliko pungufu, hapo unaweza kutumia week nzima siku za kazi.
 
habarini wana jamii. Nina jamaa yangu ana taka sana kununua Gari Toyota Altezza 6 Cyl engine CC 1,990. Huyu Jamaa anaishi Tabata Segerea anafanya kazi Posta. waswas wake upo kwenye matumizi ya mafuta. kwamba kwa siku atatumia tsh ngapi kwa safari ya kwenda posta na kurudi kwake.

kuna wadau wenye ufaham mzuri wa magari
1. je kuwa na 6 cyl inaweza kuongeza utumiaji wa Petrol ukilinganisha na 4 cyl?
2. kuna uhusiano gani wa CC na matumizi ya mafuta?
3. Kuna ukweli kuwa engine za VVTi zinatumia mafuta pungufu kidogo
4. Kwa safari ya tabata segerea kwenda posta na kurudi Altezza 6cyl CC 1990 inaweza ikatumia lita ngapi kwa siku?

Nawasilisha.
Kama hela ya mafuta ina mpa pressure si achukue gari ya engine ndogo kama Vits au Suzuki swift?,
 
Kwa ufahamu wangu cc inavokua kubwa na ndio fuel consumption ya engine ya gari yako inavokua kubwa, tusiende deep sana. Issue za VVTi, Beams 2000, etc tumuachie mshana jr

Turudi kwenye topic, Altezza kwa hiyo route uliyopitia umbali sio tatizo tena, tatizo hapo ni foreni. Asikuambie mtu gari kwenye foreni zinapoteza sana mafuta kuliko zikiwa speed ya 60kph to 100kph.

Tegemea kwenda tu lita 4 (8000Tsh) na kurudi hivo hivo. So jumla kama 16000 hivi. Hapo hujapiga misele yoyote extra.

So tuta conclude kama mkuu alivosema hapo juu, wese la 20,000 per day linahusika.

Kama wese la mawazo, itabidi uwe kila siku wa kwanza kufika kazini, by 5am uwe umeshatoka kwenu na wa mwisho kurudi nyumbani by 9pm ndio uwe unatoka kazini. Utapunguza sana hiyo gharama karibia nusu yake.
 
Ukifaham dhan ya kuomba ushauri utajua nini unapaswa umsaidie mtu kama huyu. Mtu anapoomba ushaur maana yake anataka apime. Na aaamue

Kama hela ya mafuta ina mpa pressure si achukue gari ya engine ndogo kama Vits au Suzuki swift?,
 
Hapo akiweka mafuta full tank jumapili inamfikisha kabisa wiki nzima na kubaki kuwa na foleni au isiwepo inapiga mzigo fresh tuu
 
sasa wasiwasi wa mafuta wa nini si anunue piki piki sasa

UKIONA MTU ANALALAMIKA GARI INAKUNYWA MAFUTA UJUE WAKATI WAKE WA KUMILIKI GARI BADO

atafutw vitz tu sasa
Hakuna MTU anaemiliki gari,Bali gari ndio linakumiliki wewe.
 
10,000 kwa siku si mbaya kama inaenda na kurudi na unatumia AC ni ya kawaida tu. na hapo haujazima zima barabarani maana si ule uendeshaji wa gari wa kimaskini kwenye folen unazima. inatakiwa gari ukiwasha nyumba na AC utazimia Ofisini. 10,000 si gharama.

Elfu kumi kwa siku mzeee..... Au elfu 70 kwa wiki nishamiliki 6 cylinder altezza nakaa Tabata
 
sasa wasiwasi wa mafuta wa nini si anunue piki piki sasa

UKIONA MTU ANALALAMIKA GARI INAKUNYWA MAFUTA UJUE WAKATI WAKE WA KUMILIKI GARI BADO

atafutw vitz tu sasa
Nimechekaaa sanaaa yaniii kwa hiyo ameruka stage
 
Back
Top Bottom