Mwenye uelewa wa neno 'frequency' naomba atujuze kwa kina

Habarini wajuzi mbali mbali mliopo hapa, kwani inasemekana frequency au series za namba fulani au hyper hidden knowledge ambayo ina uhusiano na nguvu za ndani za kimwili huweza kutengeneza uwezo usio wa kawaida.

Mfano katika kitabu cha anakh, viumbe jamii ya majini wanadai wao wana high frequency ya kuweza kutuona binadamu kwa vizuri sana mpaka hata viungo vya ndani lakini wanadai sisi humanoid kwa sababu tuna low frequency ni ngumu sana kuwaona wao unless utumike ujuzi wa kutafuta namba maalumu ziwe attached na mwanadamu ndio uweze kuwaona wao.

Naomba mwenye ujuzi huu anijuze The power of frequency

Kama nimekuelewa vyema ni kwamba unataka kujua nguvu ya "frequency" katika uono "vision" ya mwanadamu wa kawaida pamoja na "enhanced power of vision beyond".

Kweli hii ni elimu ya Mesmerism, elimu hii ndio inayotumiwa na wachawi (magicians) katika mazingaombwe nk, kama jinsi wadau walivyosema; ni kwamba macho ya binadamu yanaweza kuona nuru iliyomo katika uwanda unaoonekana "visible spectrum", ni frequencies band ambamo macho yetu yanaweza kuona hizo nuru juu au chini (infra, ultra) ya hapo hatuwezi kuona, sasa elimu inayotumika ni kuyapa nguvu au kuyapoteza macho ili yasiweze kuona ndani ya visible spectrum au yasiweze kuona uhalisia wa vitu kwa maana hiyo ni frequencies za uoni ndizo hupotezwa au kudanganywa kwa kutumia uwezo waliojifunza, lakini haiwezekani kwa binadamu katika hali yoyote kuona kupitia kitu Opaque isipokuwa iwe ni kioo.
 
Wakati tsunami ile ya kule mashariki ya mbali ilipotokea, wanyama wote kama mbwa na paka walikimbilia sehemu zenye miinuko, dakika 30 kabla ya wimbi la kwanza kuja. Wao waliweza kusikia frequency za hilo wimbi ila binadamu hawakuweza.

Viumbe hai mbalimbali wanauwezo tofauti wa kutambua frequencies mbalimbali. Mfano binadamu wanauwezo wa kusikia sauti kati ya frequency ya 20Hz na 20KHz, nje ya hapo binadamu hawezi kusikia. Mbwa kwa upande mwingine anaweza kusikia sauti zaidi ya 20kH.

Hata inapokuja kwenye kuona kuna frequencies chache sana ambazo binadanu wanauwezo wa kuona (visible light) nje ya hapo hatuoni. Mfano kwenye giza totoro, binadamu anakuwa kipofu ila kuna baadhi ya wanyama , kama nyoka, wanaweza kuona vizuri tuu usiku. Hii ni kwasababu wanauwezo wa kutambua lower frequencies kama infra red.

Kuhusu hivyo viumbe vinavyoweza kutuona, kama kweli, vipo basi vitakuwa vinaweza kutambua ranges nyingi za frequencies kuliko sisi.
Dooh!
 
Usipende kusema haiwezekani..
Upo uwezekano wa kuona nyuma ya ukuta, mlima, au hata nyuma ya kisogo
Inatakiwa uvumbuzi mpya labda but every is possible.
mfano Dr grobovoi wa Russia you can Google her, yeye akihusisha frequencies na numerical number akisema zinauhusiano mkubwa sana kwa kutumia computer yake maalum aliweza kugenerate series of numbers ambazo kuputia visiolizalion zinauwezo beyond ya kile tunachokitafakari,msomeni huyo ndugu.
 
Usipende kusema haiwezekani..
Upo uwezekano wa kuona nyuma ya ukuta, mlima, au hata nyuma ya kisogo

Mimi sijasema haiwezekani kuona nyuma ya mlima au ukuta na kichogo, nasema haiwezekani mtu kuona kupitia ukuta with naked eyes, mfano mtu aangalie nje ya pipa (steel drum) na aseme kitu kilichomo humo bila kufungua mfuniko.
 
Inatakiwa uvumbuzi mpya labda but every is possible.
mfano Dr grobovoi wa Russia you can Google her, yeye akihusisha frequencies na numerical number akisema zinauhusiano mkubwa sana kwa kutumia computer yake maalum aliweza kugenerate series of numbers ambazo kuputia visiolizalion zinauwezo beyond ya kile tunachokitafakari,msomeni huyo ndugu.

Uvumbuzi mpya kwa kutumia nyenzo, mfano Ultrasound kuangalia mimba, tuzungumzie "frequency" katika natural situation, hapa duniani kuna rangi nyingi sana lakini zinazoweza kuonwa na binadamu ni zile zilizomo ndani ya visible frequencies tu.
 
mfano Dr grobovoi wa Russia you can Google her, yeye akihusisha frequencies na numerical number akisema zinauhusiano mkubwa sana kwa kutumia computer yake maalum aliweza kugenerate series of numbers ambazo kuputia visiolizalion zinauwezo beyond ya kile tunachokitafakari,msomeni huyo ndugu.
Ungeweka link hapa mkuu
 
... not necessarily kwa sekunde but any unit of time even if second is the SI unit. In some contexts seconds will make sense but in others won't make much sense; rather, hours, years, even centuries are more suitable.
Dah...kwa kifupi frequency ni marudio ya tukio fulani kwa kipindi pendwa ...🤣🤣🤣🤭
 
frequency ni kipimo au jina maalumu kwa ajili ya kujua uwezo wa mawimbi kwa vipimo cha heartz(HZ).

frequency inaweza kuwa mawimbi sumaku,mawimbi ya bahari,mawimbi ya tetemeko,mawimbi joto na n.k

kuitwa jina la frequency ni kipimo kilicho kubaliwa na idara ya sayansi kama unaona vipimo kama mfano force,gravity,ohm,acceleration na n.k

View attachment 1953346

unataka kujua zaadi
.... frequency, literally, sio lazima mawimbi mzee! Chochote knachofanyika repeatedly kinaweza kupimwa kwa frequency. Frequency yako ya kwenda chooni ni ipi? Daily? Hourly?
 
.... frequency, literally, sio lazima mawimbi mzee! Chochote knachofanyika repeatedly kinaweza kupimwa kwa frequency. Frequency yako ya kwenda chooni ni ipi? Daily? Hourly?
Dah....labda mawimbi ana maana ya kwenda na kurudi 🤣🤣🤣🤭
 
Samahani mkuu

Naomba urudie apo kwenye tyre ya baiskel mfano wake
Chukulia zile reflectors zinazowekwa kwenye grurdumu la baiskeli, ikiwa chini halafu ikazunguka kwenda juu na kurudi chini kwa muda fulani hiyo ni frequency.
... not necessarily kwa sekunde but any unit of time even if second is the SI unit. In some contexts seconds will make sense but in others won't make much sense; rather, hours, years, even centuries are more suitable.
Ni kweli, ila hertz ipo kwa sekunde.
 
Ndio pia binadamu nasikia tunaweza ku control our brain frequencies at some point??
Psychedelics kama ayahuasca zinaongeza utambuzi kwa kuongeza range za brain frequencies. Unakuwa na uwezo wa kuona hata ndugu zako waliotangulia mbele za haki kabla ya wewe kuzalia. Watu wanaweza kusikia sauti na kuona rangi kwa ufasaha zaidi wakati wana "trip".
 
Samahani mkuu

Naomba urudie apo kwenye tyre ya baiskel mfano wake
Sine_curve_drawing_animation.gif
 
Back
Top Bottom