Mwenye uelewa na neno hili

Naombeni mnisaidi Utofauti wa neno....
"Expiry date" na "Best before"
Expire date maana yake ikifika hiyo tarehe hio bidhaa haifai kabisa kwa matumizi ya binadamu, ni ya kutupa.

Ila Bst before maana yake bidhaa inaweza kutumika baada ya tarehe kupita ila haitakuwa na ubora wake hasa kama ilivyokuwa kabla ya tarehe.

Ila kwa kibongo bongo best before na expire date ni sawa tu maana uchakachuaji mwingi sana kwa sababu za kibiashara.
 
Ipo hivi mkuu..!

Naomba nikujibu kwa kutumia mfano wa Chakula kilicho fungwa kwenye package.
Expire date ni tarehe ya mwisho ambayo hicho chakula kitakuwa ni salama kwa kukitumia.
Best-Before date ni tarehe ambayo ubora wa hicho chakula utaanza kupungua ( na sio usalama wa chakula )

Kwa maana hiyo basi chakula ambacho utakitumia after Expire date sio salama,
na kile ambacho utakitumia after Best-Before date, hicho kimepungua ubora (ingawa kinaweza kikawa ni salama kwa kula )
 
Naombeni mnisaidi Utofauti wa neno....
"Expiry date" na "Best before"
Expiry date - tarehe ya mwisho wa matumizi baada ya hapo ubora wake unakuwa umeisha
Best before - tumia kabla/inafaa kabla ya/ ni bora zaid kabla ya..........tarehe husika iliyo andikwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom