Mwenye uelewa kuhusu sheria za Vita vya Silaha za Moto

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
2,280
3,055
Kama kawaida JF ndo kisima changu pekee cha kuchota maarifa elimu na Mambo mengine mengi mno ya msingi, hivyo mniwie radhi kwa swali langu lingine hili.leo nataka kujua sheria za Vita zikoje maana Kuna mahali nilisoma sikumbuki Ni wapi mdau alikuwa anasema kwamba Vita havipiganwi kiholela Kuna sheria zake maalum.

Hivyo naomba kujua maana ya uwanja wa Vita na ukoje?

Ni vipi Vita ikipiganwa kwenye nchi husika raia wake huwa wanajikingaje wanajulikanaje kuwa huyu Ni raia wa kawaida na huyu ni adui?

Waandishi wa habari na wale wafanyakazi wa msalaba mwekundu kuingia uwanja wa Vita wakaendelea na shughuli zao Ni kwa vipi wanatambulika?

Naomba kujua na mambo mengine mengi kuhusu Vita.

Kuuliza sio ujinga

Shukran
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom