Mwenye uelewa atujuze kuhusu matumizi ya ving'amuzi au tochi za barabarani

kuna umuhimu wa kuzireprogram hizo tochi ili ziendane na teknolojia iliyopo vinginevyo hata polisi kuzitumia kama kielelezo cha ushaidi mahakamani inakuwa kazi kwelikweli wanapokutana na maIT guru
 
Baadhi ya nchi za wenzetu wanakuwa na vibao kwenye barabara kuu kuashiria kuwa kuna tochi mbele.
View attachment 878086 View attachment 878088 View attachment 878089

View attachment 878091

Mkuu wenzetu huko kulikoendelea lengo lao kuu ni kuzuia ajali au kupunguza ajali barabarani wakati sie lengo letu ni kutoza faini kwa madereva wakosefu as much as we can, na ndio maana kila mwezi utasikia statistics za Billion kadhaa za kufurahisha na sio statistics za ajali zilizotokea na wala hawatoi remedial action yoyote ili kupunguza ajali hizo na ndipo utakapoelewa kwanini hawataki waonekane na tochi zao au kwanini wanakuwa wakali sana pale unapotaka evidence ya picha uliyozidisha speed, kibaya zaidi unapokamatwa kwa speed jua kuwa huna mtetezi popote pale utakapoenda labda ahera na waliojaribu kusaidia yameshawakuta
 
Tatizo Madereva wakiziona tochi wanaanza kuambiana walipo Matraffic na baada ya hapo ni kukanyaga mafuta na mwendo kasi
Miaka ya mpaka 2010 ajali zilikuwa zinafikia 5,000 kwa mwaka bado vifo nk kna Mohamedi Mpinga na Waziri Masauni waliunda Tume kutafiti ni nini chanzo na watakimalizaje kuwaokoa Watanzania. sasa wameweza.
Mohamedi Mpinga atahojiwa na ITV ni vizuri akaulizwa hayo maswali,
wenye Mabasi (kina Mruma) walikubali sasa ajali zimepungua, matairi ya mabasi yanadumu kwa muda sasa na ajali hakuna tena
Bugududu Sududu labda nikueleweshe kuwa kwa sasa Mabasi ya masafa marefu /mikoani sasa yamefungiwa vidhibiti mwendo speed inayotakiwa ni 85km/h ukizidisha 86km/h GPS inasoma na mawasiliano yapo SUMATRA na hata kwa tajiri wa basi lako
na ukiwa na simu ndani ya Basi lako tumia /Download Makin App utapata mwendo wa Basi ulilomo
sema uchungu unakuja kwa magari binafsi na madogo tena km ndio lina No za zamani km A_Z au BZZ Tochi zitakutesa sana, na faini kulipa sio hapo hapo utaanikiwa na ulipe kwa mtandao wa simu ndani ya siku 7
Kuna tetesi vibao vya 50 vitapunguza humo barabarani siku za karibuni
 
Kwa ujumla tochi imesaidia kwa kiasi kupunguza ajali za mabasi ya abiria, kero yangu ni huo upuuzi wa matrafic wenye tochi kujificha na pia kitendo cha kuyaachia magari yenye plate numbers stl, sth, na dfpa yaende mwendo wautakao.
Wala sio tochi zilizopunguza ajali za mabasi bali ni speed governor
 
Hata mniambie nini lakini kwa hili niko upande wa polisi. Hii ni kwa sababu nidhamu ya madereva Bongo ni mbovu kupindukia. Sasa hata kama trafiki atajificha vichakani wewe una wasi wasi gani kama mwendo wako ni sahihi? Madereva naweza kuwatetea kwenye area moja tu. ie barabara zetu siyo user friendly na sehemu nyingine za barabara kuu wameweka speed limit ndogo kuliko ilivyotakiwa.
Mkuu we watetee ila jua kuwa hao wazee wa fedhwa sio marafiki kabisaaa, kama ni dereva siku moja utakuja kufaham juu ya jambo hili.
 
Tatizo Madereva wakiziona tochi wanaanza kuambiana walipo Matraffic na baada ya hapo ni kukanyaga mafuta na mwendo kasi
Miaka ya mpaka 2010 ajali zilikuwa zinafikia 5,000 kwa mwaka bado vifo nk kna Mohamedi Mpinga na Waziri Masauni waliunda Tume kutafiti ni nini chanzo na watakimalizaje kuwaokoa Watanzania. sasa wameweza.
Mohamedi Mpinga atahojiwa na ITV ni vizuri akaulizwa hayo maswali,
wenye Mabasi (kina Mruma) walikubali sasa ajali zimepungua, matairi ya mabasi yanadumu kwa muda sasa na ajali hakuna tena
Bugududu Sududu labda nikueleweshe kuwa kwa sasa Mabasi ya masafa marefu /mikoani sasa yamefungiwa vidhibiti mwendo speed inayotakiwa ni 85km/h ukizidisha 86km/h GPS inasoma na mawasiliano yapo SUMATRA na hata kwa tajiri wa basi lako
na ukiwa na simu ndani ya Basi lako tumia /Download Makin App utapata mwendo wa Basi ulilomo
sema uchungu unakuja kwa magari binafsi na madogo tena km ndio lina No za zamani km A_Z au BZZ Tochi zitakutesa sana, na faini kulipa sio hapo hapo utaanikiwa na ulipe kwa mtandao wa simu ndani ya siku 7
Kuna tetesi vibao vya 50 vitapunguza humo barabarani siku za karibuni
Nimekuelewa kiongozi ila mimi ninacho hoji kwanini askari wenye tochi wajifiche? Kitu ambacho sio sahihi,wakati tumeonyeshwa na mwenzetu baadhi ya nchi kuna vibao vinavyoonyesha mahali penye kamera, hivyo si sahihi wao kujificha
 
Moja ya masharti na matumizi ya hizo tochi ni askari kujificha pale anapokuwa anamuulika gari iliyoikusudia? Maana isije na madereva nao wakaanza kuangalia pembezoni mwa barabara! Tukawa tumeongeza zaidi tatizo la ajali za barabarani badala ya kupunguza

Kumbuka lile ni zoezi la kurekebisha tabia za madereva wasiotii sheria za barabarani, siyo sawa na lile zoezi la kupaka rangi kuta na kuzibua mitaro wakati wa ziara za viongozi wa juu
 
Mkuu we watetee ila jua kuwa hao wazee wa fedhwa sio marafiki kabisaaa, kama ni dereva siku moja utakuja kufaham juu ya jambo hili.
Nawajua sana. Niseme nimeshakumbuna nao na fedha zimenitoka. Ila kwa Bongo hutaniambia chochote kuhusu uendeshaji. Nchi dereva akiona kivuko cha waenda kwa miguu na watu wanasubiri kuvuka ndiyo anaongeza mwendo? Bado hujakutana na overtake na speed kali zisizo na ulazima hata kidogo! Too much.
 
Kwa Tanzania hizo tochi ni sehemu ya viwanda, kinatumika kuzalisha pesa nyingi sana,
ni chanzo cha mapato ya hii nchi.
 
Kwa ujumla tochi imesaidia kwa kiasi kupunguza ajali za mabasi ya abiria, kero yangu ni huo upuuzi wa matrafic wenye tochi kujificha na pia kitendo cha kuyaachia magari yenye plate numbers stl, sth, na dfpa yaende mwendo wautakao.
Hapo tochi inapochuja plate number zenye STL ndiyo matokeo yake tunaona mawaziri wanavunja mabega kwenye ziara zao alafu wanakua rescued na helicopter.
 
Hapo tochi inapochuja plate number zenye STL ndiyo matokeo yake tunaona mawaziri wanavunja mabega kwenye ziara zao alafu wanakua rescued na helicopter.
Unajua double atandard inawacost wakubwa na hata wasio na hatia, speed warnings sio ya raia wa kawaida tu, na kitendo cha kuwaachia sio kuwa watahatarisha maisha yao tu ni hata ya madereva na raia wengine, siku zote hii kitu huwa inaniumiza sana kichwa.
 
Nimekuelewa kiongozi ila mimi ninacho hoji kwanini askari wenye tochi wajifiche? Kitu ambacho sio sahihi,wakati tumeonyeshwa na mwenzetu baadhi ya nchi kuna vibao vinavyoonyesha mahali penye kamera, hivyo si sahihi wao kujificha
nimekuelewa Mkuu na tupo pamoja
tatizo la askari kujificha na tochi hata mm silikubali
na hawana huruma na wanakutegea ukiwa muoga utalambwa 30 ila sasa zinatumwa baada ya siku 7 na wao hawaambulii chochote
Ile ilikuwa kurekebisha mwendo uletao ajali na yale magari mapya , zenye namba za misaada (DFP) au za Escort 1- 4 hao wenzetu wanawahi mpaka mtu unatamani usafiri na mabasi tu ya 80km/h siku 2 Dar Mwanza
 
Habarini wanajukwaa
Moja ya masharti na matumizi ya hizo tochi ni askari kujificha pale anapokuwa anamuulika gari iliyoikusudia? Maana isije na madereva nao wakaanza kuangalia pembezoni mwa barabara! Tukawa tumeongeza zaidi tatizo la ajali za barabarani badala ya kupunguza!!
mm sina hamu nao, nina faini niliipata Jiji la mbali mpaka leo inasoma
yaani deni linazaana tu tangu Novemba 2017
na wewe ukitaka kujua km upo salama hudaiwi na Traffic
ingia www.tsm.tpf.go.tz
 
Wakati wenzetu lengo ni kupunguza ajali barabarani bongo lengo la hizo tochi ni kuongeza mapato ya polisi na kunenepesha mifuko yao, imekuwa kama vita sasa.
 
Kuna wakati ili trafiki asijulikane anampa kamera mtu aliyevaa kiraia. Mda mwingine wanabambikia kosa. Unapigwa tochi hata kibao hamna. Kama kungekua na application ya kuzuia tochi ningeinunua kwa gharama yoyote.
 
Back
Top Bottom