Mwenye ubavu anishtaki! - Yona

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,346
38,995
Habari zinazoingia mida hii zinasema kuwa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini na mbia mkubwa wa Mgodi wa Kiwira Bw. Daniel Yona amejitokeza na hatimaye kuzungumzia madai kuwa yeye pamoja na Rais wake walijigawia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira kwa njia za kinyemela.

Imeripotiwa katika mojawapo ya magazeti kuwa Bw. Yona anadai kuwa haki iko upande wake na hajatisikika.

Bw. Yona anasema kuwa aliposikia kuwa kuna mbunge toka Kilimanjaro ameleta hoja ya Kiwira alidhania ni Bw. Ndesamburo wa Chadema. Lakini alipogundua kuwa ni Kimaro wa Vunjo (CCM) Bw. Yona alibakia kusema "Haya bwana".
 
Mzuzu

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
517
442

Tena amesema kwamba anayejisikia aende mahakamani na ajutii wala kusiskitika na yupo tayari kusimama wakapambane huko kwenye sheria!!!
 
NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Time will tell hawa jamaaa wamenunua mgodi kwa bei chee tena wanalipwa capacity charge wanatakiwa wanyang'anywe mali ya watanzania halafu waende jela
 
WembeMkali

JF-Expert Member
Jun 16, 2007
282
3
Yona bado anafikiri ni Tanzania ile ile waliyoichunaa wee na BWM...kama Lowasa alisalimu amri atakuwa Yona?
 
Zanaki

JF-Expert Member
Sep 1, 2006
545
74
Yona bado anafikiri ni Tanzania ile ile waliyoichunaa wee na BWM...kama Lowasa alisalimu amri atakuwa Yona?

Quite right,wote hawa huanza na kauli za kibabe na kijeuri.Mimi nadhani yote ni danganya toto.Ukweli ni kwamba lazima mtu utaingiwa na uoga.Na kuna mambo mengi ya kuwafanya waogope.Kwa mfano,wao wana familia,lazima watakuwa concerned about their safety.Maana hapa ni dhahiri wao wamechangia sana kwa maisha ya Mtanzania kuwa magumu zaidi,kama ndio Tanesco inawalipa pesa zote hizo,hizo pesa Tanesco si inatoa kwa wananchi...Tulishasikia watoto wa Lowassa wakizomewa hadharani,sasa hizi kauli zao za kijeuri kwa kweli ni upumbavu tu!
Unamwibia mtu then unamwambia nenda mahakamani kama una kifua.....si uchizi huo!
 
Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,848
56
Habari zinazoingia mida hii zinasema kuwa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini na mbia mkubwa wa Mgodi wa Kiwira Bw. Daniel Yona amejitokeza na hatimaye kuzungumzia madai kuwa yeye pamoja na Rais wake walijigawia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira kwa njia za kinyemela.

Imeripotiwa katika mojawapo ya magazeti kuwa Bw. Yona anadai kuwa haki iko upande wake na hajatisikika.

Bw. Yona anasema kuwa aliposikia kuwa kuna mbunge toka Kilimanjaro ameleta hoja ya Kiwira alidhania ni Bw. Ndesamburo wa Chadema. Lakini alipogundua kuwa ni Kimaro wa Vunjo (CCM) Bw. Yona alibakia kusema "Haya bwana".

Anajua kilicho mbele yake na Chenge kwake ni kama case study. Hii kauli ni ya kujitutumua tu, anajua fika 40 zake zimefika.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
938
Siku za mwizi ni arobaini, watu wazima hawatishiani nyau..... sasa huyu yona asubiri na kuanza kuweka maji tu maana wembe ule ule uliomnyoa Chenge, unakuja mpaka mafisadi wote wasafishwe, na kutinga kwenye mikono ya sheria pole pole tunawafikia!

Haya maneno yake ukiyasoma vizuri between the lines, ni maneno ya mfa maji, sasa anategemea ubavu Mkapa ndio utamuokoa, mimi nilisema kwamba wabunge wa CCM, baada ya Richimnduli waliamua kuwa Kiwira, na mkataba wa bandari kuwa their next stop, here they come!

Na ninaomba kuwakumbusha wabunge kina Kimaro kuwa hapo tupo kwenye ukurasa mmoja hapa, mpaka kieleweke! Na wakati umefika kwa serikali yetu kuanzisha uchunguzi wa kina kwa Mkapa peke yake, na Mkewe peke yake maana nasikia huyu mama naye ametutia sana hasara taifa, hasa baada ya ule moto wa Ikulu!
 
Obe

JF-Expert Member
Dec 31, 2007
9,734
33,495
Wote waliotuhumiwa na ufisadi wanapofuatwa na waandishi, wanakuwa na lugha kama za huyu fisadi. Muda utatuambia nini kinaendelea
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,123
Unajua mtu akishazoea kuiba na wala hafuatiliwi ndo taabu yake.
Alafu nae anashindwa soma alama za nyakati ni kheri akae kimya kama Mramba sio kubwatukabwatuka....nonesense yaani ametuliza lafu anatupiga bit?
Hii ni zarau kwa watz!
Huo mgodi wapokonywe as am told thamani yake ilikuwa bil 4 na ukauzwa mill 700 na hawa jamaa wamelipa 10% tuu ambayo ni 70mil jamani si masihara haya kwa watz?
Biashara za wapi izi ata enzi za utumwa haikuwa ivyo
 
Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,216
3,638
Tena amesema kwamba anayejisikia aende mahakamani na ajutii wala kusiskitika na yupo tayari kusimama wakapambane huko kwenye sheria!!!

Mzuzu,
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe amesema 'mwenye ubavu aende mahakamani' siyo anayejisikia. angalia quatation hii

``Kama yupo mwenye ubavu na nia ya kwenda mahakamani sawa ni haki yake, sitishiki kwa vile pia nina haki zangu. Tutakutana huko,`` alisema.

HIKI NI KIBURI CHA KUTISHA
habari kamili ipo hapa http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/04/24/113047.html
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
1,156
Yona ananikumbusha kauli ya Mwema... Nchi imeshikwa na magaidi, no, I mean mafisadi
 
Single D

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
457
13
Kweli inatia uchungu na kusikitisha kiongozi kama Daniel anapoleta dhihaka,mizaha na kebehi kwa Taifa hili.

Gharama za Umeme wa TZ zimefanya watu kuwa maskini, Daniel analeta dhihaka tena kwa wananchi?poor Daniel!

Hivi Daniel anajiamini nini?Unaona mwenzio Chinga kakaa kimya maana haya mafuta yameshachemka zaidi ya digrii 200 centigrade anasubiriwa fisadi kukaangwa humo.

A young man who is poor and wise is better than a king who is old and foolish and will not be guided by the wisdom of others.

Itafika wakati watasema yote na hata jinsi hisa hizo walivyopeana
 
IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
138
Yona pole sana kakyangu,ila ujue umefuta historia njema ya wanao, siku zote kizazi chako kitadharaulika na hata kutengwa, fanya maarifa uturudishie hayo mapesa yetu, siku zote watanzania ni wapole ila siku wakicharuka, sijui itakuaje.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,231
fisadi akitajwa hadharani mwanzo kuwa ana panick, hajui anasema nini.
baada ya siku mbili tatu huyu atanywea kama chenge, tusubiri tuyaone, yapo njiani
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
Wote waliotuhumiwa na ufisadi wanapofuatwa na waandishi, wanakuwa na lugha kama za huyu fisadi. Muda utatuambia nini kinaendelea

Ubaya mmoja wa ufisadi ukishagundulika hauishii kwa yule tu aliyeufanya; unawatafuna mke/mume,watoto,wajukuu, ndugu na hata marafiki wa karibu na fisadi mwenyewe! Kazi mnayo mafisadi wa nchi hii.Ni jana tu mlikuwa mkionekana mashujaa tunawapisha na kwenye viti; leo.....
 
Kindingo

Member
Jul 31, 2007
14
0
Yap! Time will tell - Watanzania tusilegeze kamba vita ya kujikomboa toka makucha ya mafisadi iendelezwe kwa nguvu zaidi na waelewe siku zao zimefika!!!
 
Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,220
50
basi hivi alivotishia ndo alimtishia hivi hivi na Pinda ndio maana akuaja kutuambia kuwa serikali haiwawezi mafisadi
 
Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,848
56
basi hivi alivotishia ndo alimtishia hivi hivi na Pinda ndio maana akuaja kutuambia kuwa serikali haiwawezi mafisadi

kwi kwi kwi, pinda kweli kapinda yaani katishiwa nyau na dany nae kafyata mkia. Hapo kweli kiongozi hatuna.
 
Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,220
50
Jamani mbona MKAPA haongei kitu??? waandishi wa habari mnamsuburi huyu jamaa mpaka awaite???? nendeni wenywe mkamuombe mahojiano nae, msumbueni mpaka atamke neno jama, na naahidi siku atakayo fungua mdomo ataongea madudu kama haya "ooo ni magazeti ya udaku tuu, am going to grant their wish am resigning".... "ni vijisenti tu na sitajiuzulu"
 
Hajasoma bado alama za nyakati, watanzania tulivyo na hasira nae asubiri mascud tu hata kama JK akimsitiri.

Ushauri wa bure kwa Mkapa: Acha kiburi, rudisha mali zetu zote ulizotuibia. Pia unaweza toa msaada katika moja ya gereza at least wajenge vyoo na wanunue magodoro na tv at least ukienda huko usitumie ndoo kujisaidia au kulala chini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom