Albert Wilson Albert
Member
- Aug 22, 2018
- 44
- 50
Nyumba za kupanga,
Imetokea Katika nyumba moja hivi hapa Dar es Salaam, Choo kimejaa halafu Mwenye nyumba kachangisha pesa ili gari ya maji taka ije Kunyonya lakini tamaa ikamuingia mwenye nyumba akala ile pesa yote. Hali hii imetokea mara tatu pesa zinaliwa.
Siku zikaendelea, choo kinazidi kujaa na hali ni mbaya, wapangaji hawana la kufanya.
Mwisho wa siku mpangaji mmoja amegoma kutoa pesa kwa ajili ya suala hilo kwani pesa ishaliwa mara tatu ikabidi amwambie mwenye nyumba kuwa ukitaka pesa yangu kwa suala hilo tafuta pesa mwenyewe itagari ya majitaka ije isqfishe baada ya hapo nitatoa pesa.
Mwenye nyumba anaona kuwa mpangaji wake amekuwa mkaidi, anaamua kuwaita wapangaji wengine anawashawishi watoe pesa kisha Mke wa yule aliyekataa kutoa pesa kwa mara ya nne anapiga simu kwa mmewe ili pesa itolewe, Mwanaume anakataa na kutoa lake la moyoni akisema kwamba endapo gari itakuja nitatoa pesa kinyume na hapo ni ubabaishaji.
Mwenye nyumba ni Mjumbe wa nyumba kumi hapo mtaani, sasa nini kifanyike ili huyo mwenye nyumba afanye usafi wa Choo?
Ukisema uende serikali za mtaa, yeye pia ni mwakilishi mtaani hapo. Wapangaji wana watoto wadogo ambao wanaweza kuathirika kiafya.
Wapangaji washitaki wapi ili kuondoa usumbufu huo?
Karibuni