Mwenye mawasiliano ya Wizara ya Maji anisaidie, nimepata changamoto moja toka mamlaka ya maji

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,072
1,697
Nawasalimu kwa jina la jumhuri ya Muungano wa Tanzania

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza!

Nimeamua kuanzisha mraji wa maendeleo ambao ungeweza kutoa ajira kwa takriban vijana kadhaa wa kitanzania,

Nimekwishafanya taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ya eneo la mradi, kodi zote za serikali nk

Changamoto kubwa inayoni face ni kukwamishwa na hawa watu wa mamlaka ya maji ambao wamekwaisha chukua pesa za kuunganisha maji halafu kushindwa kunifikishia huduma hiyo ya maji kwa wakati eti kwa madai ya kwamba kwa sasa shirika halina vifaa.

Nimewasilisha malalamiko yangu kwa diwani pamoja na mbunge wakaahidi kulifanyiakazi swala langu lakini mpaka hivi sasa halijapatiwa ufumbuzi

Hivyo nimekuja jukwaani nikiamini wapo watu wenye conection na viongozi mbalimbali wa kitaifa ili waweze kunisaidia kupaza sauti ikiwezekana hata kwa Waziri wa Maji maana naona changamoto yangu imekuwa kubwa kwa kuwa mkataba nilioingia na yule aliyenikodishia eneo umeshaanza kusoma na mimi bado mamlaka ya maji wanaendelea kunipiga kiswahili.

Hivyo mwenye contact ya wizara ya maji au hata mh wazir AWESO ani pm ili niweze kuwasilisha malalamiko yangu

Nimejaribu kuingia kwenye website ya wizara nimepata namba lakini nikipiga simu hazitoki nashindwa kuelewa ni kwa sababu gani.

Eneo la mradi ni Sengerema Mwanza na anayekwamisha ni mkurugenzi wa mamlaka ya maji Sengerema ( SEUWASA) sababu mamlaka yake ndio inadai kuwa haina vifaa na hawajui vifaa vitakuja lini uku pesa za wateja wamechukua.

Natanguliza shukrani zangu
 
Back
Top Bottom