Mwenye mamlaka ya kutangaza vita nchini ni mkuu wa majeshi au rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenye mamlaka ya kutangaza vita nchini ni mkuu wa majeshi au rais?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 25, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  General Davis Mwamunyange

  Mwamunyanga: Hatutaingia vitani na Malawi

  WIKI moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema Tanzania haina mpango wa kupigana na Malawi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange amerejea kauli hiyo na akisisitiza kuwa Tanzania haitaingia vitani na nchi hiyo. Akiwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika (Sadc) mjini Maputo Msumbiji, Rais Kikwete alisema kuwa uhusiano wa Tanzania na Malawi utabaki kama ulivyo na diplomasia zaidi itatumika.

  Jana katika hafla ya kuwaaga Meja na Mabrigedia Jenerali, kwenye Kambi ya Abdallah Twalipo, Mwamunyange alisema wananchi wasiwe na wasiwasi kuwa Tanzania itaingia kwenye vita na Malawi.

  “Suala la mgogoro huu, linazungumzika na wahusika wanalifanyia kazi kwa karibu,” alisema Mwamunyange.
  Wakati akisema hayo, kuna taarifa kuwa baadhi ya vikosi vya jeshi vimesogezwa kusini mwa Tanzania licha ya kuwa msisitizo kuwa hakuna mpango wa mapigano.


  Mbali na hayo, katika hafla hiyo ya jana walioagwa ni Meja Jenerali, Nicholas Miti, Festo Ulomi, Samuel Kitundu na Said Kalembo ambaye mara ya mwisho alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

  Wengine ni Brigedia Jenerali Matata Magwamba, Grayson Idinga na Loth Kilama ambao wamemaliza utumishi wa jeshi wa muda usiopungua miaka 35.

  Akizungumza kwa niaba ya wastaafu hao wa jeshi, Kalembo alisema, “Ninawataka Watanzania kudumisha upendo na mshikamano, kufanya kazi kwa kujituma ili kujenga taifa.”
  Aliwataka wale wanaoingia jeshini kuwa na nidhamu ya jeshi kwa kuwa wana jukumu kubwa la kulinda mipaka ya nchi kwa jumla. Hata hivyo, alipotakiwa na waandishi wa habari kuzungumzia mipango yake ya baadaye kama ataingia kwenye siasa, alisema, “Sifikirii hivyo, kwani ukiwa mwajeshi unakuwa na amri.”

  My Take:
  Ninachokifahamu mimi ni kwamba mwenye mamlaka ya kuamua na kutangaza vita au kusitisha vita ni Rais kikatiba. Sasa hili la Mwamunyange ambaye ndiye mkuu wa majeshi nchini kutoa tamko hili ni tatilo lile lile la kutifuka kwa lugha (system) kilichowapata Waajemi walipokuwa wanajenga mnara wa babel?
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwa utawala dhaifu Kama huu mtu yeyote mwenye hela za kifisadi Kama Rostam, Manji, Lowassa Na jeetu Patel wanaweza kutangaza vita na ikapiganwa
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  44.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa
  na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali
  ya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.

  (2) Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala ya
  tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya
  kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani
  ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha
  mkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiria
  kupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita
  lililotolewa na Rais.
   
 4. Imany John

  Imany John Verified User

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Je vita ya Tanzania na uganda vilipitia mchakato tajwa hapo juu?
   
 5. mkolosai

  mkolosai JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,147
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 280
  Mchakato huo ni maandishi tu hayo, wananchi wanakufa utasubiri siku 14 ili adui alipue kila kona?
   
 6. Kibada

  Kibada Senior Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais hawezi tangaza vita pasipo kushauriana "kiufundi" na Jeshi... Naona hapo Mwamunyange alikuwa anatoa sehemu tu ya taarifa anayoifahamu kuhusu tetesi za vita na Malawi. Mpaka Rais anatangaza vita ujue kwamba logistics zote za kijeshi ziliisha fanyika... Mobilization ya vifaa na majeshi inakuwa imekamilika... Ndio maana kama kuna chokochoko majeshi yanakuwa stand by lets say 75%, 50% au 25%. 100% stand by ujue kitanuka muda si mrefu.. Taarifa za mobilization ya wanajeshi wetu na vifaa kule kusini si jambo la kushangaza kwa sisi wazoefu... Hata chokochoko ndogo za uchaguzi mkuu wanajeshi wengi wanakuwa at least 25% stand by ...
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu ilivo mkuu wa majeshi anaweza kulianzisha na Rais asijue.. Japokua kikatiba hes the commander in chief lkn mmhh huyo mkuu wa majeshi hakutakiwa kuongelea hili swala ndo ujue jinsi hii nchi haina uongozi kila mtu anaropoka vya kwake
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa nukuru hii ya katiba ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mwamunyange amekiuka katiba ya nchi, yeye ni kupata amri ya kutekelezaji, na si msemaji wa rais kuhusu masuala ya uamuzi wa vita. Hicho ndicho nilichokishangaa mie.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na kauli yako, lakini unachoeleza ni mchakacho wa maandalizi ya vita, lakini uteleaji kauli ya uamuzi Rais na kama hayupo basi anayemfuata ni makamu wake. Afadhali angetamka hivyo Waziri Mkuu ingeeleweka kwa vile ni serikali inayotoa tamko, jeshi halitoi tamko ila linafanya utekelezaji wa maamuzi ya serikali.
   
 10. C

  CHOMA Senior Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mwenye Mamlaka ya kutangaza vita kikatiba ni Amiri jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee.Hao wengine wanafanya maigizo tu ya kisanii.
   
Loading...