Mwenye line ya Uwakala M-PESA naomba anisaidie

Mayova

Senior Member
May 10, 2018
182
123
Ndugu zangu wapendwa mwenye line ya M PESA ambayo haitumii naomba aniuzie au aniazime kwa makubaliano. Au kama kuna anaye jua namna ya kuzipata kwauharaka zaid line za Tigo pesa na M pesa
Natanguliza shukrani
 
Ukihitaji line ya uwakala ya TTCL! aka TTCL Customer Care unijulishe nikupe tu bure maana tangu nilipo isajili na kuweka float, sijawahi kupata mteja hata mmoja.

Sijui hawa Mabosi wangu wanakosea wapi? Yaani nyinyi ni wenyeji, lakini mnazidiwa na wageni. Kwa nini msishushe gharama za virushi na huduma zenu kwa kiwango cha chini kabisa ili kuvutia kundi kubwa la wateja? Kwa nini msijitangaze kupitiliza?

Nakaribia mwaka sasa tangu nilipoingia kwenye biashara ya miamala. Nakula Kamisheni kiduchu kutoka kwenye makampuni mengine tu. Ila siyo ttcl!
 
Ndugu zangu wapendwa mwenye line ya M PESA ambayo haitumii naomba aniuzie au aniazime kwa makubaliano. Au kama kuna anaye jua namna ya kuzipata kwauharaka zaid line za Tigo pesa na M pesa
Natanguliza shukrani

Kwa line za uwakala za Tigo Pesa najua kwenye maduka yao hawatoi maana wanawatu wanaita super agent kitu kama hicho: so kwa mkoa wa kinondoni najua wapo pale sinza mori big bon kuna ghorofa floor ya kwanza na pale sio kwamba wanaziuaza bali uwe na mtaaji wa kuanzia ambao ni 500,000/- pamoja na tin number na lesseni ya biashara kama sijakosea.
 
Ndugu zangu wapendwa mwenye line ya M PESA ambayo haitumii naomba aniuzie au aniazime kwa makubaliano. Au kama kuna anaye jua namna ya kuzipata kwauharaka zaid line za Tigo pesa na M pesa
Natanguliza shukrani

Kwa voda M-Pesa mara ya mwisho niliuliza walisema wamesitisha zoezi la kutoa hizo line za M Pesa sijajua sasa kwa sasa lakini ni vyema kutembelea maduka yao.
 
Ndugu zangu wapendwa mwenye line ya M PESA ambayo haitumii naomba aniuzie au aniazime kwa makubaliano. Au kama kuna anaye jua namna ya kuzipata kwauharaka zaid line za Tigo pesa na M pesa
Natanguliza shukrani
M-pesa walisitisha kutoa till toka July 2022 mpaka sasa wako kimya. Mimi ninayo line ya Tigopesa ambayo kwa sasa siitumii kama utakuwa tayari kuinunua nitakuachia kwa 150000 ni ya jina langu kila kitu Biometric Registration na Menu ya Tigo pesa. Niko Dar.
 
Shida ni pale utakapoamua kuifunga baada ya huyo jamaa kuinunua, yani ustawi wa biashara yake utategemea na maamuzi yako.
 
Shida ni pale utakapoamua kuifunga baada ya huyo jamaa kuinunua, yani ustawi wa biashara yake utategemea na maamuzi yako.
Nimekuwa kwenye biashara hii ya electronic money transfer mwaka wa 12 sasa,so changamoto zake nazijua vyema. Naelewa concern yako ila kwa uzoefu niliokuwa nao hicho kitu kuna watu wa hovyo wanawafanyiaga wenzao. Ushauri wangu siku zote kuepuka changamoto hizi wekeana mikataba pia kwa till kama ya Tigo ambayo inakubali transfer of names pale ambapo mnunuzi anakuwa na valid documents zake ni bora zaidi. Nadhani nimeeleweka bosi.
 
Back
Top Bottom