Mwenye kumfahamu Mtanzania huyu mkazi wa Magomeni, anateseka nchini Pakistan

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Wakuu kuna "clip" na picha kadhaa zinasambaa mtandaoni za Mtanzania,mwanaume na mkazi wa Magomeni.
Jamaa anasema kwao ni Magomeni mtaa wa Chemchem na Idrisa,Wazazi wake wanaishi hapo,Mama yake anaitwa Rukia Daudi na baba yake anaitwa Akida.



Huyu jamaa ukiangalia video anaonekana yupo katikati ya "Wanamgambo/askari" wawili wakiwa na bunduki na yeye akiwa amekalishwa chini huku akielekezewa mitutu ya bunduki.Anaanza kujielezea kwa kuomba msaada kuwa ndugu zake wafikishuwe ujumbe kuwa amekamatwa huko aliko(Nchi hajataja ila kwa mavazi ya hao askari ni moja ya nchi za Mashariki ya mbali,mavazi kama wanamgambo wa Pakistani au Afuganstan) na yupo kizuizini kwa sababu mtu aliyekuwa naye ambaye ni mtanzania mwenzake amedhulumu pesa hao "askari" na kutokomea.

Aliyedhurumu anaitwa Juma,kamtaja kwa jina moja tu la Juma,na anasema huyo Juma anaishi Kunduchi-Dsm na Mama yake huyo Juma anaitwa Mariam.Jamaa anasema huyo Juma katoweka na pesa za hao watu na ili yeye aachiwe,huyo Juma inabidi apeleke huo "mzigo" kwa hao jamaa.

Picha za huyo jamaa zimeambatanishwa,yoyote mwenye kuwajuwa wazazi wake hapo Magomeni mtaa wa Chemchemu na Idrisa awafikishie ujumbe ili huyu jamaa asalimike,maana jamaa anapigwa kwa vitako vya bunduki na makofi ya kufa mtu.Hao wanamgambo/askari wanaomtesa wamevaa viremba na kujifunika usoni,na kwa "dressing code" yao basi si ajabu wakawa ni nchi moja ya Mashariki ya mbali,kama si Pakistan au Iran basi ni Afghanstan.

Ndugu Juma popote ulipo rudisha au lipa "mzigo" wa hao jamaa uliotoweka nao ili mwenzako aachiwe,maana kwa mateso na kipigo anachokipata si kitoto.Hivi katika matukio kama haya,Wizara ya Mashauriano ya Kigeni ya Tanzania huwa ina nafasi gani??Hakuna juhudi zinazoweza kufanyika kujuwa huyu mtu alipo ili hata kama ni "muharifu" basi zifuatwe hatua stahiki na si utesaji kama huu anaoupata?Bila shaka hatua zitachukuliwa ili huyu "mtoto wa Migomigo" apate msaada.
image.png
image.png
image.png
image.png

Baada ya kuwa South Africa kimatembezi nilipata kujuana na Watz kibao lkn asilimia 80% walioko huku wengi wanategemea maisha kwa kuuza madawa ya kulevya tena hawajifichi kama huko kwetu.

Jana nilipata mkasa wa kijana wa Magomeni aliyewekwa bondi na rafiki yake Mtanzania huko Pakistan!!!

Bahati zuri hawa watu wanajuana sana hivyo nikapata nafasi ya kuongea na kijana mmoja(Mtz aliyeloea South Africa) ambaye alimfahamu kwa jina na sehemu anayoishi huyo kijana aliyewekwa bondi na aliyemweka bondi huyo rafiki yake huko Pakistan.

Kuwekwa bondi ni nini? Kuwekwa bondi ni utaratibu wanaoutumia wauza madawa ya kulevya ili kuchukua mzigo wa kutosha (kukopeshwa) na baada ya mauzo pesa hurejeshwa kwa wakopeshaji na wewe uliyewekwa bondi unaachiwa kurudi kula bata kwenu na wajanja wezako.

Sasa hao jamaa (sitawataja majina) walichukua mzigo Pakistan na kumweka bondi ndugu yao huko Pakistan, wameuza mzigo na kula bata pesa na kumtelekeza ndugu yao.

Jamaa wametoa muda kama hawajalipwa basi wanamuua na wametuma video kwa marafiki zake na ndugu zake ili watumiwe mzigo wao.
Serikali yangu naiomba ifuatilie hiyo video mitandaoni ili kuwatia nguvuni hawa watu kwani hiyo video imesambaa sana na naamini watajulikana kwa urahisi sana,

NB: Vijana wezangu tufanyeni kazi halali biashara ya madawa ya kulevya haina tofauti na ugaidi
d31ed19634e7a5d5c34cdc14fc7c6cdf.jpg
ae5f615e33f1634d746c66d359a3c481.jpg

NI mateso. Ndivyo unavyoweza kusema, hasa baada ya kundi la maharamia linalojishughulisha na bishara ya ‘unga’ nchini Pakistan kuelezwa kumtesa kijana Mtanzania, Adamu Akida.

Kutokana na hali hiyo, timu ya MTANZANIA ilipiga kambi jana katika eneo la Magomeni, Mtaa wa Idrissa, ambako pamoja na mambo mengine, ilifanikiwa kuzungumza na kaka wa Adamu aliyejitambulisha kwa jina la Hemed Abdallah (si jina lake halisi).

Akisimulia mkasa huo, alisema miezi minane iliyopita, Adamu alikwenda kwa kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo aliyetambulika kwa jina la Juma, na kuomba msaada wa mtaji kwani kazi yake ya kinyozi haikuwa ikilipa na hali ya maisha ilikuwa ngumu.

Baada ya kueleza shida yake hiyo, kaka yake huyo (Juma) alimuhoji kama yupo tayari kwa ajili ya kutafuta maisha nje ya nchi, na Adamu alikubali kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi aweze kupata pesa.

“Adamu kwa sasa ameshikiliwa kwa muda wa miezi minane, hatujui kama alikuwa ameingia katika janga hili hadi pale tulipoona video zake katika mitandao ya kijamii. Hapa aliyepo ni baba yake mdogo, Kessy Baharia na baba yake mzazi yupo Bagamoyo Mlingotini, ndiko anakoendelea na maisha yake.

“Awali alikwenda kwa kaka yake mtoto wa mama yake mdogo anaitwa Juma na kuomba asaidiwe mtaji kwani amekuwa na maisha magumu sana. Baada ya hali hiyo aliambiwa kuna safari ya kwenda Pakistan ambayo waliondoka wakiwa wameambatana watu watatu pamoja na Juma na kijana mwengine ambaye jina lake limenitoka, ila anaishi Kinondoni.

“Walipofika kule, Juma akachukua mzigo akiwa na yule kijana wa Kinondoni, huku Adamu akiachwa Pakistan kwa maelezo kuwa baada ya siku tano atakuja nchini na mzigo mwingine. Muda wote hata tukihoji alipo Adamu tunaambiwa yupo anaendelea na kazi huko aliko ana angerudi mwezi wa tisa nane.

“Sasa hii video ndiyo imetupa picha halisi ya Adamu, maskini sijui kama tutampata akiwa hai. Hata hivyo kwa kipindi cha hivi karibuni, tulikuwa tukishangazwa na mwenendo wa Juma kwani amekuwa na fedha nyingi sana hadi kufikia kuwajengea nyumba dada zake pamoja na kuwanunulia magari,” alisema Abdallah huku akibubujikwa na machozi.

Mke wake

Inaelezwa kuwa mke wa Adamu ambaye alikuwa akiishi Mtaa wa Sunna, Magomeni, alihamia Kijitonyama.

Kwamba alihamishwa na shemeji yake, Juma ambaye ndiye aliyempangia nyumba nyingine Kijitonyama.

“Katika suala hilo, tuna shaka kuwa hata mke wa Adamu anajua kinachoendelea, maana miezi mitatu iliyopita alihama Magomeni na kuhamia Kijitonyama, tena huku akisema mume wake karibu anarejea nchini.

“Lakini baada ya video kuanza kuonekana, sasa hata kupatikana hapatikani, na hatujui amehamia nyumba gani huko Kijitonyama,” alisema Abdallah.

Serikali ya Mtaa

Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Srikali ya Mtaa wa Idrissa, Issa Mpangile, alisema kuwa jana askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi walifika katika ofisi yake na kumtaka waongozane kwenda katika nyumba ya baba mdogo wa Adamu.

Alisema walipofika nyumbani kwa Kessy Baharia, ambaye ndiye baba mdogo wa Adamu, polisi walichukua maelezo yake na baadaye wakarudi katika ofisi ya Serikali ya Mtaa kuchukua maelezo ya mwenyekiti huyo.

Akizungumza kuhusu kijana huyo, Mpangile alisema kuwa ni mzaliwa wa mtaa huo, lakini baadaye alihamia Mtaa wa Suna ambao ni jirani na Mtaa wa Idrissa, Kata ya Magomeni.

Alisema wakati kijana huyo anahama mtaa huo, alikuwa bado ni kinyozi na hakuwa na rekodi ya kusafiri kwenda nje ya nchi.

“Wakati Adamu anahama Mtaa wa Idrissa, alikuwa bado ni kinyozi na hakuna rekodi kwamba alikuwa anasafiri nje ya nchi,” alisema Mpangile.

Alisema katika mazungumzo na Baharia, alimweleza kuwa amewasiliana na baba wa kijana huyo ambaye anaishi Bagamoyo mkoani Pwani.

Mpangile alisema kwa mujibu wa Baharia, baba wa kijana huyo anayejulikana kwa jina la Akida, amesikia habari za mtoto wake na kwamba atakwenda kuripoti kituo cha polisi.

Naye mama mdogo wa Adamu, aliyetambulika kwa jina la Khadija Katundu, alikiri maofisa wa polisi kumuhoji mume wake.

Alisema wameendelea kutoa ushirikiano kwa watu wanaofika nyumbani kuhoji kuhusu suala hilo, na kwamba wanaamini ufumbuzi utapatikana.

Serikali yahaha

Baada ya taarifa hizo kuripotiwa na gazeti hili jana, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi wanafanya mawasiliano na Serikali ya Pakistan ili kuangalia namna ya kumwokoa Adamu katika mikono ya maharamia hao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba, alisema tayari wamepata taarifa dhidi ya Mtanzania huyo.

“Kwa sasa tunafanya mawasiliano na wenzetu wa Pakistan tuone namna ya kumtoa kijana huyo katika mikono ya hao watekaji, na tukikamilisha hilo tutatoa taarifa rasmi juu ya jambo hili,” alisema Advera.

Wakati hayo yakiendelea, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, kupitia mmoja wa maofisa wa idara ya habari ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini, alisema wamepata taarifa ya tukio hilo, na sasa wanafanya mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Kaka huyo bwana hajasema Wapakistan au Wa Afghanstan ni Waarabu, alichosema anamuona jamaa yupo na watu/Askari ambao wanaweza kuwa Waarabu au hao Wapakistan au Wa afghanstan hope kimavazi
Mkuu Kituko ngoja turekebishe kuondoa utata,maana tunaweza kuhama kujadili mada tukahamia mada ya "Waarabu".Nimerekebisha ili kuondoa tofauti hii.Asanta Sana
 
Kaka huyo bwana hajasema Wapakistan au Wa Afghanstan ni Waarabu, alichosema anamuona jamaa yupo na watu/Askari ambao wanaweza kuwa Waarabu au hao Wapakistan au Wa afghanstan hope kimavazi
Kwqa kifupi "HILO NI GENGE LA WAUZA UNGA" na huyo aliyeshiliwa ni DHAMANA (rehani) !!
Lingine askari ni mtumishi wa USALAMA haiendani na taswira hizo !!
 
Back
Top Bottom