Mwenye kujua utaratibu ninaoweza pitia ili kurasmisha usindikaji wa gongo kuwa pombe rasmi kwenye soko

Kontoro

Member
Apr 24, 2020
20
42
Habari wana JF,

Nyumbani kwetu kijijini kuna shughuli ya usindikaji pombe aina ya gongo ambayo wanakijiji uifanya ili kuwaingizia kipato. Shughuli hii ni ya muda mrefu sana imefanywa toka enzi za mababu zetu na ni kati ya shughuli kubwa inazoziingizia kipato familia nyingi. Familia nyingi zinapata kipato kwa kutengeneza pombe aina ya gongo na hicho kipato kinawasaidia kulipa ada za watoto shule , chakula , matibabu e.t.c. Familia 8 kati ya 10 za hapo kijijini na vijiji vingine jirani zinajihusisha na utengenezaji wa hiyo pombe. Pia kati ya bidhaa inayo nunulika sana kijijini hapo ni gongo, maana inatumiwa kalibia na rika zote. Pia kila shughuli kama harusi, misiba, sherehe za aina mbalimbali lazima hiyo pombe iwepo. Hata na wazaliwa wa hivyo vijiji wanaoishi mjini wakijaga kijijini lazima waibebe hiyo pombe na kuipeleka mjini kwa kuifichaficha wasikamatwe na askari. Kiukweli soko hiyo pombe ni kubwa sana.

Inatengenezwa kwa kutumia ndizi maalum kwa ajiri ya pombe, hizo ndizi zinavundikwa kwa siku saba, baadaye hizo ndizi zinapondwapondwa ili kutoa togwa, Hiyo togwa inakamuliwa na kuchanganywa na mtama. Baada ya siku saba togwa ilichanganywa na mtama inakuwa ipo tiyari kwaajiri ya kupikwa. Mchanganyiko wa togwa wenye mtama unawekwa kwenye pipa la lita 100 na kuwekwa kwenye moto mkali, kwenye mdomo wa pipa zinawekwa mirija ambayo inaunganishwa na birika zilizowekwa kwenye maji ili kupoza mvuke. Mvuke uliopoa kwenye birika unakuwa tiyari ni kimiminika kinachotumika kama pombe, na kina rangi kama ya maji na radha ya pombe aina ya K-Vant, Tz Kinyagi n.k. Kiutalaamu wanatumia njia ya Fractional Distallation kuitengeneza hiyo pombe.

Hii pombe ina soko kubwa ila tatizo ni kwamba haijarasimishwa, na bado serikali inaichukulia kama pombe haramu. Nataka kujenga kama kiwanda ambacho kitakuwa kinanunua pombe zote ambazo zimesindikwa na wanakijiji na kuzifanyia packaging na kuzirudisha mtaani ili wanywaji watumie pombe hiyo hiyo ila ambayo imerasimishwa kwa kuwa na viwango ambavyo vinakubalika na mamlaka.

Naomba share na mimi kama unajua utaratibu wa kupata vibali kwenye taasisi yoyote mfano TBS, TFDA n.k. Na ni njia gani nizipitie kuweza kupata vibali vya pombe.

Aksante
 
Back
Top Bottom