Mwenye kujua tafsiri ya hii katuni

Mr.Wenger

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
2,518
5,820
e7541ce147645c9fe98184fb413aaace.jpg
Kama picha inavyojieleza, haya wataalam wenye kujua tafsiri kazi kwenu
 
Ndani ya sisiem kuna fukuta inampekekea sizonje ajingine na watu wake wenyewe huku uongozi ukiwamwaga nje. Katibu yuku bze kukiendesha chombo kifike salama
 
e7541ce147645c9fe98184fb413aaace.jpg
Kama picha inavyojieleza, haya wataalam wenye kujua tafsiri kazi kwenu
1. Mcheki nahodha wa chombo, anapiga vipi makasia? Kwa staili yake chombo hakiwezi kusonga mbele.
2. Mcheki kichwa, yeye anajikinga na mwavuli bila kujua hatari ya maji yanayoingia chomboni ni kubwa zaidi ya maji anayozuia na mwavuli.
3. Mcheki fasta fasta, muda si mrefu pumzi itamwishia maana matundu ni mengi naye anafanya kazi ya mtu mmoja tu.
 
e7541ce147645c9fe98184fb413aaace.jpg
Kama picha inavyojieleza, haya wataalam wenye kujua tafsiri kazi kwenu
1: Mtumbwi una matobo ya hatari, unaingiza maji kwa style ya kuyarusha juu halafu yanadondoka kama matone ya mvua kubwa.

Jamaa mmoja anaonekana akiwa bize kuyachota hayo maji kwenye mtumbwi na kuyamwaga ili mtumbwi usizame.

Mwingine yuko bize kupiga makasia, katika style ambayo mtumbwi unazunguka tu, hauwezi kwenda kokote unabaki kina kirefu!

2: Kuna jamaa hapo kati, (huyo mwenye kichwa cha ki peke yake) yeye akili yake inamtuma kujikinga kwa mwavuli tu.

(Alitakiwa kuhakikisha mtumbwi hauvuji na unaendelea na safari!!)

Kwa maji hayo ninavyoyaona, huyo jamaa anaechota hawezi, atachoka tu! mwisho watazama wote!
 
1. Mcheki nahodha wa chombo, anapiga vipi makasia? Kwa staili yake chombo hakiwezi kusonga mbele.
2. Mcheki kichwa, yeye anajikinga na mwavuli bila kujua hatari ya maji yanayoingia chomboni ni kubwa zaidi ya maji anayozuia na mwavuli.
3. Mcheki fasta fasta, muda si mrefu pumzi itamwishia maana matundu ni mengi naye anafanya kazi ya mtu mmoja tu.
Umejitahidi mkuu
 
Mchoraji licha ya kwamba ni mbumbumbu was Siasa, hata mchoro wake haujielezi kama alivyodhamiria.
 
hapo hiyo picha inamaanisha kuwa huyo jamaa wa katkat anaimani sana na dereva (tembo man) ndio maana amempa mgongo yaan hamwangalii, yy amekazana kumtzama mwosha chombo(fasta fasta), bila kujua kuwa anayesababsha maji kujaa kwenye mtumbwi ni dereva.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom