Mwenye kujua kuhusu majini alete muongozo hapa

20PROFF

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
8,147
7,116
Habari za saa hii,
Kuna tukio lililo nipa maswali kadhaa, mwenye uelewa na ujuzi anaweza toa mchango wake ikiwezekana kujuzwa hata kile nisicho ulizwa ila napaswa kujua. Tukio lilikuwa hivi.

Leo asubuh kishale ya saa tano tulikuwa katika kazi fulani hivi za kiserikali. Ghafla nikasikia na kuona watu wanatawanyika, asilimia kubwa walikuwa ni mabinti , kwa haraka nikahisi labda kuna nyoka ameingia walipo au kuna mdudu wa hatari. Kuangalia vzuri naona binti mmoja mwenye ushungi anatembelea magoti na kutaka kutoka nje

Nilichowaza fasta ni kufunga mlango asitoke maana nilishajua ni majini yamepanda, ila wakaniambia afande usifunge mlango waliogopa kukaa naye ndani coz kumbe huwa ana habiti ya kusambaza kichapo, nikamwachia mlango wazi, kisha kwenda next room ambapo kulikuwa na watu wengine maana nilikuwa kwenye usimamiz wa shughuli flan.

Kumbe after kutoka kule akaja kwenye ile room akaja moja kwa moja hadi mbele yangu , nikapiga hatua moja nyuma ili akileta wenge nimzbue kidgo akae sawa, akaniangalia akapita kando akaanza kumfuata binti mmoja ( ambayo kwa maelezo ya watu wanasema huwa hapendi marashi ya huyo binti na hapo kuna wengine wanamajin hawakutaka kukaribia wanasema hawataki shida) wamekimbizana sana
Tukaamua kumfungia ndani binti mwenye marashi ili asisumbuliwe.
Yule mwenye majini akawa dirishani anapiga kelele analia,
Sijui ikawaje tukaon yule mwenye marashi katoka nje wameshikana kipigo kikaanza

Watu wote wanakimbia dogo anapewa kipigo kavuliwa hijabu yake wote wakawa vichwa wazi, watu wanajarib
Bt hakuna mafanikio, tukajikuta mm na mwenzangu fulan tukaenda kumchomoa kwa nguvu tukamweka room nilikuwa na kamba mfukoni funga vizuri tukamkqza miguu na mikono kama Hostages

Kahangaika kashnidwa ule mzigo ukawa unahangaika sana baadae ukapiga kelele ukisema unamtaka yule binti aje, mwenzangu akasema haji akija utampiga hatumleti, baadae kelel zikaja anasema anakufa then kimya kikatawala.

Kila tukimwita dada mwnye kujua dini amsomee anasema hana udhu nikaona anazngua basi ikabidi tutumie udhu wa kijeshi kumtel aache wenge anamsumbua Kiti, akatulia. Tuka confirm kiti karudi tukaongea naye story nyingi tukajiridhisha ni yeye basi tuka mfungua kamba kalalmika maumivu ya kamba nikajua yes kiti ndo yeye.

Maswali yangu yakaanza hapa.

After story na dk kadhaaa tukaona mtu haongei, then akamwitea askari mwenzangu mimi namcheki tu, akaomba kikombe ambacho hakitumiki akasema hamna akasema kipoooo hakina mkono nipeni, then akamwita Binti mwingine mwenye majini aka mnongoneza kwa siri kisha tukaona binti analeta maji kwenye kikombe na mchanga yeye akamix akataka aongezewe tena ikawa mingi tu, akanywaa maji yote yalimixiwa na mchanga then akaaanza kula mchanga uliomixiwa na maji.

Nilienda chooni kurud nakutaa kaama rum then anamtel rafiki yangu aletewe yule binti mwingine then akasema ananitaka na mimi tule keki eti birthday yake keki yenye tope la mchanga na akatoa demo jinsi ya kula.

Kuja pale akawa aongei ila mwanzo alikuwa anaongea na wnzangu akaanza kugalagala.

Qn.
Why hao wnye majini wngine waogope kuja?
Why atake mchange na kuanza kunywa maji yalimixiwa na mchanga then kula tope??

Marashi yanahusu vipi na majini??
Why nikienda haongei anatoka macho na kuanza kugalagal ingawa alikuwa anaongea??

Kama kuna kitu napaswa jua pia nijuzeni
 
Huyo ni kituko tu. Jinni chizi na asiyejitambua na maana.

Jinni mwenye hadhi yake havuki mipaka yake na kumuingia binaadam.

Akikufanyieni kisa kama hicho tena mnamuadhinia tu, lazima atoke mbio.
 
Huyo ni kituko tu. Jinni chizi na asiyejitambua na maana.

Jinni mwenye hadhi yake havuki mipaka yake na kumuingia binaadam.

Akikufanyieni kisa kama hicho tena mnamuadhinia tu, lazima atoke mbio.
Unaweza nisadia pata majibu ya hayo maswali??
 
Huyo ni kituko tu. Jinni chizi na asiyejitambua na hana maana.

Jinni mwenye hadhi yake havuki mipaka yake na kumuingia binaadam.

Akikufanyieni kisa kama hicho tena mnamuadhinia tu, lazima atoke mbio.
 
natamani ningekuwa maeneo hayo niliitie jina la Bwana Yesu hapo mngeona mpambano mkali na huyo jini lazma angekimbia sema nyie mnapambana na jini kibinadami lazma awasumbue. Na huyo wala sio jini ni mapepo tu mashenzi wala hayana nguvu
 
nakumbuka kulikua na kabinti mtaani kwetu hapa kakipandisha hata mje kumi hamkawezi na kuna mchungaji aliingia kichwa kichwa kumuwekea mkono akazabwa kibao akaondoka kimya kimya tulivyoitwa alipiga magoti na kunyoosha mikono juu maana jina la Yesu si mchezo
 
Tofauti ni ipi ? Jini na mapepo?
 
nakumbuka kulikua na kabinti mtaani kwetu hapa kakipandisha hata mje kumi hamkawezi na kuna mchungaji aliingia kichwa kichwa kumuwekea mkono akazabwa kibao akaondoka kimya kimya tulivyoitwa alipiga magoti na kunyoosha mikono juu maana jina la Yesu si mchezo
Hii ina kumbusha kipindi cha juzi kati tu hapo, friend wngu alipopata demu mzuri yupo fresh kaenda nae geto kumbe ana majini kilichotokea Mungu anajua
 
Huyo ni kituko tu. Jinni chizi na asiyejitambua na maana.

Jinni mwenye hadhi yake havuki mipaka yake na kumuingia binaadam.

Akikufanyieni kisa kama hicho tena mnamuadhinia tu, lazima atoke mbio.

Inaonekana unajua mengi sana kuhusu jini!
 
sina uzoefu sana wala sifahamu zaidi ila nachojua ni kuwa ni mara chache jini kumsumbua mtu ila mapepo ndo hayo huwa yanavaa watu na kusumbua
 
Back
Top Bottom