Mwenye Kujua Dawa ya Kuangamiza Mende

Hahaaa kuna sehemu nilifika ukizima taa mende wanaruka sebureni kama kumbikumbi.
 
Mende wale wakubwa wa chooni. Dawa yao ni hii: Nunua vidinge 4 vile vya Ngao ya kuulia mbu, kisha changanya na maji ndoo moja. Kisha yamwage chooni. Mende kwisha habari yao.
ni kweli wanakufa ila after some time wanarudi. mimi kuna siku nilifua net nikamwaga hayo maji chooni looh nilishangaa sana kukuta mende wengi wamekufa. ila sa ivi wapo tena
 
MI Mende nawamalizaga kwa mafutataa Yaan hawayapendi kbs ukimpulizia kidog atakimbia Mpk atakufa mwenyew alafu Maeneo wanayopenda kukaa unapulizia hawatakanyaga
 
Mende ni wadudu hatari sana kwa afya inahitajika kufanya fummigation usafi hauwezi kumaliza vyanzo na mazalia kwa sasa inahitajika kufanya fumigation kuangalia kabisa Mende hao alafu usafi uzingatiwe isitokee tena pamoja na kupiga dawa baadae ya angalau kila baada ya miezi mitatu kwa huduma Nzuri na nafuu ya fummigation wasiliana nasi 0657835309 tutakusaidia
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Enyi matabibu wa JF.

nisaidieni wajameni. natafuta dawa ya mende wananisumbua sana. dawa za kihindi za kupuliza nimejaribu aina aina lakini nimenawa, maana nikiwapuliza wanalala tu badala ya kufa.

Dawa za kupuliza wamezigeuza viroba wanazitamani kweli ili walewe.

Mnaweza kuchukulia utani, ila niko siriaz.

Naomba msaada wenu wa kitabibu.
Japo ni post ya kitambo lakini nimegundua dawa mpya! Kwa bei nafuu mno na matokeo ni ya kushangaza
Nyunyiza chumvi kwenye nyufa na maeneo wanakopendelea kujificha, lakini hii ifanyike baada ya kufanya usafi na kutoa makorokoro yasiyo na faida
 
Back
Top Bottom