Mwenye kufahamu hii nguvu ya kiroho inatoka wapi

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
803
1,000
Ni vigumu sana kuthibitisha ukweli wa visa vya namna hii ambavyo usahihi wake unategemea imani yetu tu kwa msimuliaji,

Kwanini haya matukio yasiwe "objective" kama kuchomoza kwa jua au kuhisi baridi?

Ni vigumu kujua kinachoendelea kwenye ufahamu wa mtu aliyekufa kwa sababu ufahamu ni experience yako(yake) tu

Inawezekana kuwa ufahamu wa binadam unaendelea baada ya kifo, kwa sababu hiii tu moja kuwa ufahamu ni uzoefu wa mtu binafasi,

Ila kuna sababu nyingi za kuamini kuwa hakuna ufahamu wowote baada ya kifo

Kama source ya ufahamu ni ubongo,basi hakuna ufahamu baada ya kifo

Kama hauna kumbukumbu yoyote kabla ya kuzaliwa kwako basi hautakua na kumbukumbu yoyote baada ya kifo chako

At least kila binadamu aliyezaliwa tayari ana experience nzima ya maisha baada ya kifo

Maisha baada ya kifo = Maisha kabla ya kuzaliwa
 

Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
677
1,000
Aisee, Ni mizimu ya kwenu hiyo, hakuna nguvu ya Mungu hapo ni nguvu za Giza hizo, nakosa muda wa kukuandikia , lakin ujue shetan anaweza jibadili pia kuwa malaika wa nuru,

Na pia ujue kuwa hakuna ushirika kati ya walio kufa na walio hai.
Hivyo saut uliyo isikia imebebwa tu lakin sio muhusika anaye ongea.

Niombee nipate muda niombe nipate maandiko nikuwekee hapa, cz muda sio rafiki Sana sikuhiz. Bt kwa Kiasi nimekujibu
 

Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
677
1,000
Aisee, Ni mizimu ya kwenu hiyo, hakuna nguvu ya Mungu hapo ni nguvu za Giza hizo, nakosa muda wa kukuandikia , lakin ujue shetan anaweza jibadili pia kuwa malaika wa nuru,

Na pia ujue kuwa hakuna ushirika kati ya walio kufa na walio hai.
Hivyo saut uliyo isikia imebebwa tu lakin sio muhusika anaye ongea.

Niombee nipate muda niombe nipate maandiko nikuwekee hapa, cz muda sio rafiki Sana sikuhiz. Bt kwa Kiasi nimekujibu
Ulishawahi kusoma Mkasa wa Mfalme Sauli na Nabii Samweli? Samweli akiwa mfu, alizungumza na Sauli kwa mganga wa jadi, sijui unalizungumziaje lile tukio.
 

Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
677
1,000
Kwanza kuhusu kufa na kwenda mbinguni moja kwa moja so kweli labda hukuelewa
Kwa mujibu wa neno la MUNGU kwenye biblia mtu akifa huenda Kati ya sehemu mbili yaani peponi au kuzimu kulingana na uchaguzi aliouchagua yaani kumfuata Yesu Kristo au shetani. ( Luka 23:43, Luka 16:22-31)
Lakini mbinguni tutaenda pale Yesu Kristo atakapokuja siku ya parapanda kuwafufua waliokufa katika Kristo na kuwanyakua wale walio wake (Mathayo 24:31; 1 Wakorintho 15:52; 1 Wathesalonike 4:16)

Halafu swali lako Hilo la namna gani mtu aliyekufa huweza kuongea ?
Soma 1 Samweli 25:1 na 28:3,11,12,14,15,16
Hivyo inawezekana nafsi ya mtu kuamshwa kutoka huko kuzimu. Lakini kumbuka kinachokufa ni mwili Ila nafsi yake na Roho yake havifi.

Lakini kumbuka ili Vilivyopo katika ulimwengu wa Roho viweze kufanya kazi katika ulimwengu huu vinahitaji mwili huu wa nyama. Hivyo Mungu anamtumia mwanadamu aliyemuumba kufanya makusudi yake na kuuneza ufalme wake hapa duniani pia shetani humtumia mwanadamu kuueneza ufalme wake hapa duniani.

Umeshangaa kuona pepo yakiwatumia ndugu zako kuongea na ninyi?
Mbona hata Mungu hutumia wanadamu kuongea na watu.

Labda nikuongezee kitu Cha kukushangaza zaidi. Je unajua kuwa Mungu anaongea na watu wake Kila siku?
Unajua kuwa Kuna watu wanatokewa na Yesu Kristo na Malaika wa Mungu katika ulimwengu huu na hata hapa Tanzania?
(Hili nililoliandika hapa si la kusimuliwa Bali Ni maisha yangu na familia yangu Kila siku)

Ningeweza kuandika mengi lakini yote yapo kwenye biblia. Ukisoma na ukashindwa kuelewa muulize Mungu atakujibu kikubwa muombe akufungulie masikio na macho yako ya rohoni kwa Jina la Yesu Kristo utamsikia tu. ( Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Isaya 1:18)
Mkuu naunga hoja mkono, ila shida kuna mkanganyiko wa wapi mtu(roho/nafsi) anaeenda akifa. Maana kuna mkanganyiko Sana, ndani ya biblia. Jibu siyo Moja kama uliainisha kuwa Kati ya sehemu mbili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom