Mwenye kufahamu hii nguvu ya kiroho inatoka wapi

Kama unaongeaga na Mungu basi mwambie anitokee na mimi
Unataka Mungu akutokee ili iweje? Kamaunasoma biblia utaona kuna watu wengi ambao waliishi kabla yetu ila Mungu(Yesu) aliwatokea watu wachache waliokuwa na kazi maalumu kutoka kwake mfano Musa, Yohana, Ibrahimu, na wengine wengi lakini hawakuomba awatokee. Pia kuna wakati wana waisraeli waliomba kama unachotaka wewe lakini alipowatokea hawakutamani tena kumuona Kutoka 19:10-25 na Kutoka 20:18-19. Kwa watumishi wa Mungu wanaweza kuyaelewa haya maneno zaidi maana kuna wakati Mungu anasema na mtumishi wake juu ya jambo ambalo wamekosea watu wengine hadi mtumishi unaiona hasira ya Mungu na hofu inakukuta kiasi kwamba unaanza kumwambia Mungu unisamehe. Tuache mambo ya kitoto maana kuna vitu ukiviomba wewe mwenyewe unaweza ukajiuliza hivi kweli nilichomba kina maana katika maisha yangu?
 
Unataka Mungu akutokee ili iweje? Kamaunasoma biblia utaona kuna watu wengi ambao waliishi kabla yetu ila Mungu(Yesu) aliwatokea watu wachache waliokuwa na kazi maalumu kutoka kwake mfano Musa, Yohana, Ibrahimu, na wengine wengi lakini hawakuomba awatokee. Pia kuna wakati wana waisraeli waliomba kama unachotaka wewe lakini alipowatokea hawakutamani tena kumuona Kutoka 19:10-25 na Kutoka 20:18-19. Kwa watumishi wa Mungu wanaweza kuyaelewa haya maneno zaidi maana kuna wakati Mungu anasema na mtumishi wake juu ya jambo ambalo wamekosea watu wengine hadi mtumishi unaiona hasira ya Mungu na hofu inakukuta kiasi kwamba unaanza kumwambia Mungu unisamehe. Tuache mambo ya kitoto maana kuna vitu ukiviomba wewe mwenyewe unaweza ukajiuliza hivi kweli nilichomba kina maana katika maisha yangu?
Unausonji?
 
Nimetuma hiyo attachment lakini sijajua huwa inafunguliwaje maana sio mzoefu sana, na kila niki bonyeza naona inanipeleka kwenye home page ya JF lakini kwa ufupi naomba nikujibu kama ifuatavyo.

Kwanza inabidi utambue kuwa kuna aina kama tatu za nguvu za imani zinazooperate katika ulimwengu wa kiroho na hizi ndio zinazoongoza matukio yanayofanyika mwilini. Na binadamu sisi katika njia moja au nyingine tunahusiana nazo kwa kujua au bila kujua.
Na nguvu hizo za imani ni kama vile,
1. Satanist( Hii ni nguvu ya imani inayotokana na uchifu, mizimu ya ukoo na mababu na uganga wote wa kienyeji na kuagua na uchawi uko hapa na hicho kilichotokea kwa hao baba wadogo kiko hapa hizo tunaita roho zinazofatilia (mikuri na mahurunat) Sio babu huyo yeye tayari yupo somewhere else ila hizi ni roho zinazofatilia mateso na vifungo vya ukoo uzuri na mimi ni kabila hilo na hicho kitu sio kigeni kwangu na mara nyingi huwa wanayauliza tufanye nini ili hali itulie yanatoa masharti na yakifuatwa hali huwa shwari ingawa inakuwa ni namna fulani ya utumwa kwa kabila au ukoo husika na hufanya hivi makusudi ili yaendelee kutambulika na kutambikiwa katika kila kizazi hata kama wahusika waliyoyakaribisha wameshakufa,ila mwanzoni sikuelewa mpaka nilipoanza kuchimba kutafuta ukweli wa mambo na nikawaletea sehemu kidogo sana ya nilicho nacho.na aina hii ya nguvu za imani imeenea sana Africa na Asia
2. Satans (Hawa ndio wengine huwaita devil worshippers ni wanadamu wenzetu kabisa lakini kwa sababu mbali mbali wao wamejitolea kikamilifu kuwa waabudu shetani kwa asilimia mia hawa hawaruki na ungo hawawangi uchi usiku hawana matunguri wala hirizi, wao ni wachawi wa high level unakuta kapiga suti yake safi huku anasukuma v8 yake, kinachowapa nguvu sana kuliko Satanists ni mkataba walioingia katika kumtumikia shetani kama mungu wao na hivyo kupokea uwezo wake moja kwa moja bila kutumia tunguli, na aina hii ya nguvu ya imani imeenea sana katika nchi za ulaya na marekani
3. Kafiruna (Mtanisamehe wakristo wenzangu maana sijapata tafsiri ya neno hili lakini nitalielezea kwa jinsi ya maarifa niliyonayo ila hii ndio nguvu inayotokana na Jina la Yesu na wenye imani hii .

Na katika viwango vya uwezo uSatans unanguvu kuliko uSatanist na Kafiruna ipo ontop of all.(msininukuu vibaya sijaegamia upande wowote mi nasema ninachokijua)

Ikumbukwe kuwa Satanist na Satans zinahusiana kwa namna fulani kwa sababu ya originality kwa kuwa zote zinatoka kwa ancestor mmoja aliyejulikana kama Lucifer.

Ila ya kafiruna ipo tofauti na ni kinyume cha hizo zote mbili na kama nilivyosema ndio yenye nguvu kushinda zote kwa sababu ina originality ya muumbaji wa vyote mwenye uweza wote .

Kuna elimu sana pana hapo kwanini iwe hivyo lakini nipende kuishia hapo labda kama kutakuwa na swali unaweza uliza, lakini kuhusu wafu wanapoenda nimetuma video attachment sijui huwa mnafunguaje lakini na penyewe kuna elimu nzito kidogo, ila kwa ufupi kinachokufa ni mwili na mtu sio mwili, ila ni Nafsi hai inayoishi ndani ya mwili wa udongo, lakini wakristo wenzangu wamefundishwa na kuaminishwa mtu ni mwili kitu ambacho si kweli mwili ni nyumba tu ambayo mpangaji wake mmiliki anaweza kuishi humo au nje ya humo na ndio maana Satanist na Satans wanaonekana kimtazamo ingawa sio uhalisia wananguvu kuliko wakristo ni kwa sababu wanaelewa mtu ni nani roho nini na nafsi ni nini kitu ambacho wakristo wengi hawafahamu, naomba niishie hapa kwa sasa kama nitakuwa na muda tutaendelea ila kama utakuwa na swali au dukuduku usisite kuuliza.
Ukristo una nguvu kuliko hizo Satanist zako na Satans ndo maana jina la Yesu ni kiboko ya nguvu zote za giza,pia wakristo tunajua mwili ni kama jumba tu, Kama huujui ukristo ni Bora ukae kimya ufunge huo mdomo🚶🚶🚶🚶🚶
 
NDUGU NAONA BADO HUNA UFAHAMU KUHUSU KITU KINAITWA MIZIMU, MIZIMU NI AINA YA PEPO WANAO FANYA MAGANO AU MAKUBALIANO NA FAMILIA UKOO AU MTU BINAFSI.SASA KILICHO TOKEA KWENYE FAMILIA YENU NI KWAMBA KUNA MAAGANO YA MIUNGU KATIKA FAMILIA KINACHO ZUNGUMZA HAPO SIO MAREHEMU BALI NI MIUNGU MAANA KI BIBLIA
“Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake.

— Luka 20:38
UNAONA MUNGU WETU NI MUNGU WA WALIO HAI UKISHA KUFA HUNA FURSA YA KUZUNGUMZA NA WALIO HAI HAIPO HIYO...HIYO NI MIZIMU ILIKUWA IKIONGEA NA HUYO NDUGU AKIPELEKWA KWA MTUMISHI WA MUNGU ALIYE VIZURI ANAFUNGULIWA VIZURI NA KUWEKWA HURU
 
Mzee wenu alikuwa na majini/mizimu.

Ndio yanataka mrithi..

Binadamu binafsi hawezi fanya mambo hayo, ni majini ya huyo mzee ndo yanaongea na kutenda kazi, na yanataka mrithi wa mikoba hiyo.
Mtumishi sema mizimu 😁,toa makini hapo!
Maana hizi ndo spirit Huwa zinasimamia Koo.
 
NDUGU NAONA BADO HUNA UFAHAMU KUHUSU KITU KINAITWA MIZIMU, MIZIMU NI AINA YA PEPO WANAO FANYA MAGANO AU MAKUBALIANO NA FAMILIA UKOO AU MTU BINAFSI.SASA KILICHO TOKEA KWENYE FAMILIA YENU NI KWAMBA KUNA MAAGANO YA MIUNGU KATIKA FAMILIA KINACHO ZUNGUMZA HAPO SIO MAREHEMU BALI NI MIUNGU MAANA KI BIBLIA
“Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake.

— Luka 20:38
UNAONA MUNGU WETU NI MUNGU WA WALIO HAI UKISHA KUFA HUNA FURSA YA KUZUNGUMZA NA WALIO HAI HAIPO HIYO...HIYO NI MIZIMU ILIKUWA IKIONGEA NA HUYO NDUGU AKIPELEKWA KWA MTUMISHI WA MUNGU ALIYE VIZURI ANAFUNGULIWA VIZURI NA KUWEKWA HURU
Km hajaelew hapa 🤷🤝
 
Kwanza kuhusu kufa na kwenda mbinguni moja kwa moja so kweli labda hukuelewa
Kwa mujibu wa neno la MUNGU kwenye biblia mtu akifa huenda Kati ya sehemu mbili yaani peponi au kuzimu kulingana na uchaguzi aliouchagua yaani kumfuata Yesu Kristo au shetani. ( Luka 23:43, Luka 16:22-31)
Lakini mbinguni tutaenda pale Yesu Kristo atakapokuja siku ya parapanda kuwafufua waliokufa katika Kristo na kuwanyakua wale walio wake (Mathayo 24:31; 1 Wakorintho 15:52; 1 Wathesalonike 4:16)

Halafu swali lako Hilo la namna gani mtu aliyekufa huweza kuongea ?
Soma 1 Samweli 25:1 na 28:3,11,12,14,15,16
Hivyo inawezekana nafsi ya mtu kuamshwa kutoka huko kuzimu. Lakini kumbuka kinachokufa ni mwili Ila nafsi yake na Roho yake havifi.

Lakini kumbuka ili Vilivyopo katika ulimwengu wa Roho viweze kufanya kazi katika ulimwengu huu vinahitaji mwili huu wa nyama. Hivyo Mungu anamtumia mwanadamu aliyemuumba kufanya makusudi yake na kuuneza ufalme wake hapa duniani pia shetani humtumia mwanadamu kuueneza ufalme wake hapa duniani.

Umeshangaa kuona pepo yakiwatumia ndugu zako kuongea na ninyi?
Mbona hata Mungu hutumia wanadamu kuongea na watu.

Labda nikuongezee kitu Cha kukushangaza zaidi. Je unajua kuwa Mungu anaongea na watu wake Kila siku?
Unajua kuwa Kuna watu wanatokewa na Yesu Kristo na Malaika wa Mungu katika ulimwengu huu na hata hapa Tanzania?
(Hili nililoliandika hapa si la kusimuliwa Bali Ni maisha yangu na familia yangu Kila siku)

Ningeweza kuandika mengi lakini yote yapo kwenye biblia. Ukisoma na ukashindwa kuelewa muulize Mungu atakujibu kikubwa muombe akufungulie masikio na macho yako ya rohoni kwa Jina la Yesu Kristo utamsikia tu. ( Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Isaya 1:18)
Naamini kapata kitu 🤝
 
Aisee, Ni mizimu ya kwenu hiyo, hakuna nguvu ya Mungu hapo ni nguvu za Giza hizo, nakosa muda wa kukuandikia , lakin ujue shetan anaweza jibadili pia kuwa malaika wa nuru,

Na pia ujue kuwa hakuna ushirika kati ya walio kufa na walio hai.
Hivyo saut uliyo isikia imebebwa tu lakin sio muhusika anaye ongea.

Niombee nipate muda niombe nipate maandiko nikuwekee hapa, cz muda sio rafiki Sana sikuhiz. Bt kwa Kiasi nimekujibu
Kwani Samuel alivyokufa aliongea na Nani vile??? Connection ipo sana tu
 
Watu hawaelewi haya mambo Mimi ni mhaya naomba kueleza kidogo, mizimu ipo na Ina nguvu Sana, sitaki kuifananinisha na Mungu , nitakufuru , lakini kabla ya kuja kwa dini hizi za kigeni mizimu iliabudiwa, kiufupi yenyewe hufuatilia mambo yanavyokwenda kwenye ukoo, na sio kwamba ni ngu ya shetani , hapana ile Mimi naamini binadamu hafi kabisa, ni mwezi mmoja umepita kijijini kwetu Kuna mzee alifariki muda mrefu , Sasa vijana wa ukoo ule wakaoa baadhi wake zao ni wachawi ,Tena mmoja ni mchawi hata Kijiji kizima kinajua na hata kule alikotoka anajulikana, baada ya miaka kadhaa mzimu ukamkamata Binti ambaye ni mjukuu wa yule mzee ! Sasa kilichotoekea ilikuwa timbwili , akawa Binti anaongea sauti ya mzee anasema mke fulani ameniharibia mji ni mchawi anataka kuwaua vijana wangu wote , na kweli Kuna vijana wawili walifariki mazingira ya utata Sana mmoja Alicia ziwa Victoria mpaka Leo mwili haukuonekana kumbe huyo mama ndo alimchukua kiuchawi , baadae yule Binti sauti ikawa ya yule mama Sasa akaanza kuomba msamaha akataja watu alioua na mipango yake mingine

Mama yule , baada ya tukio , kikao kikafanyika akakili kabisa na kusema hatarudia , lakini mzimu ulikuwa umesisitiza aondoke siku hiyohiyo bila kuchelewa
Ukoo wakamfukuza, kwa ufupi mizimu ya kihaya ni mizuri Sana ndo maana sio rahisi kumdhuru mhaya ambaye mizimu yake ni mikali ndi maana pia kwa wahaya hakuna waganga , wametokea hivi karibuni baada ya watu kushindaa kufuatilia mizimu , in short mimi tangu nakua mpaka Leo sikuwahi kuona mganga lakini nilikuwa nakingwa Sana katika matukio mengi mpaka mwenyewe nasema labda mizimu

Ikitokea mtu mbaya amekuja kwenye ukoo wa wahaya wenye mizimu inayofuatiliwa vizuri hawezi kukaa hata sekunde

Hivyo naona Kuna jambo wahaya tunalo nadhani watu wa Imani waende kule wafanye tafiti
Mkuu ulichoelezea nimekishuhudia 100% ila nachoona hivi vitu vinapotea na kukosa nguvu kwa kukosa wa kuviendeleza
 
Ikumbukwe mizimu ya buhaya ni tofauti kabisa na mizimu ya makabila mengine hata matambiko yalikuwa tofauti Sana , mizimu ya wahaya Inafanana Sana na ya Waganda kwa asilimia 100,

Na mizimu ya wahaya ina Koo maalumu na Ina miiko maalum, kama Kuna mtu amewahi kufika kwenye eneo la makazi ya Kabaka kule Uganda , nadhani alijifunza mengi kuhusu mizimu

Mizimu ni roho zinaishi na zinasaidia Sana Koo zao kuziepusha na majanga au matatizo na watu wabaya

Sasa kwa hiyo mzee Cyprian ni kwamba ilikuwa ni lazima mtoto wake mkubwa awepo amzike baba yake , kwa ufupi mizimu Ina wivu Sana na inapenda Sana utaratibu ,

Iliona amekaidi na ingekuwa Hana nauli au alternative ya kufika kumzika Wala isingemzuru lakini ilikuwa inaona kila kitu anachofanya na inajua kabisa alikuwa anaweza kufika ikabidi kumuadhibu,
Pia mizimu ya kihaya ni mikali saaana,

Mizimu Irungu , mfano au Mugasha , Mugasha ni mzimu wa maji / ziwa huu mzimu unaweza kumtembeza mtu kupita ziwa Victoria mpaka Bukoba juu ya maji bila ye kujua , mifano ninayo, pia ilungu ni mizimu ya pori / uwindaji hii Kuna mtu nilishuhudia anaingia kwenye moto wa Kuni nyingi Sana bila yeye kujua nilidhani atatoka mifupa tu lakini alitoka mzima bila kuungua hata shati , hapo ni mizimu ikiwa imekasirika labda Kuna jambo sio sawa kwenye ukoo
Umeongea mengi kuhusu mizimu hasa ya wahaya na mpaka majina umetaja.Lakini nafikiri kuna jambo inabidi tulijue kwanza ndo tuweze kujua kama hiyo mizimu inatufaa au la.
Kwanza jamii nyingi kama sii zote za
Kiafrika zilikuwa au zina mizimu .Na kabla ya kuja imani kuhusu Mungu mmoja/Yehova watu waliabudu miungu hiyo ya makabila au koo.Ila baada ya imani ya dini automatic hiyo mizimu ilipoteza nguvu hasa kwa zile koo ambazo waliacha kufuata taratibu za hiyo mizimu na kumfuata Mungu moja kwa moja.
Lakini koo nyingine ziliendelea na yote mawili dini na mizimu nahisi hata mzee Cyprian alikuwa kwenye kundi hili ndo maana Ana jina la Kikristo na mizimu inawavaa wanaukoo.
Sasa tujiulize hii mizimu ni nini?Je ni kweli mtu aliyekufa anaweza kuongea kupitia mtu aliye hai?
Majibu ni rahisi sana.Mizimu ni roho chafu/mapepo/majini au mawakala wa shetani ambao walikaribishwa na familia/ukoo/kabila kwa kuingia nayo makubaliano maalumu na kwamba wao watu watafanya mambo kadha wa kadha kwa hiyo mizimu mfano kutambika nk na mizimu itawalinda.
Mara nyingi/zote mikataba hii inakuwa kizazi baada ya kizazi .Ndo maana kuna baadhi ya makabila/koo hata ukizaa naye na asijue
Mizimu bado itamwandama mtoto mradi tu ni damu ya huo ukoo.
Kimsingi kwa Wakristo kuitumikia mizimu kwa namna yo yote ni kosa ndo kuabudu miungu.Kama umejikuta kwenye jamii ya aina hiyo inakubidi wewe binafsi uachane kabisa na mizimu na umfuate Kristo kwa uaminifu vinginevyo utakuwa unasumbuliwa na hiyo mizimu.
Na kuhusu Marehemu kuongea kupitia mtu aliye hai kifupi sii kweli anayeongea hapo ni mzimu na mzimu kwa kuwa ni roho huwa anaweza kujigeuza atakavyo.Kuna visa vingi ambavyo hata mtu alokufa vizazi vingi nyuma anaongea kwa njia ya kimzimu kupitia watu walio hai.Na yumkini wanasema hata mambo ya ukweli.lakini anayeongea siyo marehemu ni mzimu tu kajigeuza.Kumbuka mzimu hafi ni roho na yupo miaka mingi nyuma tangu jamii ilipoingia naye makubaliano.Lakini yote kwa yote hutakiwi kutii hayo shikilia imani yako kwa Kristo Yesu na kamwe usiichanganye na imani ya mizimu maana haviendi pamoja.
Nina kisa alichonisimulia bibi yangu kuhusu mizimu ya wachaga jinsi ilivyokuwa na nguvu lakini baada ya kupokea Ukristo mizimu hiyo automatic imepoteza nguvu hizo.Kimsingi tumwamini Mungu tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom