Mwenye kufahamu hii nguvu ya kiroho inatoka wapi

ulimi waupanga

JF-Expert Member
Aug 31, 2014
216
500
Wakuu habari? Naomba nichangie uzoefu wangu nilioushuhudia mwenyewe kwa macho yangu.

Kwenye imani ya Kikristo kuna sehemu imeandikwa" Mtu akifariki haoni, hasikii wala hajui chochote kinachoendelea Duniani" na pia kuna maelezo kwamba unapofariki roho yako inakwenda kwa Mungu moja kwa moja.

Shida yangu ni kwamba, kwenye jamii yetu ya Kihaya kuna kitu wanaita( nchweke) hii ni hali inampata mtu anakuwa kama kapandwa na mashetani lakini inakuwa ni roho ya mtu x aliyeshafariki tayari ambapo mtu huyo anaanza kuongea kwa sauti na rafudhi ya marehemu akikemea au kutoa taarifa ya jambo Fulani.

Nimekuwa nikisikia tu watu wakisimulia hili jambo lakini nikawa naichukulia kama ngano za kiafrika lakini mwaka Jana mwezi wa 12 Babu yetu kipenzi Mzee Cypriani alitutoka. Kama tamaduni zetu zilivyo tulijumuika wote kwenda kijijini kwenye msiba wa Babu hisipokuwa baba Mkubwa ambaye ndo mtoto Mkubwa wa babu alishindwa kufika kwa wakati akipanga kufika mwezi wa kwanza maana kajichimbia machimboni Msumbiji.

Siku ya Mazishi ilipofika tukatoka Malaloni(Makaburini) kumstiri Mzee ile tunafika tu ndani tukiwa kundi kubwa la watu na nyimbo za maombolezo zikitawala gafla Shangazi akadondoka akawa kama amepata kifafa Mara babu Mdogo na baba Mdogo nao wakaanza kama kuweuka. Watu wakaanza kutawanyika ovyoovyo maana ilikuwa ni taflani gafla. Wazee wa ukoo wakakusanyika wakaanza kuchoma majani machanga ya migomba na kuwawekea puani wale waliokabwa na kitu kisichojulikana huku wakiomba kilichowakaba kiongee.
Mara gafla wote watatu wakaanza kuongea kwa pamoja, sauti moja ya babu tuliyetoka kumzika mda huo huo. Akaanza kuwauliza wazee wa ukoo kwamba kwanini wamekubali kumzika bila mtoto wake Mkubwa kufika? Wakajitetea hapo na akawambia siyo kweli kwamba baba Mkubwa hana nauli Bali yuko bize tu na machimbo yake, akasema kabla baba Mkubwa hajafika nyumbani iyo tarehe aliopanga kuja atakuwa ameshamtembelea huko huko msumbiji aliko.

Niachane na iyo stori maana ni ndefu kidogo lakini swali langu ni kitu gani kinatokea kwa watu kama hawa kuweza kupanda juu ya vichwa vya wengine wakati wamekufa tayari? Je roho zao zinakuwa na kitu gani cha kipekee mpaka wawe na uwezo huu maana wengi ni wazee ndo wanaweza kufanya hili.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,403
2,000
Kimsingi hakuna anayejua mtu akifa nini hutokea. Hata hizi dhana za jehanamu na mbinguni ni dhana tu za kutunga.

Binafsi naamini binadamu hafi. Ila ana badilika kutoka ubinadamu kuwa kitu kingine ambacho ni superior zaidi ya binadamu. Yaani ni kama ame graduate.

Hiki kiumbe kipya kimepewa majina tofauti kama mzimu, roho etc.

Ndo maana kabla ya hizi dini za kisasa kuingia, babu zetu walikuwa na mila zao kuelezea dhana hii. Ndo maana walitambika, waliomba mvua na mambo mbalimbali na yakatokea.
 
Divine...

JF-Expert Member
May 22, 2015
1,551
2,000
Aisee, Ni mizimu ya kwenu hiyo, hakuna nguvu ya Mungu hapo ni nguvu za Giza hizo, nakosa muda wa kukuandikia , lakin ujue shetan anaweza jibadili pia kuwa malaika wa nuru,

Na pia ujue kuwa hakuna ushirika kati ya walio kufa na walio hai.
Hivyo saut uliyo isikia imebebwa tu lakin sio muhusika anaye ongea.

Niombee nipate muda niombe nipate maandiko nikuwekee hapa, cz muda sio rafiki Sana sikuhiz. Bt kwa Kiasi nimekujibu
 
Akili 7

JF-Expert Member
Apr 22, 2019
528
1,000
Mizimu ya ukoo hiyo wala siyo marehemu, yeye ashakufa na sehemu yake haipo tena duniani
 
Mzee Wa Kale Kabisa

JF-Expert Member
Mar 25, 2018
2,463
2,000
Kimsingi hakuna anayejua mtu akifa nini hutokea. Hata hizi dhana za jehanamu na mbinguni ni dhana tu za kutunga.

Binafsi naamini binadamu hafi. Ila ana badilika kutoka ubinadamu kuwa kitu kingine ambacho ni superior zaidi ya binadamu. Yaani ni kama ame graduate.

Hiki kiumbe kipya kimepewa majina tofauti kama mzimu, roho etc.

Ndo maana kabla ya hizi dini za kisasa kuingia, babu zetu walikuwa na mila zao kuelezea dhana hii. Ndo maana walitambika, waliomba mvua na mambo mbalimbali na yakatokea.
Nilidhani umesema hakuna aanayejua...
 
Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,287
2,000
Aliyesema kuna wajinga wanaosema hakuna Mungu, yeye ana uhakika gani kama Mungu yupo? Sema Kama yupo ana umbo gani? Nani mjinga, anaeamini kisichoonekana au ambae haamini katika kisichoonekana ? Tuseme Karl Marx aliyekataa uwepo wake ni mjinga? Ni imani ya mtu kusema hakuna Mungu, ili apambane na hali yake, hapotezi mda kuamini kitu kisichoonekana.
 
maforce

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
541
500
Kwanza kuhusu kufa na kwenda mbinguni moja kwa moja so kweli labda hukuelewa
Kwa mujibu wa neno la MUNGU kwenye biblia mtu akifa huenda Kati ya sehemu mbili yaani peponi au kuzimu kulingana na uchaguzi aliouchagua yaani kumfuata Yesu Kristo au shetani. ( Luka 23:43, Luka 16:22-31)
Lakini mbinguni tutaenda pale Yesu Kristo atakapokuja siku ya parapanda kuwafufua waliokufa katika Kristo na kuwanyakua wale walio wake (Mathayo 24:31; 1 Wakorintho 15:52; 1 Wathesalonike 4:16)

Halafu swali lako Hilo la namna gani mtu aliyekufa huweza kuongea ?
Soma 1 Samweli 25:1 na 28:3,11,12,14,15,16
Hivyo inawezekana nafsi ya mtu kuamshwa kutoka huko kuzimu. Lakini kumbuka kinachokufa ni mwili Ila nafsi yake na Roho yake havifi.

Lakini kumbuka ili Vilivyopo katika ulimwengu wa Roho viweze kufanya kazi katika ulimwengu huu vinahitaji mwili huu wa nyama. Hivyo Mungu anamtumia mwanadamu aliyemuumba kufanya makusudi yake na kuuneza ufalme wake hapa duniani pia shetani humtumia mwanadamu kuueneza ufalme wake hapa duniani.

Umeshangaa kuona pepo yakiwatumia ndugu zako kuongea na ninyi?
Mbona hata Mungu hutumia wanadamu kuongea na watu.

Labda nikuongezee kitu Cha kukushangaza zaidi. Je unajua kuwa Mungu anaongea na watu wake Kila siku?
Unajua kuwa Kuna watu wanatokewa na Yesu Kristo na Malaika wa Mungu katika ulimwengu huu na hata hapa Tanzania?
(Hili nililoliandika hapa si la kusimuliwa Bali Ni maisha yangu na familia yangu Kila siku)

Ningeweza kuandika mengi lakini yote yapo kwenye biblia. Ukisoma na ukashindwa kuelewa muulize Mungu atakujibu kikubwa muombe akufungulie masikio na macho yako ya rohoni kwa Jina la Yesu Kristo utamsikia tu. ( Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Isaya 1:18)
 
washonesko

Member
Jun 25, 2016
57
125
Wakuu habari? Naomba nichangie uzoefu wangu nilioushuhudia mwenyewe kwa macho yangu.

Kwenye imani ya Kikristo kuna sehemu imeandikwa" Mtu akifariki haoni, hasikii wala hajui chochote kinachoendelea Duniani" na pia kuna maelezo kwamba unapofariki roho yako inakwenda kwa Mungu moja kwa moja.

Shida yangu ni kwamba, kwenye jamii yetu ya Kihaya kuna kitu wanaita( nchweke) hii ni hali inampata mtu anakuwa kama kapandwa na mashetani lakini inakuwa ni roho ya mtu x aliyeshafariki tayari ambapo mtu huyo anaanza kuongea kwa sauti na rafudhi ya marehemu akikemea au kutoa taarifa ya jambo Fulani.

Nimekuwa nikisikia tu watu wakisimulia hili jambo lakini nikawa naichukulia kama ngano za kiafrika lakini mwaka Jana mwezi wa 12 Babu yetu kipenzi Mzee Cypriani alitutoka. Kama tamaduni zetu zilivyo tulijumuika wote kwenda kijijini kwenye msiba wa Babu hisipokuwa baba Mkubwa ambaye ndo mtoto Mkubwa wa babu alishindwa kufika kwa wakati akipanga kufika mwezi wa kwanza maana kajichimbia machimboni Msumbiji.

Siku ya Mazishi ilipofika tukatoka Malaloni(Makaburini) kumstiri Mzee ile tunafika tu ndani tukiwa kundi kubwa la watu na nyimbo za maombolezo zikitawala gafla Shangazi akadondoka akawa kama amepata kifafa Mara babu Mdogo na baba Mdogo nao wakaanza kama kuweuka. Watu wakaanza kutawanyika ovyoovyo maana ilikuwa ni taflani gafla. Wazee wa ukoo wakakusanyika wakaanza kuchoma majani machanga ya migomba na kuwawekea puani wale waliokabwa na kitu kisichojulikana huku wakiomba kilichowakaba kiongee.
Mara gafla wote watatu wakaanza kuongea kwa pamoja, sauti moja ya babu tuliyetoka kumzika mda huo huo. Akaanza kuwauliza wazee wa ukoo kwamba kwanini wamekubali kumzika bila mtoto wake Mkubwa kufika? Wakajitetea hapo na akawambia siyo kweli kwamba baba Mkubwa hana nauli Bali yuko bize tu na machimbo yake, akasema kabla baba Mkubwa hajafika nyumbani iyo tarehe aliopanga kuja atakuwa ameshamtembelea huko huko msumbiji aliko.

Niachane na iyo stori maana ni ndefu kidogo lakini swali langu ni kitu gani kinatokea kwa watu kama hawa kuweza kupanda juu ya vichwa vya wengine wakati wamekufa tayari? Je roho zao zinakuwa na kitu gani cha kipekee mpaka wawe na uwezo huu maana wengi ni wazee ndo wanaweza kufanya hili.
Hayo ni mashetani
Screenshot_20210705-181414.jpg

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom